1 Samweli 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 26 (Swahili) 1st Samuel 26 (English)

Basi hao Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kuelekea Yeshimoni? 1 Samweli 26:1

The Ziphites came to Saul to Gibeah, saying, Doesn't David hide himself in the hill of Hachilah, which is before the desert?

Basi Sauli akaondoka, akashuka nyikani kwa Zifu, naye alikuwa na watu elfu tatu, wateule wa Israeli, pamoja naye, ili kumtafuta Daudi katika nyika ya Zifu. 1 Samweli 26:2

Then Saul arose, and went down to the wilderness of Ziph, having three thousand chosen men of Israel with him, to seek David in the wilderness of Ziph.

Naye Sauli akapiga hema katika kilima cha Hakila, kilichoelekea Yeshimoni, barabarani; lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, akaona ya kwamba Sauli amemfuata mpaka nyikani. 1 Samweli 26:3

Saul encamped in the hill of Hachilah, which is before the desert, by the way. But David abode in the wilderness, and he saw that Saul came after him into the wilderness.

Basi Daudi akatuma wapelelezi, akapata habari ya hakika ya kwamba Sauli amefika. 1 Samweli 26:4

David therefore sent out spies, and understood that Saul was come of a certainty.

Daudi akainuka, akafika mahali pale alipotua Sauli; Daudi akapaangalia mahali alipolala Sauli, na Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi lake; naye Sauli alikuwa amelala kati ya magari, na hao watu wamepiga hema zao wakimzunguka. 1 Samweli 26:5

David arose, and came to the place where Saul had encamped; and David saw the place where Saul lay, and Abner the son of Ner, the captain of his host: and Saul lay within the place of the wagons, and the people were encamped round about him.

Ndipo Daudi akajibu, akamwambia Ahimeleki, Mhiti, na Abishai, mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, akisema, Ni nani atakayeshuka pamoja nami kwa Sauli kambini? Abishai akasema, Mimi nitashuka pamoja nawe. 1 Samweli 26:6

Then answered David and said to Ahimelech the Hittite, and to Abishai the son of Zeruiah, brother to Joab, saying, Who will go down with me to Saul to the camp? Abishai said, I will go down with you.

Basi Daudi na Abishai wakawaendea watu usiku; na tazama, Sauli alikuwapo kati ya magari amelala usingizi, na fumo lake limechomekwa chini, karibu na kichwa chake; naye Abneri na watu wake wamelala wakimzunguka. 1 Samweli 26:7

So David and Abishai came to the people by night: and, behold, Saul lay sleeping within the place of the wagons, with his spear stuck in the ground at his head; and Abner and the people lay round about him.

Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hata nchi kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili. 1 Samweli 26:8

Then said Abishai to David, God has delivered up your enemy into your hand this day: now therefore please let me strike him with the spear to the earth at one stroke, and I will not strike him the second time.

Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi 1 Samweli 26:9

David said to Abishai, Don't destroy him; for who can put forth his hand against Yahweh's anointed, and be guiltless?

Daudi akasema, Aishivyo Bwana, Bwana atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea. 1 Samweli 26:10

David said, As Yahweh lives, Yahweh will strike him; or his day shall come to die; or he shall go down into battle and perish.

Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi 1 Samweli 26:11

Yahweh forbid that I should put forth my hand against Yahweh's anointed: but now please take the spear that is at his head, and the jar of water, and let us go.

Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia. 1 Samweli 26:12

So David took the spear and the jar of water from Saul's head; and they got them away: and no man saw it, nor knew it, neither did any awake; for they were all asleep, because a deep sleep from Yahweh was fallen on them.

Kisha Daudi akaenda ng'ambo ya pili, akasimama juu ya kilima, mbali sana; palipokuwapo nafasi tele katikati yao; 1 Samweli 26:13

Then David went over to the other side, and stood on the top of the mountain afar off; a great space being between them;

naye Daudi akawapigia kelele watu wale, na Abneri, mwana wa Neri, akasema, Abneri, hujibu? Ndipo Abneri akajibu, akasema, U nani wewe unayemlilia mfalme? 1 Samweli 26:14

and David cried to the people, and to Abner the son of Ner, saying, Don't you answer, Abner? Then Abner answered, Who are you who cries to the king?

Naye Daudi akamwambia Abneri, Wewe si mtu shujaa? Tena ni nani aliye sawa na wewe katika Israeli? Mbona, basi, hukumlinda bwana wako, huyo mfalme? Kwa maana mtu mmoja aliingia ili amwangamize mfalme, bwana wako? 1 Samweli 26:15

David said to Abner, Aren't you a [valiant] man? and who is like you in Israel? why then have you not kept watch over your lord, the king? for there came one of the people in to destroy the king your lord.

Jambo hili ulilolitenda si jema. Aishivyo Bwana, mmestahili kufa, kwa sababu hamkumlinda bwana wenu, masihi*fq* wa Bwana. Haya basi! Tazameni, liko wapi fumo la mfalme, na gudulia la maji lililokuwa kichwani pake? 1 Samweli 26:16

This thing isn't good that you have done. As Yahweh lives, you are worthy to die, because you have not kept watch over your lord, Yahweh's anointed. Now see where the king's spear is, and the jar of water that was at his head.

Naye Sauli akaitambua sauti ya Daudi, akasema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Daudi akasema, Ndiyo, ni sauti yangu, bwana wangu, mfalme. 1 Samweli 26:17

Saul knew David's voice, and said, Is this your voice, my son David? David said, It is my voice, my lord, O king.

Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu? 1 Samweli 26:18

He said, Why does my lord pursue after his servant? for what have I done? or what evil is in my hand?

Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni Bwana aliyekuondokesha juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za Bwana; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa Bwana, wakisema, Enenda, katumikie miungu mingine. 1 Samweli 26:19

Now therefore, please let my lord the king hear the words of his servant. If it be Yahweh that has stirred you up against me, let him accept an offering: but if it be the children of men, cursed be they before Yahweh: for they have driven me out this day that I shouldn't cling to Yahweh's inheritance, saying, Go, serve other gods.

Basi sasa, isianguke damu yangu chini mbali na uso wa Bwana; maana mfalme wa Israeli ametoka ili kutafuta uhai wangu, kama vile mtu awindavyo kware mlimani. 1 Samweli 26:20

Now therefore, don't let my blood fall to the earth away from the presence of Yahweh: for the king of Israel is come out to seek a flea, as when one does hunt a partridge in the mountains.

Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana. 1 Samweli 26:21

Then said Saul, I have sinned: return, my son David; for I will no more do you harm, because my life was precious in your eyes this day: behold, I have played the fool, and have erred exceedingly.

Daudi akajibu, akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja na avukie huku, alitwae. 1 Samweli 26:22

David answered, Behold the spear, O king! let then one of the young men come over and get it.

Naye Bwana atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana Bwana amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA. 1 Samweli 26:23

Yahweh will render to every man his righteousness and his faithfulness; because Yahweh delivered you into my hand today, and I wouldn't put forth my hand against Yahweh's anointed.

Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa Bwana, akaniokoe katika shida zote. 1 Samweli 26:24

Behold, as your life was much set by this day in my eyes, so let my life be much set by in the eyes of Yahweh, and let him deliver me out of all oppression.

Ndipo Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao. 1 Samweli 26:25

Then Saul said to David, Blessed be you, my son David: you shall both do mightily, and shall surely prevail. So David went his way, and Saul returned to his place.