Ayabu 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 2 (Swahili) Job 2 (English)

Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za Bwana. Ayabu 2:1

Again it happened on the day when the sons of God came to present themselves before Yahweh, that Satan came also among them to present himself before Yahweh.

Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Ayabu 2:2

Yahweh said to Satan, "Where have you come from?" Satan answered Yahweh, and said, "From going back and forth in the earth, and from walking up and down in it."

Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Ayabu 2:3

Yahweh said to Satan, "Have you considered my servant Job? For there is none like him in the earth, a blameless and an upright man, one who fears God, and turns away from evil. He still maintains his integrity, although you incited me against him, to ruin him without cause."

Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Ayabu 2:4

Satan answered Yahweh, and said, "Skin for skin. Yes, all that a man has will he give for his life.

Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako. Ayabu 2:5

But put forth your hand now, and touch his bone and his flesh, and he will renounce you to your face."

Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Ayabu 2:6

Yahweh said to Satan, "Behold, he is in your hand. Only spare his life."

Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa. Ayabu 2:7

So Satan went forth from the presence of Yahweh, and struck Job with painful sores from the sole of his foot to his head.

Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. Ayabu 2:8

He took for himself a potsherd to scrape himself with, and he sat among the ashes.

Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. Ayabu 2:9

Then his wife said to him, "Do you still maintain your integrity? Renounce God, and die."

Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Ayabu 2:10

But he said to her, "You speak as one of the foolish women would speak. What? Shall we receive good at the hand of God, and shall we not receive evil?" In all this Job didn't sin with his lips.

Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo. Ayabu 2:11

Now when Job's three friends heard of all this evil that had come on him, they each came from his own place: Eliphaz the Temanite, Bildad the Shuhite, and Zophar the Naamathite, and they made an appointment together to come to sympathize with him and to comfort him.

Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni. Ayabu 2:12

When they lifted up their eyes from a distance, and didn't recognize him, they raised their voices, and wept; and they each tore his robe, and sprinkled dust on their heads toward the sky.

Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno. Ayabu 2:13

So they sat down with him on the ground seven days and seven nights, and none spoke a word to him, for they saw that his grief was very great.