Waamuzi 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 20 (Swahili) Judges 20 (English)

Ndipo wana wa Israeli walipotoka; na mkutano ukakutanika kama mtu mmoja, kutoka Dani hata Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi wakamkutanikia Bwana huko Mispa. Waamuzi 20:1

Then all the children of Israel went out, and the congregation was assembled as one man, from Dan even to Beersheba, with the land of Gilead, to Yahweh at Mizpah.

Hao wakuu wa watu, maana wakuu wa kabila zote za Israeli, wakajihudhurisha katika huo mkutano wa watu wa Mungu, watu waume mia nne elfu waendao kwa miguu, wenye kutumia upanga. Waamuzi 20:2

The chiefs of all the people, even of all the tribes of Israel, presented themselves in the assembly of the people of God, four hundred thousand footmen who drew sword.

Basi wana wa Benyamini walipata habari ya kuwa wana wa Israeli wamekwea kwenda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, Tuambieni huo uovu ulikuwaje kutendeka? Waamuzi 20:3

(Now the children of Benjamin heard that the children of Israel had gone up to Mizpah.) The children of Israel said, Tell us, how was this wickedness brought to pass?

Huyo Mlawi, huyo mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu na kusema, Mimi nilifikilia Gibea ulio wa Benyamini mimi na suria yangu, ili tulale. Waamuzi 20:4

The Levite, the husband of the woman who was murdered, answered, I came into Gibeah that belongs to Benjamin, I and my concubine, to lodge.

Nao watu waume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walidhani kuniua, na suria wangu wakamtenza nguvu, hata amekufa. Waamuzi 20:5

The men of Gibeah rose against me, and beset the house round about me by night; me they thought to have slain, and my concubine they forced, and she is dead.

Basi nikamtwaa huyo suria yangu, na kumkata vipande, na kumpeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli; kwa sababu wametenda maovu makuu na upumbavu katika Israeli. Waamuzi 20:6

I took my concubine, and cut her in pieces, and sent her throughout all the country of the inheritance of Israel; for they have committed lewdness and folly in Israel.

Angalieni, ninyi wana wa Israeli nyote, sasa toeni maneno na mashauri yenu. Waamuzi 20:7

Behold, you children of Israel, all of you, give here your advice and counsel.

Basi watu hao wote waliinuka kama mtu mmoja, wakisema, Hatutakwenda, hata mmoja, hemani kwake, wala hatutaondoka, hata mmoja, kwenda nyumbani kwake. Waamuzi 20:8

All the people arose as one man, saying, We will not any of us go to his tent, neither will we any of us turn to his house.

Lakini jambo tutakalowatenda watu wa Gibea ni hili; tutakwea kwa kura kwenda kuupiga; Waamuzi 20:9

But now this is the thing which we will do to Gibeah: [we will go up] against it by lot;

nasi tutatwaa watu kumi katika mia katika kabila zote za Israeli, na watu mia katika elfu, na watu elfu katika elfu kumi, ili waende kuwatwalia watu vyakula, ili kwamba, hapo watakapofika Gibea ya Benyamini wapate kutenda mfano wa upumbavu huo wote walioutenda wao katika Israeli. Waamuzi 20:10

and we will take ten men of one hundred throughout all the tribes of Israel, and one hundred of one thousand, and a thousand out of ten thousand, to get food for the people, that they may do, when they come to Gibeah of Benjamin, according to all the folly that they have worked in Israel.

Basi waume wote wa Israeli walikutana pamoja juu ya mji huo, walikuwa wanashikamana pamoja kama mtu mmoja. Waamuzi 20:11

So all the men of Israel were gathered against the city, knit together as one man.

Kisha kabila za Israeli wakatuma watu waende katika kabila yote ya Benyamini, wakasema, Je! Ni uovu gani huu uliokuwa kati yenu? Waamuzi 20:12

The tribes of Israel sent men through all the tribe of Benjamin, saying, What wickedness is this that is happen among you?

