Isaya 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 8 (Swahili) Isaiah 8 (English)

Bwana akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa kalamu ya binadamu, Kwa Maher-shalal-hash-bazi; Isaya 8:1

Yahweh said to me, "Take a large tablet, and write on it with a man's pen, 'For Maher Shalal Hash Baz;{"Maher Shalal Hash Baz" means "quick to the plunder, swift to the spoil."}'

nami nitajipatia mashahidi waaminifu ili kuandika habari, yaani, Uria, kuhani, na Zekaria, mwana wa Yeberekia. Isaya 8:2

and I will take to me faithful witnesses to record, Uriah the priest, and Zechariah the son of Jeberechiah.

Nami nikamwendea huyo nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume. Kisha Bwana akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi. Isaya 8:3

I went to the prophetess; and she conceived, and bore a son. Then said Yahweh to me, Call his name Maher Shalal Hash Baz.

Kwa maana kabla mtoto huyo hajapata kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru. Isaya 8:4

For before the child shall have knowledge to cry, My father, and, My mother, the riches of Damascus and the spoil of Samaria shall be carried away before the king of Assyria.

Kisha Bwana akasema nami mara ya pili, akaniambia, Isaya 8:5

Yahweh spoke to me yet again, saying,

Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia, Isaya 8:6

Because this people have refused the waters of Shiloah that go softly, and rejoice in Rezin and Remaliah's son;

basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote; Isaya 8:7

now therefore, behold, the Lord brings up on them the waters of the River, strong and many, [even] the king of Assyria and all his glory: and it shall come up over all its channels, and go over all its banks;

naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli. Isaya 8:8

and it shall sweep onward into Judah; it shall overflow and pass through; it shall reach even to the neck; and the stretching out of its wings shall fill the breadth of your land, Immanuel.

Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande. Isaya 8:9

Make an uproar, O you peoples, and be broken in pieces! And give ear, all you of far countries: gird yourselves, and be broken in pieces! Gird yourselves, and be broken in pieces!

Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi. Isaya 8:10

Take counsel together, and it shall be brought to nothing; speak the word, and it shall not stand: for God is with us.

Maana Bwana aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, Isaya 8:11

For Yahweh spoke thus to me with a strong hand, and instructed me not to walk in the way of this people, saying,

Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. Isaya 8:12

Don't you say, "A conspiracy!" concerning all about which this people shall say, "A conspiracy!" neither fear their fear, nor be in dread [of it].

Bwana wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu. Isaya 8:13

Yahweh of hosts, him shall you sanctify; and let him be your fear, and let him be your dread.

Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. Isaya 8:14

He shall be for a sanctuary; but for a stone of stumbling and for a rock of offense to both the houses of Israel, for a gin and for a snare to the inhabitants of Jerusalem.

Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa. Isaya 8:15

Many shall stumble thereon, and fall, and be broken, and be snared, and be taken.

Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. Isaya 8:16

Bind up the testimony, seal the law among my disciples.

Nami nitamngojea Bwana, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. Isaya 8:17

I will wait for Yahweh, who hides his face from the house of Jacob, and I will look for him.

Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa Bwana wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni. Isaya 8:18

Behold, I and the children whom Yahweh has given me are for signs and for wonders in Israel from Yahweh of Hosts, who dwells in Mount Zion.

Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Isaya 8:19

When they shall tell you, "Consult with those who have familiar spirits and with the wizards, who chirp and who mutter:" shouldn't a people consult with their God? on behalf of the living [should they consult] with the dead?

Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi. Isaya 8:20

To the law and to the testimony! if they don't speak according to this word, surely there is no morning for them.

Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu; Isaya 8:21

They shall pass through it, sore distressed and hungry; and it shall happen that when they shall be hungry, they shall fret themselves, and curse by their king and by their God, and turn their faces upward:

nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa. Isaya 8:22

and they shall look to the earth, and see, distress and darkness, the gloom of anguish; and into thick darkness [they shall be] driven away.