Ayabu 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 20 (Swahili) Job 20 (English)

Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema, Ayabu 20:1

Then Zophar the Naamathite answered,

Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu. Ayabu 20:2

"Therefore do my thoughts give answer to me, Even by reason of my haste that is in me.

Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu. Ayabu 20:3

I have heard the reproof which puts me to shame; The spirit of my understanding answers me.

Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi, Ayabu 20:4

Don't you know this from old time, Since man was placed on earth,

Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu? Ayabu 20:5

That the triumphing of the wicked is short, The joy of the godless but for a moment?

Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni; Ayabu 20:6

Though his height mount up to the heavens, And his head reach to the clouds,

Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi? Ayabu 20:7

Yet he shall perish forever like his own dung, Those who have seen him shall say, 'Where is he?'

Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku, Ayabu 20:8

He shall fly away as a dream, and shall not be found: Yes, he shall be chased away like a vision of the night.

Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena. Ayabu 20:9

The eye which saw him shall see him no more, Neither shall his place any more see him.

Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake. Ayabu 20:10

His children shall seek the favor of the poor. His hands shall give back his wealth.

Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini. Ayabu 20:11

His bones are full of his youth, But youth shall lie down with him in the dust.

Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake; Ayabu 20:12

"Though wickedness is sweet in his mouth, Though he hide it under his tongue,

Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake; Ayabu 20:13

Though he spare it, and will not let it go, But keep it still within his mouth;

Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake. Ayabu 20:14

Yet his food in his bowels is turned. It is cobra venom within him.

Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake. Ayabu 20:15

He has swallowed down riches, and he shall vomit them up again. God will cast them out of his belly.

Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua. Ayabu 20:16

He shall suck cobra venom. The viper's tongue shall kill him.

Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi. Ayabu 20:17

He shall not look at the rivers, The flowing streams of honey and butter.

Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi. Ayabu 20:18

That for which he labored he shall restore, and shall not swallow it down; According to the substance that he has gotten, he shall not rejoice.

Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang'anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga. Ayabu 20:19

For he has oppressed and forsaken the poor. He has violently taken away a house, and he shall not build it up.

Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia. Ayabu 20:20

"Because he knew no quietness within him, He shall not save anything of that in which he delights.

Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu. Ayabu 20:21

There was nothing left that he didn't devour, Therefore his prosperity shall not endure.

Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia. Ayabu 20:22

In the fullness of his sufficiency, distress shall overtake him: The hand of everyone who is in misery shall come on him.

Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula. Ayabu 20:23

When he is about to fill his belly, God will cast the fierceness of his wrath on him. It will rain on him while he is eating.

Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili. Ayabu 20:24

He shall flee from the iron weapon. The bronze arrow shall strike him through.

Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing'aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake. Ayabu 20:25

He draws it forth, and it comes out of his body. Yes, the glittering point comes out of his liver. Terrors are on him.

Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake. Ayabu 20:26

All darkness is laid up for his treasures. An unfanned fire shall devour him. It shall consume that which is left in his tent.

Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake. Ayabu 20:27

The heavens shall reveal his iniquity, The earth shall rise up against him.

Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake. Ayabu 20:28

The increase of his house shall depart; They shall rush away in the day of his wrath.

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu. Ayabu 20:29

This is the portion of a wicked man from God, The heritage appointed to him by God."