Waamuzi 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 18 (Swahili) Judges 18 (English)

Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila ya Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hata siku hiyo urithi wao haujawaangukia kati ya kabila za Israeli. Waamuzi 18:1

In those days there was no king in Israel: and in those days the tribe of the Danites sought them an inheritance to dwell in; for to that day [their] inheritance had not fallen to them among the tribes of Israel.

Basi wana wa Dani wakatuma watu wa jamaa zao, watu watano katika hesabu yao yote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuiaua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hata nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko. Waamuzi 18:2

The children of Dan sent of their family five men from their whole number, men of valor, from Zorah, and from Eshtaol, to spy out the land, and to search it; and they said to them, Go, search the land. They came to the hill-country of Ephraim, to the house of Micah, and lodged there.

Basi hapo walipokuwa karibu na nyumba ya Mika, wakatambua sauti yake huyo hirimu, huyo Mlawi; ndipo wakageuka wakaenda kuko, na kumwuliza, Je! Ni nani aliyekuleta wewe huku? Nawe wafanya nini mahali hapa? Una kazi gani hapa? Waamuzi 18:3

When they were by the house of Micah, they knew the voice of the young man the Levite; and they turned aside there, and said to him, Who brought you here? and what do you in this place? and what have you here?

Naye akawaambia, Hivi na hivi ndivyo alivyonifanyia Mika, ameniajiri, nami nimekuwa kuhani wake. Waamuzi 18:4

He said to them, Thus and thus has Micah dealt with me, and he has hired me, and I am become his priest.

Nao wakamwambia, Tafadhali tutakie shauri la Mungu, ili tupate kujua kwamba njia yetu tuiendeayo itafanikiwa. Waamuzi 18:5

They said to him, Ask counsel, we pray you, of God, that we may know whether our way which we go shall be prosperous.

Kuhani akawaambia, Haya endeni na amani; njia mnayoiendea i mbele za Bwana. Waamuzi 18:6

The priest said to them, Go in peace: before Yahweh is your way wherein you go.

Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa salama salimini kwa mfano wa walivyokaa hao Wasidoni, wenye starehe na hifadhi, kwa maana hapakuwa na mtu katika nchi hiyo aliyekuwa na amri, aliyeweza kuwatweza katika neno lo lote, nao walikuwa wa mbali na hao Wasidoni, wala hawakuwa na shughuli na mtu ye yote. Waamuzi 18:7

Then the five men departed, and came to Laish, and saw the people who were therein, how they lived in security, after the manner of the Sidonians, quiet and secure; for there was none in the land, possessing authority, that might put [them] to shame in anything, and they were far from the Sidonians, and had no dealings with any man.

Kisha wakawarudia ndugu zao huko Sora na Eshtaoli; ndugu zao wakawauliza; Haya, mna habari gani? Waamuzi 18:8

They came to their brothers to Zorah and Eshtaol: and their brothers said to them, What [say] you?

Wakasema, Haya, inukeni, twende tukapigane nao; kwa maana tumeiona hiyo nchi nayo ni nchi nzuri sana; nanyi, je! Mwanyamaa tu? Msiwe wavivu kwenda, na kuingia, ili mpate kuimiliki nchi hiyo. Waamuzi 18:9

They said, Arise, and let us go up against them; for we have seen the land, and, behold, it is very good: and are you still? don't be slothful to go and to enter in to possess the land.

Hapo mtakapokwenda mtawafikilia watu wakaao salama salimini, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapana kupungukiwa na kitu cho chote kilicho duniani. Waamuzi 18:10

When you go, you shall come to a people secure, and the land is large; for God has given it into your hand, a place where there is no want of anything that is in the earth.

Basi wakatoka hapo watu mia sita waliovaa silaha za vita, wa jamaa ya Wadani, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli. Waamuzi 18:11

There set forth from there of the family of the Danites, out of Zorah and out of Eshtaol, six hundred men girt with weapons of war.

Wakakwea juu na kupiga kambi huko Kiriath-yearimu, katika Yuda; kwa sababu hiyo wakapaita mahali pale jina lake Mahane-dani hata hivi leo; tazama, ni hapo nyuma ya Kiriath-yearimu. Waamuzi 18:12

They went up, and encamped in Kiriath Jearim, in Judah: therefore they called that place Mahaneh-dan, to this day; behold, it is behind Kiriath Jearim.

Nao wakapita huko hata hiyo nchi ya vilima vilima ya Efraimu, wakafikilia nyumba ya huyo Mika. Waamuzi 18:13

They passed there to the hill-country of Ephraim, and came to the house of Micah.

Ndipo hao watu watano waliokwenda kuipeleleza nchi ya Laisha wakajibu, na kuwaambia ndugu zao Je! Ninyi mwajua ya kwamba mna naivera ndani ya nyumba hizi, na kinyago na sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Basi sasa fikirini iwapasayo kufanya. Waamuzi 18:14

Then the five men who went to spy out the country of Laish answered, and said to their brothers, Do you know that there is in these houses an ephod, and teraphim, and an engraved image, and a molten image? now therefore consider what you have to do.

Basi wakageuka wakaenda kuko, wakafikilia nyumba ya huyo hirimu, Mlawi, hata hiyo nyumba ya Mika, nao wakamwuliza habari za hali yake. Waamuzi 18:15

They turned aside there, and came to the house of the young man the Levite, even to the house of Micah, and asked him of his welfare.

