Ayabu 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 9 (Swahili) Job 9 (English)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Ayabu 9:1

Then Job answered,

Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu? Ayabu 9:2

"Truly I know that it is so, But how can man be just with God?

Kama akipenda kushindana naye, Hawezi kumjibu neno moja katika elfu. Ayabu 9:3

If he is pleased to contend with him, He can't answer him one time in a thousand.

Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa? Ayabu 9:4

God who is wise in heart, and mighty in strength: Who has hardened himself against him, and prospered?

Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake. Ayabu 9:5

Who removes the mountains, and they don't know it, When he overturns them in his anger

Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetema. Ayabu 9:6

Who shakes the earth out of its place; The pillars of it tremble;

Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri. Ayabu 9:7

Who commands the sun, and it doesn't rise, And seals up the stars;

Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Ayabu 9:8

Who alone stretches out the heavens, Treads on the waves of the sea;

Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini. Ayabu 9:9

Who makes the Bear, Orion, and the Pleiades, And the chambers of the south;

Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana; Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika. Ayabu 9:10

Who does great things past finding out, Yes, marvelous things without number.

Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone; Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue. Ayabu 9:11

Behold, he goes by me, and I don't see him. He passes on also, but I don't perceive him.

Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini? Ayabu 9:12

Behold, he snatches away; who can hinder him? Who will ask him, 'What are you doing?'

Mungu haondoi hasira zake; Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake. Ayabu 9:13

"God will not withdraw his anger; The helpers of Rahab stoop under him.

Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye? Ayabu 9:14

How much less shall I answer him, Choose my words to argue with him?

Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu; Ningemsihi-sihi mtesi wangu. Ayabu 9:15

Whom, though I were righteous, yet would I not answer. I would make supplication to my judge.

Kama ningemwita, naye akaniitikia; Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu. Ayabu 9:16

If I had called, and he had answered me, Yet would I not believe that he listened to my voice.

Yeye anipondaye kwa dhoruba, Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu. Ayabu 9:17

For he breaks me with a tempest, Multiplies my wounds without cause.

Haniachi nipate kuvuta pumzi, Lakini hunijaza uchungu. Ayabu 9:18

He will not allow me to take my breath, But fills me with bitterness.

Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo! Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayeniwekea muhula? Ayabu 9:19

If it is a matter of strength, behold, he is mighty! If of justice, 'Who,' says he, 'will summon me?'

Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu. Ayabu 9:20

Though I am righteous, my own mouth shall condemn me. Though I am blameless, it shall prove me perverse.

Mimi ni mkamilifu; siangalii nafsi yangu; Naudharau uhai wangu. Ayabu 9:21

I am blameless. I don't regard myself. I despise my life.

Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema, Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia. Ayabu 9:22

"It is all the same. Therefore I say, He destroys the blameless and the wicked.

Kama hilo pigo likiua ghafula, Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa. Ayabu 9:23

If the scourge kills suddenly, He will mock at the trial of the innocent.

Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi? Ayabu 9:24

The earth is given into the hand of the wicked. He covers the faces of the judges of it. If not he, then who is it?

Basi siku zangu zina mbio kuliko tarishi; Zakimbia, wala hazioni mema. Ayabu 9:25

"Now my days are swifter than a runner. They flee away, they see no good,

Zimepita kama merikebu ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiaye mawindo. Ayabu 9:26

They have passed away as the swift ships, As the eagle that swoops on the prey.

Nikisema, Mimi nitasahau kuugua kwangu, Nitaacha kununa uso nikachangamke moyo; Ayabu 9:27

If I say, 'I will forget my complaint, I will put off my sad face, and cheer up;'

Mimi huziogopa huzuni zangu zote, Najua kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia. Ayabu 9:28

I am afraid of all my sorrows, I know that you will not hold me innocent.

Nitahukumiwa kuwa ni mkosa; Ya nini basi nitaabike bure? Ayabu 9:29

I shall be condemned; Why then do I labor in vain?

Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji, Na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni; Ayabu 9:30

If I wash myself with snow, And cleanse my hands with lye,

Lakini utanitupa shimoni, Nami hata nguo zangu zitanichukia. Ayabu 9:31

Yet you will plunge me in the ditch. My own clothes shall abhor me.

Kwani yeye si mtu, kama mimi, hata nimjibu, Hata tukaribiane katika hukumu. Ayabu 9:32

For he is not a man, as I am, that I should answer him, That we should come together in judgment.

Hapana mwenye kuamua katikati yetu, Awezaye kutuwekea mkono sote wawili. Ayabu 9:33

There is no umpire between us, That might lay his hand on us both.

Na aniondolee fimbo yake, Na utisho wake usinitie hofu; Ayabu 9:34

Let him take his rod away from me, Let his terror not make me afraid:

Ndipo hapo ningesema, nisimwogope; Kwani sivyo nilivyo nafsini mwangu. Ayabu 9:35

Then I would speak, and not fear him, For I am not so in myself.