Waamuzi 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 1 (Swahili) Judges 1 (English)

Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? Waamuzi 1:1

It happened after the death of Joshua, the children of Israel asked of Yahweh, saying, Who shall go up for us first against the Canaanites, to fight against them?

Bwana akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. Waamuzi 1:2

Yahweh said, Judah shall go up: behold, I have delivered the land into his hand.

Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika kura yangu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika kura yako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye. Waamuzi 1:3

Judah said to Simeon his brother, Come up with me into my lot, that we may fight against the Canaanites; and I likewise will go with you into your lot. So Simeon went with him.

Yuda akakwea; naye Bwana akawatia Wakanaani na Waperizi mkononi mwao; nao wakawapiga huko Bezeki watu elfu kumi. Waamuzi 1:4

Judah went up; and Yahweh delivered the Canaanites and the Perizzites into their hand: and they struck of them in Bezek ten thousand men.

Wakampata huyo Adoni-bezeki huko Bezeki; wakapigana naye, nao wakawapiga Wakanaani na Waperizi. Waamuzi 1:5

They found Adoni-bezek in Bezek; and they fought against him, and they struck the Canaanites and the Perizzites.

Lakini Adoni-bezeki akakimbia; nao wakamwandamia na kumshika, wakamkata vyanda vyake vya gumba vya mikono na vya miguu. Waamuzi 1:6

But Adoni-bezek fled; and they pursued after him, and caught him, and cut off his thumbs and his great toes.

Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vyanda vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko. Waamuzi 1:7

Adoni-bezek said, "Seventy kings, having their thumbs and their great toes cut off, gathered [their food] under my table: as I have done, so God has requited me." They brought him to Jerusalem, and he died there.

Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji. Waamuzi 1:8

The children of Judah fought against Jerusalem, and took it, and struck it with the edge of the sword, and set the city on fire.

Baadaye wana wa Yuda wakatelemka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi ya milimani, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela. Waamuzi 1:9

Afterward the children of Judah went down to fight against the Canaanites who lived in the hill-country, and in the South, and in the lowland.

Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai. Waamuzi 1:10

Judah went against the Canaanites who lived in Hebron (now the name of Hebron before was Kiriath Arba); and they struck Sheshai, and Ahiman, and Talmai.

Kisha kutoka hapo akawafuatia wale wenye kukaa Debiri. (Jina la Debiri hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-seferi.) Waamuzi 1:11

From there he went against the inhabitants of Debir. (Now the name of Debir before was Kiriath Sepher.)

Huyo Kalebu alisema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, nitamwoza mwanangu Aksa awe mkewe. Waamuzi 1:12

Caleb said, He who strikes Kiriath Sepher, and takes it, to him will I give Achsah my daughter as wife.

Naye Othnieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa huyo Kalebu, aliutwaa; basi akamwoza mwanawe Aksa. Waamuzi 1:13

Othniel the son of Kenaz, Caleb's younger brother, took it: and he gave him Achsah his daughter as wife.

Ikawa hapo alipokwenda kukaa naye, huyo mwanamke akamtaka ili aombe shamba kwa baba yake; na huyo mwanamke akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Una haja gani utakayo? Waamuzi 1:14

It happened, when she came [to him], that she moved him to ask of her father a field: and she alighted from off her donkey; and Caleb said to her, What would you?

Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini. Waamuzi 1:15

She said to him, Give me a blessing; for that you have set me in the land of the South, give me also springs of water. Caleb gave her the upper springs and the lower springs.

Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao. Waamuzi 1:16

The children of the Kenite, Moses' brother-in-law, went up out of the city of palm trees with the children of Judah into the wilderness of Judah, which is in the south of Arad; and they went and lived with the people.

Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma. Waamuzi 1:17

Judah went with Simeon his brother, and they struck the Canaanites who inhabited Zephath, and utterly destroyed it. The name of the city was called Hormah.

Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake. Waamuzi 1:18

Also Judah took Gaza with the border of it, and Ashkelon with the border of it, and Ekron with the border of it.

Bwana alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi ya milimani; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma. Waamuzi 1:19

Yahweh was with Judah; and drove out [the inhabitants of] the hill-country; for he could not drive out the inhabitants of the valley, because they had chariots of iron.

Kisha wakampa huyo Kalebu Hebroni, kama alivyonena Musa naye akawafukuza wale wana watatu wa Anaki. Waamuzi 1:20

They gave Hebron to Caleb, as Moses had spoken: and he drove out there the three sons of Anak.

Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo. Waamuzi 1:21

The children of Benjamin did not drive out the Jebusites who inhabited Jerusalem; but the Jebusites dwell with the children of Benjamin in Jerusalem to this day.

Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye Bwana alikuwa pamoja nao. Waamuzi 1:22

The house of Joseph, they also went up against Bethel; and Yahweh was with them.

Kisha mbari ya Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.) Waamuzi 1:23

The house of Joseph sent to spy out Bethel. (Now the name of the city before was Luz.)

Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuonyeshe maingilio ya mji huu, nasi tutakutendea mema. Waamuzi 1:24

The watchers saw a man come forth out of the city, and they said to him, Show us, we pray you, the entrance into the city, and we will deal kindly with you.

Basi akawaonyesha maingilio ya mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake. Waamuzi 1:25

He shown them the entrance into the city; and they struck the city with the edge of the sword; but they let the man go and all his family.

Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo. Waamuzi 1:26

The man went into the land of the Hittites, and built a city, and called the name of it Luz, which is the name of it to this day.

Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Bethsheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo. Waamuzi 1:27

Manasseh did not drive out [the inhabitants of] Beth-shean and its towns, nor [of] Taanach and its towns, nor the inhabitants of Dor and its towns, nor the inhabitants of Ibleam and its towns, nor the inhabitants of Megiddo and its towns; but the Canaanites would dwell in that land.

Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa. Waamuzi 1:28

It happened, when Israel had grown strong, that they put the Canaanites to forced labor, and did not utterly drive them out.

Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao. Waamuzi 1:29

Ephraim didn't drive out the Canaanites who lived in Gezer; but the Canaanites lived in Gezer among them.

Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa. Waamuzi 1:30

Zebulun didn't drive out the inhabitants of Kitron, nor the inhabitants of Nahalol; but the Canaanites lived among them, and became subject to forced labor.

Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu; Waamuzi 1:31

Asher didn't drive out the inhabitants of Acco, nor the inhabitants of Sidon, nor of Ahlab, nor of Achzib, nor of Helbah, nor of Aphik, nor of Rehob;

lakini Waasheri wakakaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; kwa kuwa hawakuwafukuza. Waamuzi 1:32

but the Asherites lived among the Canaanites, the inhabitants of the land; for they did not drive them out.

Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Bethshemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya hao wenyeji wa Bethshemeshi, na wenyeji wa Bethanathi, wakawatumikia kazi ya shokoa. Waamuzi 1:33

Naphtali didn't drive out the inhabitants of Beth-shemesh, nor the inhabitants of Beth Anath; but he lived among the Canaanites, the inhabitants of the land: nevertheless the inhabitants of Beth-shemesh and of Beth Anath became subject to forced labor.

Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kutelemkia bondeni; Waamuzi 1:34

The Amorites forced the children of Dan into the hill-country; for they would not allow them to come down to the valley;

lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. Waamuzi 1:35

but the Amorites would dwell in Mount Heres, in Aijalon, and in Shaalbim: yet the hand of the house of Joseph prevailed, so that they became subject to forced labor.

Mpaka wa Waamori ulikuwa tangu huko kupandia Akrabimu, tangu hilo jabali, na juu yake.

Waamuzi 1:36

The border of the Amorites was from the ascent of Akrabbim, from the rock, and upward.