Hao watu mia sita wenye kuvaa silaha zao za vita, waliokuwa ni wana wa Dani, wakasimama penye maingilio ya lango. Waamuzi 18:16

The six hundred men girt with their weapons of war, who were of the children of Dan, stood by the entrance of the gate.

Na hao watu watano waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi wakakwea juu, wakaingia ndani, na kuitwaa hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu; na huyo kuhani akasimama penye maingilio ya lango pamoja na hao watu waume sita mia wenye kuvaa silaha za vita. Waamuzi 18:17

The five men who went to spy out the land went up, and came in there, and took the engraved image, and the ephod, and the teraphim, and the molten image: and the priest stood by the entrance of the gate with the six hundred men girt with weapons of war.

Nao hapo walipoingia ndani ya nyumba ya Mika, na kuileta hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu, huyo kuhani akawauliza, Je! Mwafanya nini ninyi? Waamuzi 18:18

When these went into Micah's house, and fetched the engraved image, the ephod, and the teraphim, and the molten image, the priest said to them, What do you?

Wao wakamwambia, Nyamaza wewe, weka mkono wako kinywani mwako, uende pamoja nasi, uwe kwetu baba, tena kuhani; je! Ni vema kwako kuwa kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuwa kuhani kwa ajili ya kabila na jamaa katika Israeli? Waamuzi 18:19

They said to him, Hold your peace, lay your hand on your mouth, and go with us, and be to us a father and a priest: is it better for you to be priest to the house of one man, or to be priest to a tribe and a family in Israel?

Huyo kuhani moyo wake ukafurahi, naye akaitwaa hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kuchonga, akaenda katikati ya hao watu. Waamuzi 18:20

The priest's heart was glad, and he took the ephod, and the teraphim, and the engraved image, and went in the midst of the people.

Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa mifugo, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao. Waamuzi 18:21

So they turned and departed, and put the little ones and the cattle and the goods before them.

Walipokuwa wamekwenda kitambo kizima kutoka nyumba ya Mika, wale watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na nyumba ya Mika walikutana, wakawaandama na kuwapata hao wana wa Dani. Waamuzi 18:22

When they were a good way from the house of Micah, the men who were in the houses near to Micah's house were gathered together, and overtook the children of Dan.

Wakawapigia kelele wana wa Dani. Nao wakageuza nyuso zao na kumwambia Mika, Una nini wewe, hata ukaja na mkutano namna hii? Waamuzi 18:23

They cried to the children of Dan. They turned their faces, and said to Micah, What ails you, that you come with such a company?

Akasema, Ninyi mmeichukua miungu niliyoifanya, na huyo kuhani, nanyi mmekwenda zenu, nami nina nini tena? Basi imekuwaje ninyi kuniuliza, Una nini wewe? Waamuzi 18:24

He said, you have taken away my gods which I made, and the priest, and are gone away, and what have I more? and how then say you to me, What ails you?

Hao wana wa Dani wakamwambia, Hiyo sauti yako isisikiwe kati yetu, wasije walio na hasira wakakuangukia, nawe ukapotewa na uhai wako, pamoja na uhai wa watu wa nyumbani mwako. Waamuzi 18:25

The children of Dan said to him, "Don't let your voice be heard among us, lest angry fellows fall on you, and you lose your life, with the lives of your household."

Basi wana wa Dani wakaenda zao; naye Mika alipoona ya kuwa ni wenye nguvu kumshinda yeye, akageuka akarudi nyumbani kwake. Waamuzi 18:26

The children of Dan went their way: and when Micah saw that they were too strong for him, he turned and went back to his house.

Nao wakakitwaa hicho alichokuwa amekifanya Mika, na kuhani aliyekuwa naye nao wakafikilia Laisha, kwenye watu waliokuwa wenye starehe na hifadhi, wakawapiga kwa makali ya upanga; wakaupiga moto mji wao. Waamuzi 18:27

They took that which Micah had made, and the priest whom he had, and came to Laish, to a people quiet and secure, and struck them with the edge of the sword; and they burnt the city with fire.

Wala hakuwako mwokozi, kwa sababu huo mji ulikuwa ni mbali sana na Sidoni, nao hawakuwa na shughuli na mtu awaye yote; na mji huo ulikuwa katika hilo bonde lililo karibu na Bethrehobu. Nao wakaujenga huo mji na kukaa humo. Waamuzi 18:28

There was no deliverer, because it was far from Sidon, and they had no dealings with any man; and it was in the valley that lies by Beth Rehob. They built the city, and lived therein.

Wakauita mji jina lake Dani, kwa kuliandama jina la baba yao Dani, aliyezaliwa kwake Israeli; lakini jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Laisha. Waamuzi 18:29

They called the name of the city Dan, after the name of Dan their father, who was born to Israel: however the name of the city was Laish at the first.

Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga; na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni makuhani katika kabila ya Wadani hata siku ya kuchukuliwa mateka hiyo nchi. Waamuzi 18:30

The children of Dan set up for themselves the engraved image: and Jonathan, the son of Gershom, the son of Moses, he and his sons were priests to the tribe of the Danites until the day of the captivity of the land.

Basi wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga aliyoifanya Mika, wakati wote ile nyumba ya Mungu ilipokuwako huko Shilo.

Waamuzi 18:31

So they set them up Micah's engraved image which he made, all the time that the house of God was in Shiloh.