Waamuzi 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 2 (Swahili) Judges 2 (English)

Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; Waamuzi 2:1

The angel of Yahweh came up from Gilgal to Bochim. He said, I made you to go up out of Egypt, and have brought you to the land which I swore to your fathers; and I said, I will never break my covenant with you:

nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? Waamuzi 2:2

and you shall make no covenant with the inhabitants of this land; you shall break down their altars. But you have not listened to my voice: why have you done this?

Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu. Waamuzi 2:3

Therefore I also said, I will not drive them out from before you; but they shall be [as thorns] in your sides, and their gods shall be a snare to you.

Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia. Waamuzi 2:4

It happened, when the angel of Yahweh spoke these words to all the children of Israel, that the people lifted up their voice, and wept.

Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia Bwana sadaka huko. Waamuzi 2:5

They called the name of that place Bochim: and they sacrificed there to Yahweh.

Basi hapo Yoshua alipowapa watu ruhusa waende zao, wana wa Israeli wakaenda kila mtu kuuendea urithi wake, ili kuimiliki hiyo nchi. Waamuzi 2:6

Now when Joshua had sent the people away, the children of Israel went every man to his inheritance to possess the land.

Watu hao wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya Bwana yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. Waamuzi 2:7

The people served Yahweh all the days of Joshua, and all the days of the elders who outlived Joshua, who had seen all the great work of Yahweh that he had worked for Israel.

Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi. Waamuzi 2:8

Joshua the son of Nun, the servant of Yahweh, died, being one hundred ten years old.

Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi. Waamuzi 2:9

They buried him in the border of his inheritance in Timnath Heres, in the hill country of Ephraim, on the north of the mountain of Gaash.

Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. Waamuzi 2:10

Also all that generation were gathered to their fathers: and there arose another generation after them, who didn't know Yahweh, nor yet the work which he had worked for Israel.

Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. Waamuzi 2:11

The children of Israel did that which was evil in the sight of Yahweh, and served the Baals;

Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Waamuzi 2:12

and they forsook Yahweh, the God of their fathers, who brought them out of the land of Egypt, and followed other gods, of the gods of the peoples who were round about them, and bowed themselves down to them: and they provoked Yahweh to anger.

Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. Waamuzi 2:13

They forsook Yahweh, and served Baal and the Ashtaroth.

Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. Waamuzi 2:14

The anger of Yahweh was kindled against Israel, and he delivered them into the hands of spoilers who despoiled them; and he sold them into the hands of their enemies round about, so that they could not any longer stand before their enemies.

Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. Waamuzi 2:15

Wherever they went out, the hand of Yahweh was against them for evil, as Yahweh had spoken, and as Yahweh had sworn to them: and they were sore distressed.

Kisha Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara. Waamuzi 2:16

Yahweh raised up judges, who saved them out of the hand of those who despoiled them.

Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo. Waamuzi 2:17

Yet they didn't listen to their judges; for they played the prostitute after other gods, and bowed themselves down to them: they turned aside quickly out of the way in which their fathers walked, obeying the commandments of Yahweh; [but] they didn't do so.

Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. Waamuzi 2:18

When Yahweh raised them up judges, then Yahweh was with the judge, and saved them out of the hand of their enemies all the days of the judge: for it repented Yahweh because of their groaning by reason of those who oppressed them and vexed them.

Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi. Waamuzi 2:19

But it happened, when the judge was dead, that they turned back, and dealt more corruptly than their fathers, in following other gods to serve them, and to bow down to them; they didn't cease from their doings, nor from their stubborn way.

Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu; Waamuzi 2:20

The anger of Yahweh was kindled against Israel; and he said, Because this nation have transgressed my covenant which I commanded their fathers, and have not listened to my voice;

mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa; Waamuzi 2:21

I also will not henceforth drive out any from before them of the nations that Joshua left when he died;

ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia hiyo, au sivyo. Waamuzi 2:22

that by them I may prove Israel, whether they will keep the way of Yahweh to walk therein, as their fathers did keep it, or not.

Basi Bwana akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.

Waamuzi 2:23

So Yahweh left those nations, without driving them out hastily; neither delivered he them into the hand of Joshua.