1 Samweli 30 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 30 (Swahili) 1st Samuel 30 (English)

Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 1 Samweli 30:1

It happened, when David and his men were come to Ziklag on the third day, that the Amalekites had made a raid on the South, and on Ziklag, and had struck Ziklag, and burned it with fire,

nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. 1 Samweli 30:2

and had taken captive the women [and all] who were therein, both small and great: they didn't kill any, but carried them off, and went their way.

Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. 1 Samweli 30:3

When David and his men came to the city, behold, it was burned with fire; and their wives, and their sons, and their daughters, were taken captive.

Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. 1 Samweli 30:4

Then David and the people who were with him lifted up their voice and wept, until they had no more power to weep.

Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. 1 Samweli 30:5

David's two wives were taken captive, Ahinoam the Jezreelitess, and Abigail the wife of Nabal the Carmelite.

Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. 1 Samweli 30:6

David was greatly distressed; for the people spoke of stoning him, because the soul of all the people was grieved, every man for his sons and for his daughters: but David strengthened himself in Yahweh his God.

Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 1 Samweli 30:7

David said to Abiathar the priest, the son of Ahimelech, Please bring me here the ephod. Abiathar brought there the ephod to David.

Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. 1 Samweli 30:8

David inquired of Yahweh, saying, If I pursue after this troop, shall I overtake them? He answered him, Pursue; for you shall surely overtake [them], and shall without fail recover [all].

Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. 1 Samweli 30:9

So David went, he and the six hundred men who were with him, and came to the brook Besor, where those who were left behind stayed.

Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. 1 Samweli 30:10

But David pursued, he and four hundred men; for two hundred stayed behind, who were so faint that they couldn't go over the brook Besor.

Nao wakamkuta Mmisri mavueni, wakamleta kwa Daudi, na kumpa chakula, naye akala; nao wakampa maji ya kunywa; 1 Samweli 30:11

They found an Egyptian in the field, and brought him to David, and gave him bread, and he ate; and they gave him water to drink.

kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana alikuwa hakula chakula wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku. 1 Samweli 30:12

They gave him a piece of a cake of figs, and two clusters of raisins: and when he had eaten, his spirit came again to him; for he had eaten no bread, nor drunk any water, three days and three nights.

Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani; nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na ugonjwa. 1 Samweli 30:13

David said to him, To whom belong you? and whence are you? He said, I am a young man of Egypt, servant to an Amalekite; and my master left me, because three days ago I fell sick.

Sisi tulishambulia Negebu ya Wakerethi, na ya milki ya Yuda, na Negebu ya Kalebu; na huo mji wa Siklagi tukauchoma moto. 1 Samweli 30:14

We made a raid on the South of the Cherethites, and on that which belongs to Judah, and on the South of Caleb; and we burned Ziklag with fire.

Daudi akamwambia, Je! Wewe utaniongoza chini hata nilifikilie jeshi hilo? Naye akasema, Uniapie kwa Mungu, ya kwamba hutaniua, wala kunitia mikononi mwa huyo bwana wangu, nami nitakuongoza chini hata kulifikilia jeshi hilo. 1 Samweli 30:15

David said to him, Will you bring me down to this troop? He said, Swear to me by God, that you will neither kill me, nor deliver me up into the hands of my master, and I will bring you down to this troop.

Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 1 Samweli 30:16

When he had brought him down, behold, they were spread abroad over all the ground, eating and drinking, and dancing, because of all the great spoil that they had taken out of the land of the Philistines, and out of the land of Judah.

Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 1 Samweli 30:17

David struck them from the twilight even to the evening of the next day: and there not a man of them escaped, except four hundred young men, who rode on camels and fled.

Daudi akawapokonya wote waliokuwa wamechukuliwa na Waamaleki; naye Daudi akawaokoa wakeze wawili. 1 Samweli 30:18

David recovered all that the Amalekites had taken; and David rescued his two wives.

Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote. 1 Samweli 30:19

There was nothing lacking to them, neither small nor great, neither sons nor daughters, neither spoil, nor anything that they had taken to them: David brought back all.

