Ayabu 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 18 (Swahili) Job 18 (English)

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, Ayabu 18:1

Then Bildad the Shuhite answered,

Je! Hata lini utayategea maneno mitambo? Fikiri, kisha baadaye tutanena. Ayabu 18:2

"How long will you hunt for words? Consider, and afterwards we will speak.

Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani, Tena kuwa wanajisi machoni pako? Ayabu 18:3

Why are we counted as animals, Which have become unclean in your sight?

Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake? Ayabu 18:4

You who tear yourself in your anger, Shall the earth be forsaken for you? Or shall the rock be removed out of its place?

Naam, mwanga wa waovu utazimika, Wala mwali wa moto wake hautang'aa. Ayabu 18:5

"Yes, the light of the wicked shall be put out, The spark of his fire shall not shine.

Mwanga hemani mwake utakuwa giza, Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa. Ayabu 18:6

The light shall be dark in his tent, His lamp above him shall be put out.

Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini. Ayabu 18:7

The steps of his strength shall be shortened, His own counsel shall cast him down.

Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi. Ayabu 18:8

For he is cast into a net by his own feet, And he wanders into its mesh.

Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtambo utamgwia. Ayabu 18:9

A snare shall take him by the heel; A trap shall lay hold on him.

Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani. Ayabu 18:10

A noose is hidden for him in the ground, A trap for him in the way.

Matisho yatamtia hofu pande zote, Na kumfukuza karibu na visigino vyake. Ayabu 18:11

Terrors shall make him afraid on every side, And shall chase him at his heels.

Nguvu zake zitaliwa na njaa, Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake. Ayabu 18:12

His strength shall be famished, Calamity shall be ready at his side.

Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake. Ayabu 18:13

The members of his body shall be devoured, The firstborn of death shall devour his members.

Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho. Ayabu 18:14

He shall be rooted out of his tent where he trusts. He shall be brought to the king of terrors.

Ambacho si chake kitakaa katika hema yake; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake. Ayabu 18:15

There shall dwell in his tent that which is none of his. Sulfur shall be scattered on his habitation.

Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa. Ayabu 18:16

His roots shall be dried up beneath, Above shall his branch be cut off.

Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani. Ayabu 18:17

His memory shall perish from the earth. He shall have no name in the street.

Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani. Ayabu 18:18

He shall be driven from light into darkness, And chased out of the world.

Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake, Wala hatasalia mtu hapo alipokaa. Ayabu 18:19

He shall have neither son nor grandson among his people, Nor any remaining where he sojourned.

Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu. Ayabu 18:20

Those who come after shall be astonished at his day, As those who went before were frightened.

Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu, Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.

Ayabu 18:21

Surely such are the dwellings of the unrighteous, This is the place of him who doesn't know God."