Waamuzi 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 6 (Swahili) Judges 6 (English)

Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana; Bwana akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba Waamuzi 6:1

The children of Israel did that which was evil in the sight of Yahweh: and Yahweh delivered them into the hand of Midian seven years.

Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome. Waamuzi 6:2

The hand of Midian prevailed against Israel; and because of Midian the children of Israel made them the dens which are in the mountains, and the caves, and the strongholds.

Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakakwea juu yao; Waamuzi 6:3

So it was, when Israel had sown, that the Midianites came up, and the Amalekites, and the children of the east; they came up against them;

wakapanga marago juu yao, na kuyaharibu hayo maongeo ya nchi, hata ufikapo Gaza, wala hawakuacha katika Israeli riziki ziwazo zote; kondoo, wala ng'ombe, wala punda. Waamuzi 6:4

and they encamped against them, and destroyed the increase of the earth, until you come to Gaza, and left no sustenance in Israel, neither sheep, nor ox, nor donkey.

Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu. Waamuzi 6:5

For they came up with their cattle and their tents; they came in as locusts for multitude; both they and their camels were without number: and they came into the land to destroy it.

Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana. Waamuzi 6:6

Israel was brought very low because of Midian; and the children of Israel cried to Yahweh.

Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Midiani, Waamuzi 6:7

It happened, when the children of Israel cried to Yahweh because of Midian,

Bwana akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli; naye akawaambia, Bwana, yeye Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi niliwaleta ninyi mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa; Waamuzi 6:8

that Yahweh sent a prophet to the children of Israel: and he said to them, Thus says Yahweh, the God of Israel, I brought you up from Egypt, and brought you forth out of the house of bondage;

nami niliwaokoa na mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao; Waamuzi 6:9

and I delivered you out of the hand of the Egyptians, and out of the hand of all who oppressed you, and drove them out from before you, and gave you their land;

kisha niliwaambia, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; msiiche miungu ya Waamori, ambayo mwaketi katika nchi yao; lakini hamkuitii sauti yangu. Waamuzi 6:10

and I said to you, I am Yahweh your God; you shall not fear the gods of the Amorites, in whose land you dwell. But you have not listened to my voice.

Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. Waamuzi 6:11

The angel of Yahweh came, and sat under the oak which was in Ophrah, that pertained to Joash the Abiezrite: and his son Gideon was beating out wheat in the winepress, to hide it from the Midianites.

Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. Waamuzi 6:12

The angel of Yahweh appeared to him, and said to him, Yahweh is with you, you mighty man of valor.

Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. Waamuzi 6:13

Gideon said to him, Oh, my lord, if Yahweh is with us, why then has all this happened to us? and where are all his wondrous works which our fathers told us of, saying, Did not Yahweh bring us up from Egypt? but now Yahweh has cast us off, and delivered us into the hand of Midian.

Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? Waamuzi 6:14

Yahweh looked at him, and said, Go in this your might, and save Israel from the hand of Midian: have not I sent you?

Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. Waamuzi 6:15

He said to him, Oh, Lord, with which shall I save Israel? behold, my family is the poorest in Manasseh, and I am the least in my father's house.

Bwana akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. Waamuzi 6:16

Yahweh said to him, Surely I will be with you, and you shall strike the Midianites as one man.

Naye akamwambia, Kama nimepata kibali mbele za macho yako, basi unionyeshe ishara, ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami. Waamuzi 6:17

He said to him, If now I have found favor in your sight, then show me a sign that it is you who talk with me.

Tafadhali, usiondoke hapa hata nikujie, nikatoe zawadi yangu, na kuiweka mbele zako. Akasema, Nitangoja hata utakaporudi. Waamuzi 6:18

Please don't go away, until I come to you, and bring out my present, and lay it before you. He said, I will wait until you come again.

Basi Gideoni akaingia ndani, akaandaa mwana-mbuzi, na mikate isiyotiwa chachu, ya efa ya unga; akaitia ile nyama katika kikapu, akautia mchuzi katika nyungu, akamletea hapo nje chini ya mwaloni, akampa. Waamuzi 6:19

Gideon went in, and made ready a kid, and unleavened cakes of an ephah of meal: the flesh he put in a basket, and he put the broth in a pot, and brought it out to him under the oak, and presented it.

Naye malaika wa Mungu akamwambia, Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uiweke juu ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo. Waamuzi 6:20

The angel of God said to him, Take the flesh and the unleavened cakes, and lay them on this rock, and pour out the broth. He did so.