Naye Daudi akatwaa makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambao waliwatanguliza mbele ya wanyama wale wengine, wakasema, Hao ndio nyara za Daudi. 1 Samweli 30:20

David took all the flocks and the herds, [which] they drove before those [other] cattle, and said, This is David's spoil.

Kisha Daudi aliwafikilia wale watu mia mbili, waliokuwa wametaka kuzimia, hata wasiweze kumfuata Daudi, wale waliowaacha wakae karibu na kijito cha Besori; nao wakatoka nje ili kumlaki Daudi, na kuwalaki hao watu waliokuwa pamoja naye, naye Daudi alipowakaribia hao watu, aliwasalimu. 1 Samweli 30:21

David came to the two hundred men, who were so faint that they could not follow David, whom also they had made to abide at the brook Besor; and they went forth to meet David, and to meet the people who were with him: and when David came near to the people, he greeted them.

Ndipo watu waovu wote na wale wasiofaa, miongoni mwa hao waliokwenda pamoja na Daudi, wakasema, Kwa kuwa watu hawa hawakuenda pamoja na sisi, hatutawapa kitu cho chote katika hizo nyara tulizozitwaa tena, isipokuwa kila mtu atapewa mkewe na watoto wake, wawachukue na kwenda zao. 1 Samweli 30:22

Then answered all the wicked men and base fellows, of those who went with David, and said, Because they didn't go with us, we will not give them anything of the spoil that we have recovered, except to every man his wife and his children, that he may lead them away, and depart.

Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa Bwana, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu. 1 Samweli 30:23

Then said David, You shall not do so, my brothers, with that which Yahweh has given to us, who has preserved us, and delivered the troop that came against us into our hand.

Tena ni nani atakayewasikiliza ninyi katika jambo hili? Kwa kuwa kama lilivyo fungu lake yeye ashukaye vitani, ndivyo litakavyokuwa na fungu lake huyo akaaye karibu na vyombo; watagawiwa sawasawa. 1 Samweli 30:24

Who will listen to you in this matter? for as his share is who goes down to the battle, so shall his share be who tarries by the baggage: they shall share alike.

Basi ikawa hivyo tangu siku ile na baadaye; akaiweka iwe amri na agizo la Israeli hata leo. 1 Samweli 30:25

It was so from that day forward, that he made it a statute and an ordinance for Israel to this day.

Basi Daudi alipofika Siklagi, aliwapelekea wazee wa Yuda, rafiki zake, sehemu ya nyara, akasema, Angalieni, zawadi yenu katika nyara za adui za Bwana; 1 Samweli 30:26

When David came to Ziklag, he sent of the spoil to the elders of Judah, even to his friends, saying, Behold, a present for you of the spoil of the enemies of Yahweh:

yaani, kwa hao wa Betheli, na kwa hao wa Ramoth-Negebu, na kwa hao wa Yatiri; 1 Samweli 30:27

To those who were in Bethel, and to those who were in Ramoth of the South, and to those who were in Jattir,

na kwa hao wa Aroeri, na kwa hao wa Sifmothi, na kwa hao wa Eshtemoa; 1 Samweli 30:28

and to those who were in Aroer, and to those who were in Siphmoth, and to those who were in Eshtemoa,

na kwa hao wa Rakali, na kwa hao wa miji ya Wayerameeli, na kwa hao wa miji ya Wakeni; 1 Samweli 30:29

and to those who were in Racal, and to those who were in the cities of the Jerahmeelites, and to those who were in the cities of the Kenites,

na kwa hao wa Horma, na kwa hao wa Korashani, na kwa hao wa Athaki; 1 Samweli 30:30

and to those who were in Hormah, and to those who were in Borashan, and to those who were in Athach,

na kwa hao wa Hebroni, na kwa hao wa kila mahali alipozoelea Daudi mwenyewe na watu wake. 1 Samweli 30:31

and to those who were in Hebron, and to all the places where David himself and his men used to stay.