Waamuzi 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 4 (Swahili) Judges 4 (English)

Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya Bwana. Waamuzi 4:1

The children of Israel again did that which was evil in the sight of Yahweh, when Ehud was dead.

Bwana akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa amiri wa jeshi lake. Waamuzi 4:2

Yahweh sold them into the hand of Jabin king of Canaan, who reigned in Hazor; the captain of whose host was Sisera, who lived in Harosheth of the Gentiles.

Wana wa Israeli wakamlilia Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini. Waamuzi 4:3

The children of Israel cried to Yahweh: for he had nine hundred chariots of iron; and twenty years he mightily oppressed the children of Israel.

Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. Waamuzi 4:4

Now Deborah, a prophetess, the wife of Lappidoth, she judged Israel at that time.

Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue. Waamuzi 4:5

She lived under the palm tree of Deborah between Ramah and Bethel in the hill-country of Ephraim: and the children of Israel came up to her for judgment.

Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni? Waamuzi 4:6

She sent and called Barak the son of Abinoam out of Kedesh-naphtali, and said to him, Hasn't Yahweh, the God of Israel, commanded, [saying], Go and draw to Mount Tabor, and take with you ten thousand men of the children of Naphtali and of the children of Zebulun?

Nami nitakuvutia Sisera, amiri wa jeshi lake Yabini, hata mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako. Waamuzi 4:7

I will draw to you, to the river Kishon, Sisera, the captain of Jabin's army, with his chariots and his multitude; and I will deliver him into your hand.

Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Waamuzi 4:8

Barak said to her, If you will go with me, then I will go; but if you will not go with me, I will not go.

Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana Bwana atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. Waamuzi 4:9

She said, I will surely go with you: notwithstanding, the journey that you take shall not be for your honor; for Yahweh will sell Sisera into the hand of a woman. Deborah arose, and went with Barak to Kedesh.

Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye. Waamuzi 4:10

Barak called Zebulun and Naphtali together to Kedesh; and there went up ten thousand men at his feet: and Deborah went up with him.

Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni, yaani na wana wa Hobabu, shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mwaloni ulioko Saanaimu, karibu na Kedeshi. Waamuzi 4:11

Now Heber the Kenite had separated himself from the Kenites, even from the children of Hobab the brother-in-law of Moses, and had pitched his tent as far as the oak in Zaanannim, which is by Kedesh.

Watu wakamwambia Sisera ya kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu amekwea kwenda mlima wa Tabori. Waamuzi 4:12

They told Sisera that Barak the son of Abinoam was gone up to Mount Tabor.

Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia kenda, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni. Waamuzi 4:13

Sisera gathered together all his chariots, even nine hundred chariots of iron, and all the people who were with him, from Harosheth of the Gentiles, to the river Kishon.

Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo Bwana amemtia Sisera katika mkono wako. Je! Bwana hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata. Waamuzi 4:14

Deborah said to Barak, Up; for this is the day in which Yahweh has delivered Sisera into your hand; hasn't Yahweh gone out before you? So Barak went down from Mount Tabor, and ten thousand men after him.

Bwana akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu. Waamuzi 4:15

Yahweh confused Sisera, and all his chariots, and all his host, with the edge of the sword before Barak; and Sisera alighted from his chariot, and fled away on his feet.

Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hata Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja. Waamuzi 4:16

But Barak pursued after the chariots, and after the host, to Harosheth of the Gentiles: and all the host of Sisera fell by the edge of the sword; there was not a man left.

Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni. Waamuzi 4:17

However Sisera fled away on his feet to the tent of Jael the wife of Heber the Kenite; for there was peace between Jabin the king of Hazor and the house of Heber the Kenite.

Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti. Waamuzi 4:18

Jael went out to meet Sisera, and said to him, Turn in, my lord, turn in to me; don't be afraid. He came in to her into the tent, and she covered him with a rug.

Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika. Waamuzi 4:19

He said to her, Please give me a little water to drink; for I am thirsty. She opened a bottle of milk, and gave him drink, and covered him.

Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana. Waamuzi 4:20

He said to her, Stand in the door of the tent, and it shall be, when any man does come and inquire of you, and say, Is there any man here? that you shall say, No.

Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa. Waamuzi 4:21

Then Jael Heber's wife took a tent-pin, and took a hammer in her hand, and went softly to him, and struck the pin into his temples, and it pierced through into the ground; for he was in a deep sleep; so he swooned and died.

Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonyesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake. Waamuzi 4:22

Behold, as Barak pursued Sisera, Jael came out to meet him, and said to him, Come, and I will show you the man whom you seek. He came to her; and, behold, Sisera lay dead, and the tent-pin was in his temples.

Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo. Waamuzi 4:23

So God subdued on that day Jabin the king of Canaan before the children of Israel.

Mkono wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani. Waamuzi 4:24

The hand of the children of Israel prevailed more and more against Jabin the king of Canaan, until they had destroyed Jabin king of Canaan.