Matendo ya Mitume 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 4 (Swahili) Acts 4 (English)

Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, Matendo ya Mitume 4:1

As they spoke to the people, the priests and the captain of the temple and the Sadducees came to them,

wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu. Matendo ya Mitume 4:2

being upset because they taught the people and proclaimed in Jesus the resurrection from the dead.

Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. Matendo ya Mitume 4:3

They laid hands on them, and put them in custody until the next day, for it was now evening.

Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano. Matendo ya Mitume 4:4

But many of those who heard the word believed, and the number of the men came to be about five thousand.

Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, Matendo ya Mitume 4:5

It happened in the morning, that their rulers, elders, and scribes were gathered together in Jerusalem.

na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu. Matendo ya Mitume 4:6

Annas the high priest was there, with Caiaphas, John, Alexander, and as many as were relatives of the high priest.

Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? Matendo ya Mitume 4:7

When they had stood them in the middle of them, they inquired, "By what power, or in what name, have you done this?"

Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, Matendo ya Mitume 4:8

Then Peter, filled with the Holy Spirit, said to them, "You rulers of the people, and elders of Israel,

kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, Matendo ya Mitume 4:9

if we are examined today concerning a good deed done to a crippled man, by what means this man has been healed,

jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Matendo ya Mitume 4:10

be it known to you all, and to all the people of Israel, that in the name of Jesus Christ of Nazareth, whom you crucified, whom God raised from the dead, in him does this man stand here before you whole.

Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Matendo ya Mitume 4:11

He is 'the stone which was regarded as worthless by you, the builders, which has become the head of the corner.'

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo ya Mitume 4:12

There is salvation in none other, for neither is there any other name under heaven, that is given among men, by which we must be saved!"

Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. Matendo ya Mitume 4:13

Now when they saw the boldness of Peter and John, and had perceived that they were unlearned and ignorant men, they marveled. They recognized that they had been with Jesus.

Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Matendo ya Mitume 4:14

Seeing the man who was healed standing with them, they could say nothing against it.

Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, Matendo ya Mitume 4:15

But when they had commanded them to go aside out of the council, they conferred among themselves,

wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. Matendo ya Mitume 4:16

saying, "What shall we do to these men? Because indeed a notable miracle has been done through them, as can be plainly seen by all who dwell in Jerusalem, and we can't deny it.

Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Matendo ya Mitume 4:17

But so that this spreads no further among the people, let's threaten them, that from now on they don't speak to anyone in this name."

Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Matendo ya Mitume 4:18

They called them, and charged them not to speak at all nor teach in the name of Jesus.

Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; Matendo ya Mitume 4:19

But Peter and John answered them, "Whether it is right in the sight of God to listen to you rather than to God, judge for yourselves,

maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Matendo ya Mitume 4:20

for we can't help telling the things which we saw and heard."

Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka; Matendo ya Mitume 4:21

When they had further threatened them, they let them go, finding no way to punish them, because of the people; for everyone glorified God for that which was done.

maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini. Matendo ya Mitume 4:22

For the man on whom this miracle of healing was performed was more than forty years old.

Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. Matendo ya Mitume 4:23

Being let go, they came to their own company, and reported all that the chief priests and the elders had said to them.

Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; Matendo ya Mitume 4:24

When they heard it, they lifted up their voice to God with one accord, and said, "O Lord, you are God, who made the heaven, the earth, the sea, and all that is in them;

nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili? Matendo ya Mitume 4:25

who by the mouth of your servant, David, said, 'Why do the nations rage, And the peoples plot a vain thing?

Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. Matendo ya Mitume 4:26

The kings of the earth take a stand, And the rulers take council together, Against the Lord, and against his Christ{Christ (Greek) and Messiah (Hebrew) both mean Anointed One. (Compare Psalm 2)}.'

Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, Matendo ya Mitume 4:27

For truly, in this city against your holy servant, Jesus, whom you anointed, both Herod and Pontius Pilate, with the Gentiles and the people of Israel, were gathered together

ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Matendo ya Mitume 4:28

to do whatever your hand and your council foreordained to happen.

Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, Matendo ya Mitume 4:29

Now, Lord, look at their threats, and grant to your servants to speak your word with all boldness,

ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Matendo ya Mitume 4:30

while you stretch out your hand to heal; and that signs and wonders may be done through the name of your holy Servant Jesus."

Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Matendo ya Mitume 4:31

When they had prayed, the place was shaken where they were gathered together. They were all filled with the Holy Spirit, and they spoke the word of God with boldness.

Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Matendo ya Mitume 4:32

The multitude of those who believed were of one heart and soul. Not one of them claimed that anything of the things which he possessed was his own, but they had all things in common.

Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Matendo ya Mitume 4:33

With great power, the apostles gave their testimony of the resurrection of the Lord Jesus. Great grace was on them all.

Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, Matendo ya Mitume 4:34

For neither was there among them any who lacked, for as many as were owners of lands or houses sold them, and brought the proceeds of the things that were sold,

wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Matendo ya Mitume 4:35

and laid them at the apostles' feet, and distribution was made to each, according as anyone had need.

Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, Matendo ya Mitume 4:36

Joses, who by the apostles was surnamed Barnabas (which is, being interpreted, Son of Encouragement), a Levite, a man of Cyprus by race,

alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. Matendo ya Mitume 4:37

having a field, sold it, and brought the money and laid it at the apostles' feet.