Basi sasa watoeni watu hao, hao mabaradhuli walio katika Gibea, ili kwamba tupate kuwaua, na kuuondoa uovu katika Israeli. Lakini Benyamini hawakukubali kuisikia sauti ya ndugu zao wana wa Israeli. Waamuzi 20:13

Now therefore deliver up the men, the base fellows, who are in Gibeah, that we may put them to death, and put away evil from Israel. But Benjamin would not listen to the voice of their brothers the children of Israel.

Lakini wana wa Benyamini wakakutanika huko Gibea kutoka katika miji yao, ili watoke kwenda kupiga vita juu ya wana wa Israeli. Waamuzi 20:14

The children of Benjamin gathered themselves together out of the cities to Gibeah, to go out to battle against the children of Israel.

Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, watu waume ishirini na sita elfu waliotumia upanga, zaidi ya hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba. Waamuzi 20:15

The children of Benjamin were numbered on that day out of the cities twenty-six thousand men who drew the sword, besides the inhabitants of Gibeah, who were numbered seven hundred chosen men.

Katika watu hao wote walikuwako watu waume mia saba waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa teo, wala asikose. Waamuzi 20:16

Among all this people there were seven hundred chosen men left-handed; everyone could sling stones at a hair-breadth, and not miss.

Nao watu wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, walihesabiwa kuwa ni watu waume mia nne elfu, wenye kutumia upanga; hao wote walikuwa ni watu wa vita. Waamuzi 20:17

The men of Israel, besides Benjamin, were numbered four hundred thousand men who drew sword: all these were men of war.

Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? Bwana akawaambia, Yuda atakwea kwanza. Waamuzi 20:18

The children of Israel arose, and went up to Bethel, and asked counsel of God; and they said, Who shall go up for us first to battle against the children of Benjamin? Yahweh said, Judah [shall go up] first.

Basi wana wa Israeli waliondoka asubuhi, wakapanga hema zao juu ya Gibea. Waamuzi 20:19

The children of Israel rose up in the morning, and encamped against Gibeah.

Watu wa Israeli walitoka ili wapigane na Benyamini; nao watu wa Israeli wakaviandaa vita juu yao huko Gibea. Waamuzi 20:20

The men of Israel went out to battle against Benjamin; and the men of Israel set the battle in array against them at Gibeah.

Wana wa Benyamini wakatoka Gibea, wakaangamiza hata nchi watu ishirini na mbili elfu katika Israeli siku hiyo. Waamuzi 20:21

The children of Benjamin came forth out of Gibeah, and destroyed down to the ground of the Israelites on that day Twenty-two thousand men.

Lakini watu hao, watu wa Israeli, walijitia nguvu, wakaviandaa vile vita mara ya pili mahali pale walipojiandaa siku ya kwanza. Waamuzi 20:22

The people, the men of Israel, encouraged themselves, and set the battle again in array in the place where they set themselves in array the first day.

Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za Bwana hata jioni; wakamwuliza Bwana, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? Bwana akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye. Waamuzi 20:23

The children of Israel went up and wept before Yahweh until even; and they asked of Yahweh, saying, Shall I again draw near to battle against the children of Benjamin my brother? Yahweh said, Go up against him.

Basi wana wa Israeli wakakaribia juu ya wana wa Benyamini siku ya pili. Waamuzi 20:24

The children of Israel came near against the children of Benjamin the second day.

Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea siku ya pili, wakaangamiza hata nchi watu kumi na nane elfu tena katika watu wa Israeli; hao wote walikuwa wenye kutumia upanga. Waamuzi 20:25

Benjamin went forth against them out of Gibeah the second day, and destroyed down to the ground of the children of Israel again eighteen thousand men; all these drew the sword.

Ndipo wana Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za Bwana, wakafunga siku hiyo hata jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana. Waamuzi 20:26

Then all the children of Israel, and all the people, went up, and came to Bethel, and wept, and sat there before Yahweh, and fasted that day until even; and they offered burnt-offerings and peace-offerings before Yahweh.

