1 Samweli 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 18 (Swahili) 1st Samuel 18 (English)

Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. 1 Samweli 18:1

It happened, when he had made an end of speaking to Saul, that the soul of Jonathan was knit with the soul of David, and Jonathan loved him as his own soul.

Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 1 Samweli 18:2

Saul took him that day, and would let him go no more home to his father's house.

Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 1 Samweli 18:3

Then Jonathan and David made a covenant, because he loved him as his own soul.

Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake. 1 Samweli 18:4

Jonathan stripped himself of the robe that was on him, and gave it to David, and his clothing, even to his sword, and to his bow, and to his sash.

Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia. 1 Samweli 18:5

David went out wherever Saul sent him, [and] behaved himself wisely: and Saul set him over the men of war, and it was good in the sight of all the people, and also in the sight of Saul's servants.

Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 1 Samweli 18:6

It happened as they came, when David returned from the slaughter of the Philistine, that the women came out of all the cities of Israel, singing and dancing, to meet king Saul, with tambourines, with joy, and with instruments of music.

Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 1 Samweli 18:7

The women sang one to another as they played, and said, Saul has slain his thousands, David his ten thousands.

Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 1 Samweli 18:8

Saul was very angry, and this saying displeased him; and he said, They have ascribed to David ten thousands, and to me they have ascribed but thousands: and what can he have more but the kingdom?

Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 1 Samweli 18:9

Saul eyed David from that day and forward.

Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 1 Samweli 18:10

It happened on the next day, that an evil spirit from God came mightily on Saul, and he prophesied in the midst of the house: and David played with his hand, as he did day by day. Saul had his spear in his hand;

Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. 1 Samweli 18:11

and Saul cast the spear; for he said, I will strike David even to the wall. David avoided out of his presence twice.

Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli. 1 Samweli 18:12

Saul was afraid of David, because Yahweh was with him, and was departed from Saul.

Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe akida wake juu ya askari elfu; naye akatoka na kuingia mbele ya watu. 1 Samweli 18:13

Therefore Saul removed him from him, and made him his captain over a thousand; and he went out and came in before the people.

Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye. 1 Samweli 18:14

David behaved himself wisely in all his ways; and Yahweh was with him.

Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa. 1 Samweli 18:15

When Saul saw that he behaved himself very wisely, he stood in awe of him.

Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao. 1 Samweli 18:16

But all Israel and Judah loved David; for he went out and came in before them.

Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya Bwana. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake. 1 Samweli 18:17

Saul said to David, Behold, my elder daughter Merab, her will I give you as wife: only be valiant for me, and fight Yahweh's battles. For Saul said, Don't let my hand be on him, but let the hand of the Philistines be on him.

Naye Daudi akamwambia Sauli, Mimi ni nani, na jamaa zangu ni akina nani, au mbari ya babangu, katika Israeli, hata mimi niwe mkwewe mfalme? 1 Samweli 18:18

David said to Saul, Who am I, and what is my life, [or] my father's family in Israel, that I should be son-in-law to the king?

Lakini ikawa, wakati ule, ilipopasa Daudi apewe Merabu, binti Sauli, aliolewa na Adrieli, Mmeholathi. 1 Samweli 18:19

But it happened at the time when Merab, Saul's daughter, should have been given to David, that she was given to Adriel the Meholathite as wife.

Walakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi; watu wakamwambia Sauli, na neno hilo likampendeza. 1 Samweli 18:20

Michal, Saul's daughter, loved David: and they told Saul, and the thing pleased him.

Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu. 1 Samweli 18:21

Saul said, I will give her to him, that she may be a snare to him, and that the hand of the Philistines may be against him. Therefore Saul said to David, You shall this day be my son-in-law a second time.

Naye Sauli akawaagiza watumishi wake, Zungumzeni na Daudi kwa siri, na kusema, Angalia, mfalme anakuridhia, na watumishi wake wote wanakupenda; haya basi! Na uwe mkwewe mfalme. 1 Samweli 18:22

Saul commanded his servants, [saying], Commune with David secretly, and say, Behold, the king has delight in you, and all his servants love you: now therefore be the king's son-in-law.

Nao watumishi wa Sauli wakanena maneno hayo masikioni mwa Daudi. Daudi akasema, Je! Ninyi mwaona kuwa ni shani mimi kuwa mkwewe mfalme, nami ni maskini, tena sina cheo? 1 Samweli 18:23

Saul's servants spoke those words in the ears of David. David said, Seems it to you a light thing to be the king's son-in-law, seeing that I am a poor man, and lightly esteemed?

Na hao watumishi wa Sauli wakampasha habari, wakisema, Ndivyo hivyo alivyosema Daudi. 1 Samweli 18:24

The servants of Saul told him, saying, On this manner spoke David.

Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti. 1 Samweli 18:25

Saul said, Thus shall you tell David, The king desires no dowry except one hundred foreskins of the Philistines, to be avenged of the king's enemies. Now Saul thought to make David fall by the hand of the Philistines.

Na watumishi wake walipomwambia Daudi; maneno hayo, ilimpendeza Daudi sana kuwa mkwewe mfalme. Na siku zilikuwa hazijaisha bado; 1 Samweli 18:26

When his servants told David these words, it pleased David well to be the king's son-in-law. The days were not expired;

basi Daudi akainuka, akaenda yeye na watu wake, akaua katika Wafilisti watu mia mbili; na Daudi akazileta govi zao, wakampa mfalme hesabu kamili, ili awe mkwewe mfalme. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake. 1 Samweli 18:27

and David arose and went, he and his men, and killed of the Philistines two hundred men; and David brought their foreskins, and they gave them in full number to the king, that he might be the king's son-in-law. Saul gave him Michal his daughter as wife.

Sauli akaona na kutambua ya kwamba Bwana alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda. 1 Samweli 18:28

Saul saw and knew that Yahweh was with David; and Michal, Saul's daughter, loved him.

Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote. 1 Samweli 18:29

Saul was yet the more afraid of David; and Saul was David's enemy continually.

Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu. 1 Samweli 18:30

Then the princes of the Philistines went forth: and it happened, as often as they went forth, that David behaved himself more wisely than all the servants of Saul; so that his name was much set by.