Ayabu 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 33 (Swahili) Job 33 (English)

Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Ayabu 33:1

"However, Job, Please hear my speech, And listen to all my words.

Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Ayabu 33:2

See now, I have opened my mouth. My tongue has spoken in my mouth.

Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu. Ayabu 33:3

My words shall utter the uprightness of my heart; That which my lips know they shall speak sincerely.

Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Ayabu 33:4

The Spirit of God has made me, And the breath of the Almighty gives me life.

Kwamba waweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame. Ayabu 33:5

If you can, answer me; Set your words in order before me, and stand forth.

Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo. Ayabu 33:6

Behold, I am toward God even as you are: I am also formed out of the clay.

Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito. Ayabu 33:7

Behold, my terror shall not make you afraid, Neither shall my pressure be heavy on you.

Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema, Ayabu 33:8

"Surely you have spoken in my hearing, I have heard the voice of your words, saying,

Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu; Ayabu 33:9

'I am clean, without disobedience. I am innocent, neither is there iniquity in me:

Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake; Ayabu 33:10

Behold, he finds occasions against me, He counts me for his enemy:

Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza. Ayabu 33:11

He puts my feet in the stocks, He marks all my paths.'

Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Ayabu 33:12

"Behold, I will answer you. In this you are not just; For God is greater than man.

Nawe kwani kumnung'unikia, Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote? Ayabu 33:13

Why do you strive against him, Because he doesn't give account of any of his matters?

Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Ayabu 33:14

For God speaks once, Yes twice, though man pays no attention.

Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ayabu 33:15

In a dream, in a vision of the night, When deep sleep falls on men, In slumbering on the bed;

Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ayabu 33:16

Then he opens the ears of men, And seals their instruction,

Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Ayabu 33:17

That he may withdraw man from his purpose, And hide pride from man.

Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Ayabu 33:18

He keeps back his soul from the pit, And his life from perishing by the sword.

Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Ayabu 33:19

He is chastened also with pain on his bed, With continual strife in his bones;

Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Ayabu 33:20

So that his life abhors bread, And his soul dainty food.

Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje. Ayabu 33:21

His flesh is so consumed away, that it can't be seen; His bones that were not seen stick out.

Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi. Ayabu 33:22

Yes, his soul draws near to the pit, And his life to the destroyers.

Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo; Ayabu 33:23

"If there is beside him an angel, An interpreter, one among a thousand, To show to man what is right for him;

Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi. Ayabu 33:24

Then God is gracious to him, and says, 'Deliver him from going down to the pit, I have found a ransom.'

Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake; Ayabu 33:25

His flesh shall be fresher than a child's; He returns to the days of his youth.

Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake. Ayabu 33:26

He prays to God, and he is favorable to him, So that he sees his face with joy: He restores to man his righteousness.

Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo; Ayabu 33:27

He sings before men, and says, 'I have sinned, and perverted that which was right, And it didn't profit me.

Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga. Ayabu 33:28

He has redeemed my soul from going into the pit, My life shall see the light.'

Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu, Ayabu 33:29

"Behold, God works all these things, Twice, yes three times, with a man,

Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai. Ayabu 33:30

To bring back his soul from the pit, That he may be enlightened with the light of the living.

Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize; Nyamaza, mimi nitasema. Ayabu 33:31

Mark well, Job, and listen to me: Hold your peace, and I will speak.

Kama una neno la kusema, nijibu; Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki. Ayabu 33:32

If you have anything to say, answer me: Speak, for I desire to justify you.

Kama sivyo, unisikilize mimi; Nyamaza, nami nitakufunza hekima. Ayabu 33:33

If not, listen to me: Hold your peace, and I will teach you wisdom."