Kisha wana wa Israeli wakauliza kwa Bwana (kwa sababu sanduku la agano la Mungu lilikuwako huko siku hizo, Waamuzi 20:27

The children of Israel asked of Yahweh (for the ark of the covenant of God was there in those days,

na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anasimama mbele ya hilo sanduku siku hizo), wakasema, Je! Nitoke tena niende kupigana na wana wa Benyamini ndugu yangu, au niache? Bwana akawaambia, Haya, kweeni; kwa kuwa kesho nitamtoa na kumtia mkononi mwako. Waamuzi 20:28

and Phinehas, the son of Eleazar, the son of Aaron, stood before it in those days), saying, Shall I yet again go out to battle against the children of Benjamin my brother, or shall I cease? Yahweh said, Go up; for tomorrow I will deliver him into your hand.

Basi Israeli akaweka watu wavizie kinyume cha Gibea kuuzunguka pande zote. Waamuzi 20:29

Israel set liers-in-wait against Gibeah round about.

Basi wana wa Israeli wakakwea kwenda kupigana na wana wa Benyamini siku ya tatu, wakajipanga ili kupigana na Gibea, kama walivyofanya nyakati nyingine. Waamuzi 20:30

The children of Israel went up against the children of Benjamin on the third day, and set themselves in array against Gibeah, as at other times.

Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kupiga na kuua katika hao watu, wapata kama watu thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika hizo njia kuu, ambazo njia mojawapo huendelea Betheli, na njia ya pili huendelea Gibea, katika shamba. Waamuzi 20:31

The children of Benjamin went out against the people, and were drawn away from the city; and they began to strike and kill of the people, as at other times, in the highways, of which one goes up to Bethel, and the other to Gibeah, in the field, about thirty men of Israel.

Wana wa Benyamini wakasema, Wamepigwa mbele yetu kama kwanza. Lakini wana wa Israeli wakasema, Haya, na tukimbie, na kuwavuta wauache mji waende katika njia kuu. Waamuzi 20:32

The children of Benjamin said, They are struck down before us, as at the first. But the children of Israel said, Let us flee, and draw them away from the city to the highways.

Basi hao watu wote wa Israeli wakaondoka mahali pao wakajipanga huko Baal-tamari; na hao wenye kuvizia wa Israeli wakatoka mahali hapo walipokuwa, hata Maare-geba. Waamuzi 20:33

All the men of Israel rose up out of their place, and set themselves in array at Baal Tamar: and the liers-in-wait of Israel broke forth out of their place, even out of Maareh Geba.

Kisha watu elfu kumi waliochaguliwa katika Israeli wote wakaja juu ya Gibea, na vile vita vilikuwa vikali sana; lakini hawakujua ya kuwa uovu ulikuwa karibu nao. Waamuzi 20:34

There came over against Gibeah ten thousand chosen men out of all Israel, and the battle was sore; but they didn't know that evil was close on them.

Bwana akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza watu waume ishirini na tano elfu na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga. Waamuzi 20:35

Yahweh struck Benjamin before Israel; and the children of Israel destroyed of Benjamin that day twenty-five thousand one hundred men: all these drew the sword.

Basi wana wa Benyamini waliona kuwa wamepigwa; kwa kuwa watu wa Israeli wakaondoka mbele ya Benyamini, kwa sababu walikuwa wanawatumaini hao wenye kuvizia waliokuwa wamewaweka kinyume cha Gibea. Waamuzi 20:36

So the children of Benjamin saw that they were struck; for the men of Israel gave place to Benjamin, because they trusted to the liers-in-wait whom they had set against Gibeah.

Hao wenye kuvizia wakafanya haraka, wakaurukia Gibea; na hao wenye kuvizia wakaenda wakaupiga huo mji wote kwa makali ya upanga. Waamuzi 20:37

The liers-in-wait hurried, and rushed on Gibeah; and the liers-in-wait drew themselves along, and struck all the city with the edge of the sword.

