Matendo ya Mitume 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 5 (Swahili) Acts 5 (English)

Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, Matendo ya Mitume 5:1

But a certain man named Ananias, with Sapphira, his wife, sold a possession,

akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Matendo ya Mitume 5:2

and kept back part of the price, his wife also being aware of it, and brought a certain part, and laid it at the apostles' feet.

Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Matendo ya Mitume 5:3

But Peter said, "Ananias, why has Satan filled your heart to lie to the Holy Spirit, and to keep back part of the price of the land?

Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Matendo ya Mitume 5:4

While you kept it, didn't it remain your own? After it was sold, wasn't it in your power? How is it that you have conceived this thing in your heart? You haven't lied to men, but to God."

Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Matendo ya Mitume 5:5

Ananias, hearing these words, fell down and died. Great fear came on all who heard these things.

Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Matendo ya Mitume 5:6

The young men arose and wrapped him up, and they carried him out and buried him.

Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Matendo ya Mitume 5:7

About three hours later, his wife, not knowing what had happened, came in.

Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Matendo ya Mitume 5:8

Peter answered her, "Tell me whether you sold the land for so much." She said, "Yes, for so much."

Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. Matendo ya Mitume 5:9

But Peter asked her, "How is it that you have agreed together to tempt the Spirit of the Lord? Behold, the feet of those who have buried your husband are at the door, and they will carry you out."

Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. Matendo ya Mitume 5:10

She fell down immediately at his feet, and died. The young men came in and found her dead, and they carried her out and buried her by her husband.

Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya. Matendo ya Mitume 5:11

Great fear came on the whole assembly, and on all who heard these things.

Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; Matendo ya Mitume 5:12

By the hands of the apostles many signs and wonders were done among the people. They were all with one accord in Solomon's porch.

na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha; Matendo ya Mitume 5:13

None of the rest dared to join them, however the people honored them.

walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; Matendo ya Mitume 5:14

More believers were added to the Lord, multitudes of both men and women.

hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao. Matendo ya Mitume 5:15

They even carried out the sick into the streets, and laid them on cots and mattresses, so that as Peter came by, at the least his shadow might overshadow some of them.

Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa. Matendo ya Mitume 5:16

Multitudes also came together from the cities around Jerusalem, bringing sick people, and those who were tormented by unclean spirits: and they were all healed.

Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu, Matendo ya Mitume 5:17

But the high priest rose up, and all those who were with him (which is the sect of the Sadducees), and they were filled with jealousy,

wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; Matendo ya Mitume 5:18

and laid hands on the apostles, and put them in public custody.

lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Matendo ya Mitume 5:19

But an angel of the Lord opened the prison doors by night, and brought them out, and said,

Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu. Matendo ya Mitume 5:20

"Go stand and speak in the temple to the people all the words of this life."

Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete. Matendo ya Mitume 5:21

When they heard this, they entered into the temple about daybreak, and taught. But the high priest came, and those who were with him, and called the council together, and all the senate of the children of Israel, and sent to the prison to have them brought.

Hata watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, Matendo ya Mitume 5:22

But the officers who came didn't find them in the prison. They returned and reported,

wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu ndani. Matendo ya Mitume 5:23

"We found the prison shut and locked, and the guards standing before the doors, but when we opened them, we found no one inside!"

Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo. Matendo ya Mitume 5:24

Now when the high priest, the captain of the temple, and the chief priests heard these words, they were very perplexed about them and what might become of this.

Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. Matendo ya Mitume 5:25

One came and told them, "Behold, the men whom you put in prison are in the temple, standing and teaching the people."

Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe. Matendo ya Mitume 5:26

Then the captain went with the officers, and brought them without violence, for they were afraid that the people might stone them.

Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, Matendo ya Mitume 5:27

When they had brought them, they set them before the council. The high priest questioned them,

akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Matendo ya Mitume 5:28

saying, "Didn't we strictly charge you not to teach in this name? Behold, you have filled Jerusalem with your teaching, and intend to bring this man's blood on us."

Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Matendo ya Mitume 5:29

But Peter and the apostles answered, "We must obey God rather than men.

Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Matendo ya Mitume 5:30

The God of our fathers raised up Jesus, whom you killed, hanging him on a tree.

Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Matendo ya Mitume 5:31

God exalted him with his right hand to be a Prince and a Savior, to give repentance to Israel, and remission of sins.

Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio. Matendo ya Mitume 5:32

We are His witnesses of these things; and so also is the Holy Spirit, whom God has given to those who obey him."

Wao waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua. Matendo ya Mitume 5:33

But they, when they heard this, were cut to the heart, and determined to kill them.

Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo, Matendo ya Mitume 5:34

But one stood up in the council, a Pharisee named Gamaliel, a teacher of the law, honored by all the people, and commanded to put the apostles out for a little while.

akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa. Matendo ya Mitume 5:35

He said to them, "You men of Israel, be careful concerning these men, what you are about to do.

Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. Matendo ya Mitume 5:36

For before these days Theudas rose up, making himself out to be somebody; to whom a number of men, about four hundred, joined themselves: who was slain; and all, as many as obeyed him, were dispersed, and came to nothing.

Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika. Matendo ya Mitume 5:37

After this man, Judas of Galilee rose up in the days of the enrollment, and drew away some people after him. He also perished, and all, as many as obeyed him, were scattered abroad.

Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, Matendo ya Mitume 5:38

Now I tell you, withdraw from these men, and leave them alone. For if this counsel or this work is of men, it will be overthrown.

lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu. Matendo ya Mitume 5:39

But if it is of God, you will not be able to overthrow it, and you would be found even to be fighting against God!"

Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao. Matendo ya Mitume 5:40

They agreed with him. Summoning the apostles, they beat them and charged them not to speak in the name of Jesus, and let them go.

Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. Matendo ya Mitume 5:41

They therefore departed from the presence of the council, rejoicing that they were counted worthy to suffer dishonor for Jesus' name.

Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo. Matendo ya Mitume 5:42

Every day, in the temple and at home, they never stopped teaching and preaching Jesus, the Christ.