1 Samweli 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 2 (Swahili) 1st Samuel 2 (English)

Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; 1 Samweli 2:1

Hannah prayed, and said: My heart exults in Yahweh; My horn is exalted in Yahweh; My mouth is enlarged over my enemies; Because I rejoice in your salvation.

Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. 1 Samweli 2:2

There is none holy as Yahweh; For there is none besides you, Neither is there any rock like our God.

Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. 1 Samweli 2:3

Talk no more so exceeding proudly; Don't let arrogance come out of your mouth; For Yahweh is a God of knowledge, By him actions are weighed.

Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. 1 Samweli 2:4

The bows of the mighty men are broken; Those who stumbled are girded with strength.

Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. 1 Samweli 2:5

Those who were full have hired out themselves for bread; Those who were hungry have ceased [to hunger]: Yes, the barren has borne seven; She who has many children languishes.

Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. 1 Samweli 2:6

Yahweh kills, and makes alive: He brings down to Sheol, and brings up.

Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. 1 Samweli 2:7

Yahweh makes poor, and makes rich: He brings low, he also lifts up.

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. 1 Samweli 2:8

He raises up the poor out of the dust, He lifts up the needy from the dunghill, To make them sit with princes, Inherit the throne of glory: For the pillars of the earth are Yahweh's, He has set the world on them.

Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; 1 Samweli 2:9

He will keep the feet of his holy ones; But the wicked shall be put to silence in darkness; For by strength shall no man prevail.

Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake. 1 Samweli 2:10

Those who strive with Yahweh shall be broken to pieces; Against them will he thunder in the sky: Yahweh will judge the ends of the earth; He will give strength to his king, Exalt the horn of his anointed.

Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia Bwana mbele yake Eli, kuhani. 1 Samweli 2:11

Elkanah went to Ramah to his house. The child did minister to Yahweh before Eli the priest.

Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali Bwana, 1 Samweli 2:12

Now the sons of Eli were base men; they didn't know Yahweh.

wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu ye yote alipotoa dhabihu wakati wo wote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake; 1 Samweli 2:13

The custom of the priests with the people was that when any man offered sacrifice, the priest's servant came, while the flesh was boiling, with a flesh-hook of three teeth in his hand;

naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko. 1 Samweli 2:14

and he struck it into the pan, or kettle, or caldron, or pot; all that the flesh-hook brought up the priest took therewith. So they did in Shiloh to all the Israelites who came there.

Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi. 1 Samweli 2:15

Yes, before they burnt the fat, the priest's servant came, and said to the man who sacrificed, Give flesh to roast for the priest; for he will not have boiled flesh of you, but raw.

Tena, ikiwa mtu yule amwambia, Hawakosi wataichoma moto hayo mafuta kwanza, kisha utwae kadiri roho yako itakavyopenda; ndipo husema, Sivyo, lakini sharti unipe sasa hivi; la, hunipi, basi nitaitwaa kwa nguvu. 1 Samweli 2:16

If the man said to him, They will surely burn the fat first, and then take as much as your soul desires; then he would say, No, but you shall give it me now: and if not, I will take it by force.

Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa Bwana; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya Bwana. 1 Samweli 2:17

The sin of the young men was very great before Yahweh; for the men despised the offering of Yahweh.

Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za Bwana, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani. 1 Samweli 2:18

But Samuel ministered before Yahweh, being a child, girded with a linen ephod.

Tena mamaye humfanyizia kanzu ndogo, na kumletea mwaka kwa mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. 1 Samweli 2:19

Moreover his mother made him a little robe, and brought it to him from year to year, when she came up with her husband to offer the yearly sacrifice.

Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, Bwana na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa Bwana. Kisha wakaenda nyumbani kwao. 1 Samweli 2:20

Eli blessed Elkanah and his wife, and said, Yahweh give you seed of this woman for the petition which was asked of Yahweh. They went to their own home.

Naye Bwana akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za Bwana. 1 Samweli 2:21

Yahweh visited Hannah, and she conceived, and bore three sons and two daughters. The child Samuel grew before Yahweh.

Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 1 Samweli 2:22

Now Eli was very old; and he heard all that his sons did to all Israel, and how that they lay with the women who served at the door of the tent of meeting.

Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. 1 Samweli 2:23

He said to them, Why do you such things? for I hear of your evil dealings from all this people.

Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana. 1 Samweli 2:24

No, my sons; for it is no good report that I hear: you make Yahweh's people to disobey.

Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua. 1 Samweli 2:25

If one man sin against another, God shall judge him; but if a man sin against Yahweh, who shall entreat for him? Notwithstanding, they didn't listen to the voice of their father, because Yahweh was minded to kill them.

Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia. 1 Samweli 2:26

The child Samuel grew on, and increased in favor both with Yahweh, and also with men.

Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, Bwana asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao? 1 Samweli 2:27

There came a man of God to Eli, and said to him, Thus says Yahweh, Did I reveal myself to the house of your father, when they were in Egypt [in bondage] to Pharaoh's house?

Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto? 1 Samweli 2:28

and did I choose him out of all the tribes of Israel to be my priest, to go up to my altar, to burn incense, to wear an ephod before me? and did I give to the house of your father all the offerings of the children of Israel made by fire?

Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema? 1 Samweli 2:29

Why kick you at my sacrifice and at my offering, which I have commanded in [my] habitation, and honor your sons above me, to make yourselves fat with the best of all the offerings of Israel my people?

Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. 1 Samweli 2:30

Therefore Yahweh, the God of Israel, says, I said indeed that your house, and the house of your father, should walk before me forever: but now Yahweh says, Be it far from me; for those who honor me I will honor, and those who despise me shall be lightly esteemed.

Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. 1 Samweli 2:31

Behold, the days come, that I will cut off your arm, and the arm of your father's house, that there shall not be an old man in your house.

Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. 1 Samweli 2:32

You shall see the affliction of [my] habitation, in all the wealth which [God] shall give Israel; and there shall not be an old man in your house forever.

Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa watu wazima. 1 Samweli 2:33

The man of yours, [whom] I shall not cut off from my altar, [shall be] to consume your eyes, and to grieve your heart; and all the increase of your house shall die in the flower of their age.

Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; watakufa wote wawili katika siku moja. 1 Samweli 2:34

This shall be the sign to you, that shall come on your two sons, on Hophni and Phinehas: in one day they shall die both of them.

Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele. 1 Samweli 2:35

I will raise me up a faithful priest, that shall do according to that which is in my heart and in my mind: and I will build him a sure house; and he shall walk before my anointed forever.

Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali unitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate. 1 Samweli 2:36

It shall happen, that everyone who is left in your house shall come and bow down to him for a piece of silver and a loaf of bread, and shall say, Please put me into one of the priests' offices, that I may eat a morsel of bread.