Basi hiyo ishara iliyoaganwa kati ya watu wa Israeli na hao wenye kuvizia ilikuwa ni hii, kwamba wafanye lipande wingu kubwa la moshi kutoka katika huo mji. Waamuzi 20:38

Now the appointed sign between the men of Israel and the liers-in-wait was that they should make a great cloud of smoke rise up out of the city.

Nao watu wa Israeli walipogeuka katika vile vita, Benyamini naye akaanza kupiga na kuwaua watu wa Israeli kama watu thelathini; kwani walisema, Hakika yetu wamepigwa mbele yetu, vile vile kama katika vile vita vya kwanza. Waamuzi 20:39

The men of Israel turned in the battle, and Benjamin began to strike and kill of the men of Israel about thirty persons; for they said, Surely they are struck down before us, as in the first battle.

Lakini hapo hilo wingu lilipoanza kupanda kutoka katika mji, kama nguzo ya moshi, ndipo Wabenyamini wakaangalia nyuma, na tazama, huo mji mzima ulikuwa wapaa juu katika moshi kwenda mbinguni. Waamuzi 20:40

But when the cloud began to arise up out of the city in a pillar of smoke, the Benjamites looked behind them; and, behold, the whole of the city went up in smoke to the sky.

Ndipo watu wa Israeli wakageuka, na watu wa Benyamini walisitushwa; kwa kuwa waliona ya kwamba wamefikiliwa na uovu. Waamuzi 20:41

The men of Israel turned, and the men of Benjamin were dismayed; for they saw that evil had come on them.

Kwa hiyo wakageuza maungo yao mbele ya wana wa Israeli kuelekea njia ya kwenda nyikani; lakini vile vita vikawaandamia kwa kasi; na hao waliotoka katika ile miji wakawaangamiza katikati yake. Waamuzi 20:42

Therefore they turned their backs before the men of Israel to the way of the wilderness; but the battle followed hard after them; and those who came out of the cities destroyed them in the midst of it.

Waliwazingira Wabenyamini pande zote na kuwafukuza, na kuwakanyaga-kanyaga hapo walipopumzika, hata kufikilia Gibea upande wa maawio ya jua. Waamuzi 20:43

They enclosed the Benjamites round about, [and] chased them, [and] trod them down at [their] resting-place, as far as over against Gibeah toward the sunrise.

Wakaanguka watu wa Benyamini watu kumi na nane elfu, hao wote walikuwa ni watu waume mashujaa. Waamuzi 20:44

There fell of Benjamin eighteen thousand men; all these [were] men of valor.

Kisha wakageuka na kukimbia upande wa nyika hata kulifikilia jabali la Rimoni; nao wakaokota katika watu hao katika njia kuu watu waume elfu tano; wakawaandamia kwa kasi mpaka Gidomu, nako wakawapiga wengine wao watu elfu mbili. Waamuzi 20:45

They turned and fled toward the wilderness to the rock of Rimmon: and they gleaned of them in the highways five thousand men, and followed hard after them to Gidom, and struck of them two thousand men.

Basi jumla ya watu wa Benyamini walioanguka siku ile walikuwa ni watu ishirini na tano elfu waliokuwa wanatumia upanga; wote hao walikuwa ni watu mashujaa. Waamuzi 20:46

So that all who fell that day of Benjamin were twenty-five thousand men who drew the sword; all these [were] men of valor.

Lakini watu waume mia sita wakageuka, wakakimbia upande wa nyikani mpaka jabali la Rimoni, wakakaa kwenye hilo jabali la Rimoni muda wa miezi minne. Waamuzi 20:47

But six hundred men turned and fled toward the wilderness to the rock of Rimmon, and abode in the rock of Rimmon four months.

Kisha watu wa Israeli wakageuka tena kuwaendea wana wa Benyamini, wakawapiga kwa makali ya upanga, huo mji mzima, na hao wanyama wa mji, na kila kitu walichokiona; tena miji yote waliyoiona wakaitia moto. Waamuzi 20:48

The men of Israel turned again on the children of Benjamin, and struck them with the edge of the sword, both the entire city, and the cattle, and all that they found: moreover all the cities which they found they set on fire.