Isaya 27 Swahili & English
Listen/Download AudioIsaya 27 (Swahili) | Isaiah 27 (English) |
---|---|
Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. Isaya 27:1 |
In that day Yahweh with his hard and great and strong sword will punish leviathan the swift serpent, and leviathan the crooked serpent; and he will kill the monster that is in the sea. |
Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni. Isaya 27:2 |
In that day: A vineyard of wine, sing you to it. |
Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda. Isaya 27:3 |
I Yahweh am its keeper; I will water it every moment: lest any hurt it, I will keep it night and day. |
Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja. Isaya 27:4 |
Wrath is not in me: would that the briers and thorns were against me in battle! I would march on them, I would burn them together. |
Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami. Isaya 27:5 |
Or else let him take hold of my strength, that he may make peace with me; [yes], let him make peace with me. |
Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda. Isaya 27:6 |
In days to come shall Jacob take root; Israel shall blossom and bud; and they shall fill the surface of the world with fruit. |
Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye? Isaya 27:7 |
Has he struck them as he struck those who struck them? or are they slain according to the slaughter of those who were slain by them? |
Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. Isaya 27:8 |
In measure, when you send them away, you do contend with them; he has removed [them] with his rough blast in the day of the east wind. |
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena. Isaya 27:9 |
Therefore by this shall the iniquity of Jacob be forgiven, and this is all the fruit of taking away his sin: that he makes all the stones of the altar as chalk stones that are beaten in sunder, [so that] the Asherim and the sun-images shall rise no more. |
Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake. Isaya 27:10 |
For the fortified city is solitary, a habitation deserted and forsaken, like the wilderness: there shall the calf feed, and there shall he lie down, and consume the branches of it. |
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe. Isaya 27:11 |
When the boughs of it are withered, they shall be broken off; the women shall come, and set them on fire; for it is a people of no understanding: therefore he who made them will not have compassion on them, and he who formed them will show them no favor. |
Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli. Isaya 27:12 |
It shall happen in that day, that Yahweh will beat off [his fruit] from the flood of the River to the brook of Egypt; and you shall be gathered one by one, you children of Israel. |
Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu. Isaya 27:13 |
It shall happen in that day, that a great trumpet shall be blown; and they shall come who were ready to perish in the land of Assyria, and those who were outcasts in the land of Egypt; and they shall worship Yahweh in the holy mountain at Jerusalem. |