Waamuzi 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 19 (Swahili) Judges 19 (English)

Ikawa katika siku hizo, hapo kulipokuwa hapana mfalme katika Israeli, alikuwapo Mlawi mmoja aliyekuwa akikaa hali ya ugeni upande wa mbele wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu, aliyejitwalia suria katika Bethlehemu-yuda. Waamuzi 19:1

It happened in those days, when there was no king in Israel, that there was a certain Levite sojourning on the farther side of the hill-country of Ephraim, who took to him a concubine out of Bethlehem Judah.

Kisha huyo suria yake akaandama ukahaba kinyume chake, kumwacha kwenda nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu-yuda, akakaa kuko muda wa miezi minne. Waamuzi 19:2

His concubine played the prostitute against him, and went away from him to her father's house to Bethlehem Judah, and was there the space of four months.

Kisha mumewe akainuka akamfuata, aseme naye kwa upendo, ili apate kumrudisha tena, naye alikuwa na mtumishi wake pamoja naye na punda wawili; huyo mwanamke akamkaribisha katika nyumba ya baba yake; naye baba yake alipomwona akafurahi kuonana naye. Waamuzi 19:3

Her husband arose, and went after her, to speak kindly to her, to bring her again, having his servant with him, and a couple of donkeys: and she brought him into her father's house; and when the father of the young lady saw him, he rejoiced to meet him.

Kisha mkwewe, babaye huyo mwanamke, akamzuia; akakaa naye siku tatu; basi wakala na kunywa na kulala kuko. Waamuzi 19:4

His father-in-law, the young lady's father, retained him; and he abode with him three days: so they ate and drink, and lodged there.

Kisha ilikuwa siku ya nne, wakaamka asubuhi na mapema, naye akaondoka ili aende zake; baba yake huyo mwanamke akamwambia mkwewe, Tuza moyo wako, ule chakula kidogo, kisha baadaye mtakwenda zenu. Waamuzi 19:5

It happened on the fourth day, that they arose early in the morning, and he rose up to depart: and the young lady's father said to his son-in-law, Strengthen your heart with a morsel of bread, and afterward you shall go your way.

Basi wakaketi, wakala na kunywa wote wawili pamoja; kisha baba yake mwanamke akamwambia huyo mtu, Uwe radhi, tafadhali, ukae usiku kucha, na moyo wako na ufurahi. Waamuzi 19:6

So they sat down, and ate and drink, both of them together: and the young lady's father said to the man, Please be pleased to stay all night, and let your heart be merry.

Yule mtu akainuka ili aondoke; lakini mkwewe akamsihi-sihi, naye akalala kuko tena. Waamuzi 19:7

The man rose up to depart; but his father-in-law urged him, and he lodged there again.

Basi akaamka asubuhi na mapema siku ya tano ili aende zake; na baba yake mwanamke akasema, Tuza moyo wako, tafadhali, ukae hata jua lipinduke; nao wakala chakula wote wawili. Waamuzi 19:8

He arose early in the morning on the fifth day to depart; and the young lady's father said, Please strengthen your heart and stay until the day declines; and they ate, both of them.

Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria yake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu. Waamuzi 19:9

When the man rose up to depart, he, and his concubine, and his servant, his father-in-law, the young lady's father, said to him, Behold, now the day draws toward evening, please stay all night: behold, the day grows to an end, lodge here, that your heart may be merry; and tomorrow get you early on your way, that you may go home.

Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda wawili waliotandikwa; suria yake naye alikuwa pamoja naye. Waamuzi 19:10

But the man wouldn't stay that night, but he rose up and departed, and came over against Jebus (the same is Jerusalem): and there were with him a couple of donkeys saddled; his concubine also was with him.

Basi hapo walipokuwa karibu na Yebusi, mchana ulikuwa umeendelea mno; yule mtumishi akamwambia bwana wake, Haya, tafadhali, tugeuke kando na kuingia mji huu wa Wayebusi, tulale humu. Waamuzi 19:11

When they were by Jebus, the day was far spent; and the servant said to his master, Please come and let us turn aside into this city of the Jebusites, and lodge in it.

Bwana wake akamwambia, Hatutageuka sisi kuingia mji wa wageni, ambao si wa wana wa Israeli; lakini tutapita mpaka Gibea. Waamuzi 19:12

His master said to him, We won't turn aside into the city of a foreigner, that is not of the children of Israel; but we will pass over to Gibeah.

Kisha akamwambia mtumishi wake, Haya, tuifikilie miji hii mmojawapo nasi tutalala katika Gibea au katika Rama. Waamuzi 19:13

He said to his servant, Come and let us draw near to one of these places; and we will lodge in Gibeah, or in Ramah.

Basi wakashika njia kwenda zao mbele; jua likawachwea walipokuwa karibu na Gibea, ambao ni mji wa Benyamini. Waamuzi 19:14

So they passed on and went their way; and the sun went down on them near to Gibeah, which belongs to Benjamin.

Wakageuka huko, wapate kuingia na kulala katika Gibea; akaingia ndani, akaketi katika njia kuu ya mji; kwa kuwa hapakuwa na mtu awaye yote aliyewakaribisha nyumbani kwake kulala. Waamuzi 19:15

They turned aside there, to go in to lodge in Gibeah: and he went in, and sat him down in the street of the city; for there was no man who took them into his house to lodge.

