Waamuzi 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 7 (Swahili) Judges 7 (English)

Kisha Yerubaali, yaani Gideoni, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka na mapema, wakapiga kambi yao karibu na kijito cha Harodi; na kambi ya Midiani ilikuwa upande wao wa kaskazini, karibu na mlima wa More, bondeni. Waamuzi 7:1

Then Jerubbaal, who is Gideon, and all the people who were with him, rose up early, and encamped beside the spring of Harod: and the camp of Midian was on the north side of them, by the hill of Moreh, in the valley.

Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. Waamuzi 7:2

Yahweh said to Gideon, The people who are with you are too many for me to give the Midianites into their hand, lest Israel vaunt themselves against me, saying, My own hand has saved me.

Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi. Waamuzi 7:3

Now therefore proclaim in the ears of the people, saying, Whoever is fearful and trembling, let him return and depart from Mount Gilead. There returned of the people twenty-two thousand; and there remained ten thousand.

Bwana akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda. Waamuzi 7:4

Yahweh said to Gideon, The people are yet too many; bring them down to the water, and I will try them for you there: and it shall be, that of whom I tell you, This shall go with you, the same shall go with you; and of whoever I tell you, This shall not go with you, the same shall not go.

Basi akawaleta watu chini majini. Bwana akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa. Waamuzi 7:5

So he brought down the people to the water: and Yahweh said to Gideon, Everyone who laps of the water with his tongue, as a dog laps, him shall you set by himself; likewise everyone who bows down on his knees to drink.

Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji. Waamuzi 7:6

The number of those who lapped, putting their hand to their mouth, was three hundred men: but all the rest of the people bowed down on their knees to drink water.

Bwana akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake. Waamuzi 7:7

Yahweh said to Gideon, By the three hundred men who lapped will I save you, and deliver the Midianites into your hand; and let all the people go every man to his place.

Basi wale watu wakachukua vyakula vyao mikononi mwao, na tarumbeta zao; naye akawapeleka watu wote wa Israeli, kila mtu hemani kwake; bali aliwazuia wale watu mia tatu; na kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake, bondeni. Waamuzi 7:8

So the people took food in their hand, and their trumpets; and he sent all the men of Israel every man to his tent, but retained the three hundred men: and the camp of Midian was beneath him in the valley.

Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako. Waamuzi 7:9

It happened the same night, that Yahweh said to him, Arise, get you down into the camp; for I have delivered it into your hand.

Lakini, ukiogopa kushuka, shuka pamoja na Pura mtumishi wako kambini; Waamuzi 7:10

But if you fear to go down, go you with Purah your servant down to the camp:

nawe utasikia wanayoyasema, na baada ya haya mikono yako itatiwa nguvu; ushuke kambini. Ndipo akashuka pamoja na Pura mtumishi wake hata kufikilia mwisho wa watu wenye silaha waliokuwa kambini. Waamuzi 7:11

and you shall hear what they say; and afterward shall your hands be strengthened to go down into the camp. Then went he down with Purah his servant to the outermost part of the armed men who were in the camp.

Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia zao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi. Waamuzi 7:12

The Midianites and the Amalekites and all the children of the east lay along in the valley like locusts for multitude; and their camels were without number, as the sand which is on the sea-shore for multitude.

Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini. Waamuzi 7:13

When Gideon had come, behold, there was a man telling a dream to his fellow; and he said, Behold, I dreamed a dream; and, behold, a cake of barley bread tumbled into the camp of Midian, and came to the tent, and struck it so that it fell, and turned it upside down, so that the tent lay flat.

Mwenzake akamjibu akasema, Habari hii haikosi kuwa upanga wa Gideoni, mwana wa Yoashi, mtu wa Israeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote katika mkono wake. Waamuzi 7:14

His fellow answered, This is nothing else save the sword of Gideon the son of Joash, a man of Israel: into his hand God has delivered Midian, and all the host.

Ikawa, aliposikia habari ya ile ndoto, na kufasiriwa kwake, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana Bwana amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu. Waamuzi 7:15

It was so, when Gideon heard the telling of the dream, and the interpretation of it, that he worshiped; and he returned into the camp of Israel, and said, Arise; for Yahweh has delivered into your hand the host of Midian.

Kisha akawapanga wale watu mia tatu wawe vikosi vitatu, akatia tarumbeta katika mikono ya watu wote, na mitungi isiyo maji, na mienge ndani ya hiyo mitungi. Waamuzi 7:16

He divided the three hundred men into three companies, and he put into the hands of all of them trumpets, and empty pitchers, with torches within the pitchers.

Akawaambia, Nitazameni, mkafanye kama nifanyavyo mimi; angalieni, nitakapofika mwisho wa kambi, itakuwa, nifanyavyo mimi nanyi fanyeni kadhalika. Waamuzi 7:17

He said to them, Look on me, and do likewise: and, behold, when I come to the outermost part of the camp, it shall be that, as I do, so shall you do.

Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa Bwana, na kwa Gideoni. Waamuzi 7:18

When I blow the trumpet, I and all who are with me, then blow you the trumpets also on every side of all the camp, and say, For Yahweh and for Gideon.

Basi Gideoni, na wale watu mia waliokuwa pamoja naye, wakafika mwisho wa kambi, mwanzo wa zamu ya kati, wakati walipokuwa wamebadili wenye zamu; wakazipiga hizo tarumbeta, wakaivunja vipande vipande ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. Waamuzi 7:19

So Gideon, and the hundred men who were with him, came to the outermost part of the camp in the beginning of the middle watch, when they had but newly set the watch: and they blew the trumpets, and broke in pieces the pitchers that were in their hands.

Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa Bwana na wa Gideoni. Waamuzi 7:20

The three companies blew the trumpets, and broke the pitchers, and held the torches in their left hands, and the trumpets in their right hands with which to blow; and they cried, The sword of Yahweh and of Gideon.

Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote; jeshi lote wakakimbia; nao wakapiga kelele, wakawakimbiza. Waamuzi 7:21

They stood every man in his place round about the camp; and all the host ran; and they shouted, and put [them] to flight.

Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye Bwana akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi. Waamuzi 7:22

They blew the three hundred trumpets, and Yahweh set every man's sword against his fellow, and against all the host; and the host fled as far as Beth-shittah toward Zererah, as far as the border of Abel Meholah, by Tabbath.

Wanaume wa Israeli walikuwa wamekusanyika kutoka Naftali, na kutoka Asheri, na kutoka Manase yote, wakawafuata Midiani. Waamuzi 7:23

The men of Israel were gathered together out of Naphtali, and out of Asher, and out of all Manasseh, and pursued after Midian.

Kisha Gideoni akapeleka wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, telemkeni juu ya Midiani, na kuyashika hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. Basi watu waume wote wa Efraimu walikutana pamoja, wakayashika maji mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. Waamuzi 7:24

Gideon sent messengers throughout all the hill-country of Ephraim, saying, Come down against Midian, and take before them the waters, as far as Beth Barah, even the Jordan. So all the men of Ephraim were gathered together, and took the waters as far as Beth Barah, even the Jordan.

Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng'ambo ya pili ya Yordani. Waamuzi 7:25

They took the two princes of Midian, Oreb and Zeeb; and they killed Oreb at the rock of Oreb, and Zeeb they killed at the winepress of Zeeb, and pursued Midian: and they brought the heads of Oreb and Zeeb to Gideon beyond the Jordan.