Ndipo malaika wa Bwana akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; malaika wa Bwana akaondoka mbele ya macho yake. Waamuzi 6:21

Then the angel of Yahweh put forth the end of the staff that was in his hand, and touched the flesh and the unleavened cakes; and there went up fire out of the rock, and consumed the flesh and the unleavened cakes; and the angel of Yahweh departed out of his sight.

Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso. Waamuzi 6:22

Gideon saw that he was the angel of Yahweh; and Gideon said, Alas, Lord Yahweh! because I have seen the angel of Yahweh face to face.

Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa. Waamuzi 6:23

Yahweh said to him, Peace be to you; don't be afraid: you shall not die.

Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. Waamuzi 6:24

Then Gideon built an altar there to Yahweh, and called it Yahweh-shalom: to this day it is yet in Ophrah of the Abiezrites.

Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; Waamuzi 6:25

It happened the same night, that Yahweh said to him, Take your father's bull, even the second bull seven years old, and throw down the altar of Baal that your father has, and cut down the Asherah that is by it;

ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. Waamuzi 6:26

and build an altar to Yahweh your God on the top of this stronghold, in the orderly manner, and take the second bull, and offer a burnt offering with the wood of the Asherah which you shall cut down.

Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. Waamuzi 6:27

Then Gideon took ten men of his servants, and did as Yahweh had spoken to him: and it happened, because he feared his father's household and the men of the city, so that he could not do it by day, that he did it by night.

Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. Waamuzi 6:28

When the men of the city arose early in the morning, behold, the altar of Baal was broken down, and the Asherah was cut down that was by it, and the second bull was offered on the altar that was built.

Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. Waamuzi 6:29

They said one to another, Who has done this thing? When they inquired and asked, they said, Gideon the son of Joash has done this thing.

Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo. Waamuzi 6:30

Then the men of the city said to Joash, Bring out your son, that he may die, because he has broken down the altar of Baal, and because he has cut down the Asherah that was by it.

Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake. Waamuzi 6:31

Joash said to all who stood against him, Will you contend for Baal? Or will you save him? he who will contend for him, let him be put to death while [it is yet] morning: if he be a god, let him contend for himself, because one has broken down his altar.

Basi akamwita Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake. Waamuzi 6:32

Therefore on that day he named him Jerubbaal, saying, Let Baal contend against him, because he has broken down his altar.

Wakati huo Wamidiani na Waamaleki, na hao wana wa mashariki walikutana pamoja; wakavuka na kupanga hema zao katika bonde la Yezreeli. Waamuzi 6:33

Then all the Midianites and the Amalekites and the children of the east assembled themselves together; and they passed over, and encamped in the valley of Jezreel.

Lakini roho ya Bwana ikaja juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata. Waamuzi 6:34

But the Spirit of Yahweh came on Gideon; and he blew a trumpet; and Abiezer was gathered together after him.

Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote; wao nao walikutana pamoja ili kumfuata; kisha akatuma wajumbe waende kwa Asheri, na kwa Zabuloni, na kwa Naftali; nao wakakwea ili kumlaki. Waamuzi 6:35

He sent messengers throughout all Manasseh; and they also were gathered together after him: and he sent messengers to Asher, and to Zebulun, and to Naphtali; and they came up to meet them.

Gideoni akamwambia Mungu, Ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema, Waamuzi 6:36

Gideon said to God, If you will save Israel by my hand, as you have spoken,

tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema. Waamuzi 6:37

behold, I will put a fleece of wool on the threshing floor; if there be dew on the fleece only, and it be dry on all the ground, then shall I know that you will save Israel by my hand, as you have spoken.

Ikawa hivyo; kwa maana aliondoka asubuhi na mapema, akaikamua ile ngozi, akautoa ule umande katika ile ngozi, bakuli zima la maji. Waamuzi 6:38

It was so; for he rose up early on the next day, and pressed the fleece together, and wrung the dew out of the fleece, a bowl full of water.

Gideoni akamwambia Mungu, Hasira yako isiwake juu yangu, nami nitasema mara hii tu; nakuomba, nijaribu kwa ngozi hii mara hii tu; sasa ngozi tu na iwe kavu, na uwe umande juu ya nchi yote. Waamuzi 6:39

Gideon said to God, Don't let your anger be kindled against me, and I will speak but this once: Please let me make a trial just this once with the fleece; let it now be dry only on the fleece, and on all the ground let there be dew.

Mungu akafanya hivyo usiku ule; maana ile ngozi tu ilikuwa kavu, napo palikuwa na umande juu ya nchi yote. Waamuzi 6:40

God did so that night: for it was dry on the fleece only, and there was dew on all the ground.