Matendo ya Mitume 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 2 (Swahili) Acts 2 (English)

Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Matendo ya Mitume 2:1

Now when the day of Pentecost had come, they were all with one accord in one place.

Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Matendo ya Mitume 2:2

Suddenly there came from the sky a sound like the rushing of a mighty wind, and it filled all the house where they were sitting.

Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Matendo ya Mitume 2:3

Tongues like fire appeared and were distributed to them, and one sat on each of them.

Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Matendo ya Mitume 2:4

They were all filled with the Holy Spirit, and began to speak with other languages, as the Spirit gave them the ability to speak.

Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Matendo ya Mitume 2:5

Now there were dwelling in Jerusalem Jews, devout men, from every nation under the sky.

Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Matendo ya Mitume 2:6

When this sound was heard, the multitude came together, and were bewildered, because everyone heard them speaking in his own language.

Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Matendo ya Mitume 2:7

They were all amazed and marveled, saying to one another, "Behold, aren't all these who speak Galileans?

Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Matendo ya Mitume 2:8

How do we hear, everyone in our own native language?

Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Matendo ya Mitume 2:9

Parthians, Medes, Elamites, and people from Mesopotamia, Judea, Cappadocia, Pontus, Asia,

Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Matendo ya Mitume 2:10

Phrygia, Pamphylia, Egypt, the parts of Libya around Cyrene, visitors from Rome, both Jews and proselytes,

Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. Matendo ya Mitume 2:11

Cretans and Arabians: we hear them speaking in our languages the mighty works of God!"

Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? Matendo ya Mitume 2:12

They were all amazed, and were perplexed, saying one to another, "What does this mean?"

Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. Matendo ya Mitume 2:13

Others, mocking, said, "They are filled with new wine."

Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. Matendo ya Mitume 2:14

But Peter, standing up with the eleven, lifted up his voice, and spoke out to them, "You men of Judea, and all you who dwell at Jerusalem, let this be known to you, and listen to my words.

Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; Matendo ya Mitume 2:15

For these aren't drunken, as you suppose, seeing it is only the third hour of the day{about 9:00 AM}.

lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, Matendo ya Mitume 2:16

But this is what has been spoken through the prophet Joel:

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Matendo ya Mitume 2:17

'It will be in the last days, says God, That I will pour out my Spirit on all flesh. Your sons and your daughters will prophesy. Your young men will see visions. Your old men will dream dreams.

Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. Matendo ya Mitume 2:18

Yes, and on my servants and on my handmaidens in those days, I will pour out my Spirit, and they will prophesy.

Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Matendo ya Mitume 2:19

I will show wonders in the sky above, And signs on the earth beneath; Blood, and fire, and billows of smoke.

Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. Matendo ya Mitume 2:20

The sun will be turned into darkness, And the moon into blood, Before the great and glorious day of the Lord comes.

Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Matendo ya Mitume 2:21

It will be, that whoever will call on the name of the Lord will be saved.'

Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; Matendo ya Mitume 2:22

"Men of Israel, hear these words! Jesus of Nazareth, a man approved by God to you by mighty works and wonders and signs which God did by him in the midst of you, even as you yourselves know,

mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; Matendo ya Mitume 2:23

him, being delivered up by the determined counsel and foreknowledge of God, you have taken by the hand of lawless men, crucified and killed;

ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Matendo ya Mitume 2:24

whom God raised up, having freed him from the agony of death, because it was not possible that he should be held by it.

Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. Matendo ya Mitume 2:25

For David says concerning him, 'I saw the Lord always before my face, For he is on my right hand, that I should not be moved.

Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. Matendo ya Mitume 2:26

Therefore my heart was glad, and my tongue rejoiced. Moreover my flesh also will dwell in hope;

Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. Matendo ya Mitume 2:27

Because you will not leave my soul in Hades, Neither will you allow your Holy One to see decay.

Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. Matendo ya Mitume 2:28

You made known to me the ways of life. You will make me full of gladness with your presence.'

Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. Matendo ya Mitume 2:29

"Brothers, I may tell you freely of the patriarch David, that he both died and was buried, and his tomb is with us to this day.

Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi; Matendo ya Mitume 2:30

Therefore, being a prophet, and knowing that God had sworn with an oath to him that of the fruit of his body, according to the flesh, he would raise up the Christ to sit on his throne,

yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. Matendo ya Mitume 2:31

he foreseeing this spoke about the resurrection of the Christ, that neither was his soul left in Hades, nor did his flesh see decay.

Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. Matendo ya Mitume 2:32

This Jesus God raised up, to which we all are witnesses.

Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. Matendo ya Mitume 2:33

Being therefore exalted by the right hand of God, and having received from the Father the promise of the Holy Spirit, he has poured out this, which you now see and hear.

Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume. Matendo ya Mitume 2:34

For David didn't ascend into the heavens, but he says himself, 'The Lord said to my Lord, "Sit by my right hand,

Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako. Matendo ya Mitume 2:35

Until I make your enemies a footstool for your feet."'

Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. Matendo ya Mitume 2:36

"Let all the house of Israel therefore know assuredly that God has made him both Lord and Christ, this Jesus whom you crucified."

Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Matendo ya Mitume 2:37

Now when they heard this, they were cut to the heart, and said to Peter and the rest of the apostles, "Brothers, what shall we do?"

Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 2:38

Peter said to them, "Repent, and be baptized, everyone of you, in the name of Jesus Christ for the forgiveness of sins, and you will receive the gift of the Holy Spirit.

Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Matendo ya Mitume 2:39

For to you is the promise, and to your children, and to all who are far off, even as many as the Lord our God will call to himself."

Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Matendo ya Mitume 2:40

With many other words he testified, and exhorted them, saying, "Save yourselves from this crooked generation!"

Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Matendo ya Mitume 2:41

Then those who gladly received his word were baptized. There were added that day about three thousand souls.

Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Matendo ya Mitume 2:42

They continued steadfastly in the apostles' teaching and fellowship, in the breaking of bread, and prayer.

Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Matendo ya Mitume 2:43

Fear came on every soul, and many wonders and signs were done through the apostles.

Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, Matendo ya Mitume 2:44

All who believed were together, and had all things in common.

wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Matendo ya Mitume 2:45

They sold their possessions and goods, and distributed them to all, according as anyone had need.

Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, Matendo ya Mitume 2:46

Day by day, continuing steadfastly with one accord in the temple, and breaking bread at home, they took their food with gladness and singleness of heart,

wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. Matendo ya Mitume 2:47

praising God, and having favor with all the people. The Lord added to the assembly day by day those who were being saved.