Matendo ya Mitume 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 17 (Swahili) Acts 17 (English)

Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. Matendo ya Mitume 17:1

Now when they had passed through Amphipolis and Apollonia, they came to Thessalonica, where there was a synagogue of the Jews.

Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, Matendo ya Mitume 17:2

Paul, as was his custom, went in to them, and for three Sabbath days reasoned with them from the Scriptures,

akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Matendo ya Mitume 17:3

explaining and demonstrating that the Christ had to suffer and rise again from the dead, and saying, "This Jesus, whom I proclaim to you, is the Christ."

Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Matendo ya Mitume 17:4

Some of them were persuaded, and joined Paul and Silas, of the devout Greeks a great multitude, and not a few of the chief women.

Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; Matendo ya Mitume 17:5

But the unpersuaded Jews took along{TR reads "And the Jews who were unpersuaded, becoming envious and taking along" instead of "But the unpersuaded Jews took along"} some wicked men from the marketplace, and gathering a crowd, set the city in an uproar. Assaulting the house of Jason, they sought to bring them out to the people.

na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, Matendo ya Mitume 17:6

When they didn't find them, they dragged Jason and certain brothers{The word for "brothers" here and where the context allows may be also correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} before the rulers of the city, crying, "These who have turned the world upside down have come here also,

na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Matendo ya Mitume 17:7

whom Jason has received. These all act contrary to the decrees of Caesar, saying that there is another king, Jesus!"

Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Matendo ya Mitume 17:8

The multitude and the rulers of the city were troubled when they heard these things.

Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. Matendo ya Mitume 17:9

When they had taken security from Jason and the rest, they let them go.

Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Matendo ya Mitume 17:10

The brothers immediately sent Paul and Silas away by night to Beroea. When they arrived, they went into the Jewish synagogue.

Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Matendo ya Mitume 17:11

Now these were more noble than those in Thessalonica, in that they received the word with all readiness of the mind, examining the Scriptures daily to see whether these things were so.

Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. Matendo ya Mitume 17:12

Many of them therefore believed; also of the prominent Greek women, and not a few men.

Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano. Matendo ya Mitume 17:13

But when the Jews of Thessalonica had knowledge that the word of God was proclaimed by Paul at Beroea also, they came there likewise, agitating the multitudes.

Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko. Matendo ya Mitume 17:14

Then the brothers immediately sent out Paul to go as far as to the sea, and Silas and Timothy still stayed there.

Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie kumfuata, wakaenda zao. Matendo ya Mitume 17:15

But those who escorted Paul brought him as far as Athens. Receiving a commandment to Silas and Timothy that they should come to him very quickly, they departed.

Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake. Matendo ya Mitume 17:16

Now while Paul waited for them at Athens, his spirit was provoked within him as he saw the city full of idols.

Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku. Matendo ya Mitume 17:17

So he reasoned in the synagogue with the Jews and the devout persons, and in the marketplace every day with those who met him.

Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo. Matendo ya Mitume 17:18

Some of the Epicurean and Stoic philosophers also{TR omits "also"} were conversing with him. Some said, "What does this babbler want to say?" Others said, "He seems to be advocating foreign deities," because he preached Jesus and the resurrection.

Wakamshika, wakamchukua Areopago, wakisema, Je! Twaweza kujua maana ya elimu hii mpya unayoinena? Matendo ya Mitume 17:19

They took hold of him, and brought him to the Areopagus, saying, "May we know what this new teaching is, which is spoken by you?

Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, basi, maana ya mambo haya. Matendo ya Mitume 17:20

For you bring certain strange things to our ears. We want to know therefore what these things mean."

Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya. Matendo ya Mitume 17:21

Now all the Athenians and the strangers living there spent their time in nothing else, but either to tell or to hear some new thing.

Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Matendo ya Mitume 17:22

Paul stood in the middle of the Areopagus, and said, "You men of Athens, I perceive that you are very religious in all things.

Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Matendo ya Mitume 17:23

For as I passed along, and observed the objects of your worship, I found also an altar with this inscription: 'TO AN UNKNOWN GOD.' What therefore you worship in ignorance, this I announce to you.

Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; Matendo ya Mitume 17:24

The God who made the world and all things in it, he, being Lord of heaven and earth, doesn't dwell in temples made with hands,

wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. Matendo ya Mitume 17:25

neither is he served by men's hands, as though he needed anything, seeing he himself gives to all life and breath, and all things.

Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; Matendo ya Mitume 17:26

He made from one blood every nation of men to dwell on all the surface of the earth, having determined appointed seasons, and the boundaries of their dwellings,

ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Matendo ya Mitume 17:27

that they should seek the Lord, if perhaps they might reach out for him and find him, though he is not far from each one of us.

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Matendo ya Mitume 17:28

'For in him we live, and move, and have our being.' As some of your own poets have said, 'For we are also his offspring.'

Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu. Matendo ya Mitume 17:29

Being then the offspring of God, we ought not to think that the Divine Nature is like gold, or silver, or stone, engraved by art and design of man.

Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Matendo ya Mitume 17:30

The times of ignorance therefore God overlooked. But now he commands that all people everywhere should repent,

Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu. Matendo ya Mitume 17:31

because he has appointed a day in which he will judge the world in righteousness by the man whom he has ordained; of which he has given assurance to all men, in that he has raised him from the dead."

Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo. Matendo ya Mitume 17:32

Now when they heard of the resurrection of the dead, some mocked; but others said, "We want to hear you again concerning this."

Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha. Matendo ya Mitume 17:33

Thus Paul went out from among them.

Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao. Matendo ya Mitume 17:34

But certain men joined with him, and believed, among whom also was Dionysius the Areopagite, and a woman named Damaris, and others with them.