Isaya 56 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 56 (Swahili) Isaiah 56 (English)

Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Isaya 56:1

Thus says Yahweh, Keep you justice, and do righteousness; for my salvation is near to come, and my righteousness to be revealed.

Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote. Isaya 56:2

Blessed is the man who does this, and the son of man who holds it fast; who keeps the Sabbath from profaning it, and keeps his hand from doing any evil.

Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. Isaya 56:3

Neither let the foreigner, who has joined himself to Yahweh, speak, saying, Yahweh will surely separate me from his people; neither let the eunuch say, Behold, I am a dry tree.

Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; Isaya 56:4

For thus says Yahweh of the eunuchs who keep my Sabbaths, and choose the things that please me, and hold fast my covenant:

Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Isaya 56:5

To them will I give in my house and within my walls a memorial and a name better than of sons and of daughters; I will give them an everlasting name, that shall not be cut off.

Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Isaya 56:6

Also the foreigners who join themselves to Yahweh, to minister to him, and to love the name of Yahweh, to be his servants, everyone who keeps the Sabbath from profaning it, and holds fast my covenant;

Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Isaya 56:7

even them will I bring to my holy mountain, and make them joyful in my house of prayer: their burnt offerings and their sacrifices shall be accepted on my altar; for my house shall be called a house of prayer for all peoples.

Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa. Isaya 56:8

The Lord Yahweh, who gathers the outcasts of Israel, says, Yet will I gather [others] to him, besides his own who are gathered.

Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni. Isaya 56:9

All you animals of the field, come to devour, [yes], all you animals in the forest.

Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. Isaya 56:10

His watchmen are blind, they are all without knowledge; they are all mute dogs, they can't bark; dreaming, lying down, loving to slumber.

Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote. Isaya 56:11

Yes, the dogs are greedy, they can never have enough; and these are shepherds who can't understand: they have all turned to their own way, each one to his gain, from every quarter.

Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi. Isaya 56:12

Come you, [say they], I will get wine, and we will fill ourselves with strong drink; and tomorrow shall be as this day, [a day] great beyond measure.