Kisha, tazama, akatokea mtu mume mzee, atoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea hali ya ugeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini. Waamuzi 19:16

Behold, there came an old man from his work out of the field at even: now the man was of the hill-country of Ephraim, and he sojourned in Gibeah; but the men of the place were Benjamites.

Naye alipovua macho yake, akamwona huyo mtu msafiri katika njia kuu ya mji; huyo mzee akamwuliza, Waenda wapi wewe? Nawe watoka wapi? Waamuzi 19:17

He lifted up his eyes, and saw the wayfaring man in the street of the city; and the old man said, Where go you? and whence come you?

Akamwambia, Sisi twapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, twaenda huko upande wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya Bwana wala hapana mtu anikaribishaye nyumbani mwake. Waamuzi 19:18

He said to him, We are passing from Bethlehem Judah to the farther side of the hill-country of Ephraim; from there am I, and I went to Bethlehem Judah: and I am [now] going to the house of Yahweh; and there is no man who takes me into his house.

Walakini nyasi tunazo, na chakula cha hawa punda zetu; mkate pia tunao na divai kwa mimi na huyu kijakazi wako, na kwa huyu kijana aliye pamoja nasi watumishi wako; hapana uhitaji wa kitu cho chote. Waamuzi 19:19

Yet there is both straw and provender for our donkeys; and there is bread and wine also for me, and for your handmaid, and for the young man who is with your servants: there is no want of anything.

Kisha huyo mzee alisema, Na iwe amani kwako; lakini na haya yaliyokupungukia na yawe juu yangu mimi lakini usilale njiani. Waamuzi 19:20

The old man said, Peace be to you; howsoever let all your wants lie on me; only don't lodge in the street.

Basi akamtia ndani ya nyumba yake, akawapa punda chakula; nao wakaosha miguu, wakala na kunywa. Waamuzi 19:21

So he brought him into his house, and gave the donkeys fodder; and they washed their feet, and ate and drink.

Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua. Waamuzi 19:22

As they were making their hearts merry, behold, the men of the city, certain base fellows, beset the house round about, beating at the door; and they spoke to the master of the house, the old man, saying, Bring forth the man who came into your house, that we may know him.

Naye mtu mwenye nyumba akawatokea hapo nje, na kuwaambia, La, sivyo, ndugu zangu nawasihi msifanye uovu jinsi hii; kwa kuwa mtu huyu ameingia ndani ya nyumba yangu, msifanye upumbavu huu. Waamuzi 19:23

The man, the master of the house, went out to them, and said to them, No, my brothers, please don't act so wickedly; seeing that this man is come into my house, don't do this folly.

Tazama, binti yangu yupo hapa, ni mwanamwali, na suria wake huyo mtu; nitawaleta hapa nje sasa nanyi watwezeni, na kuwatenda hayo myaonayo kuwa ni mema; lakini mtu huyu msimtende jambo la upumbavu namna hii. Waamuzi 19:24

Behold, here is my daughter a virgin, and his concubine; them I will bring out now, and humble you them, and do with them what seems good to you: but to this man don't do any such folly.

Lakini hao watu hawakukubali kumsikia; basi mtu huyo akamshika suria wake, na kumleta nje kwao; nao wakamjua, na kumtenda uovu usiku kucha hata asubuhi kisha kulipoanza kupambauka wakamwacha aende zake. Waamuzi 19:25

But the men wouldn't listen to him: so the man laid hold on his concubine, and brought her forth to them; and they knew her, and abused her all the night until the morning: and when the day began to spring, they let her go.

Ndipo huyo mwanamke akaja alfajiri, akaanguka chini mlangoni pa nyumba ya mtu yule alimokuwamo bwana wake, hata kulipokucha. Waamuzi 19:26

Then came the woman in the dawning of the day, and fell down at the door of the man's house where her lord was, until it was light.

Bwana wake akaondoka asubuhi, akaifungua milango ya nyumba, akatoka nje ili aende zake, na tazama, huyo mwanamke suria yake alikuwa ameanguka pale mlangoni pa nyumba, na mikono yake ilikuwa i pale kizingitini. Waamuzi 19:27

Her lord rose up in the morning, and opened the doors of the house, and went out to go his way; and, behold, the woman his concubine was fallen down at the door of the house, with her hands on the threshold.

Akamwambia, Haya ondoka, twende zetu; lakini hakuna aliyemjibu; ndipo akamwinua akamweka juu ya punda; mtu huyo akaondoka, akaenda mahali pake mwenyewe. Waamuzi 19:28

He said to her, Up, and let us be going; but none answered: then he took her up on the donkey; and the man rose up, and got him to his place.

Naye alipokwisha kuingia nyumbani mwake, akatwaa kisu, kisha akamshika huyo suria yake, akampasua kiungo kwa kiungo, vipande kumi na viwili akampeleka katika mipaka yote ya Israeli. Waamuzi 19:29

When he was come into his house, he took a knife, and laid hold on his concubine, and divided her, limb by limb, into twelve pieces, and sent her throughout all the borders of Israel.

Basi ikawa, wote walioliona jambo hilo wakasema, Jambo kama hili halijatendeka wala kuonekana tangu siku hiyo wana wa Israeli walipokwea kutoka katika nchi ya Misri hata leo; haya, lifikirini, fanyeni shauri, mkanene. Waamuzi 19:30

It was so, that all who saw it said, There was no such deed done nor seen from the day that the children of Israel came up out of the land of Egypt to this day: consider it, take counsel, and speak.