Yeremia 49 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 49 (Swahili) Jeremiah 49 (English)

Habari za wana wa Amoni. Bwana asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake? Yeremia 49:1

Of the children of Ammon. Thus says Yahweh: Has Israel no sons? has he no heir? why then does Malcam possess Gad, and his people well in the cities of it?

Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakaposikizisha mshindo wa vita juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema Bwana. Yeremia 49:2

Therefore, behold, the days come, says Yahweh, that I will cause an alarm of war to be heard against Rabbah of the children of Ammon; and it shall become a desolate heap, and her daughters shall be burned with fire: then shall Israel possess those who did possess him, says Yahweh.

Piga yowe, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja. Yeremia 49:3

Wail, Heshbon, for Ai is laid waste; cry, you daughters of Rabbah, gird you with sackcloth: lament, and run back and forth among the fences; for Malcam shall go into captivity, his priests and his princes together.

Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia? Yeremia 49:4

Why glory you in the valleys, your flowing valley, backsliding daughter? who trusted in her treasures, [saying], Who shall come to me?

Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, Bwana wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao. Yeremia 49:5

Behold, I will bring a fear on you, says the Lord, Yahweh of Hosts, from all who are round about you; and you shall be driven out every man right forth, and there shall be none to gather together the fugitives.

Lakini baada ya hayo nitawarudisha wana wa Amoni walio utumwani, asema Bwana. Yeremia 49:6

But afterward I will bring back the captivity of the children of Ammon, says Yahweh.

Habari za Edomu. Bwana wa majeshi asema hivi, Je! Hapana tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao? Yeremia 49:7

Of Edom. Thus says Yahweh of Hosts: Is wisdom no more in Teman? is counsel perished from the prudent? is their wisdom vanished?

Kimbieni, rudini nyuma, kaeni chini sana, enyi mnaokaa Dedani; maana nitaleta msiba wa Esau juu yake, wakati nitakapomwangalia. Yeremia 49:8

Flee you, turn back, dwell in the depths, inhabitants of Dedan; for I will bring the calamity of Esau on him, the time that I shall visit him.

Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wevi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha? Yeremia 49:9

If grape-gatherers came to you, would they not leave some gleaning grapes? if thieves by night, wouldn't they destroy until they had enough?

Lakini nimemwacha Esau hana kitu, nimepafunua mahali pake pa siri, wala hataweza kujificha; kizazi chake kimeangamizwa, na ndugu zake, na jirani zake, naye mwenyewe hayuko. Yeremia 49:10

But I have made Esau bare, I have uncovered his secret places, and he shall not be able to hide himself: his seed is destroyed, and his brothers, and his neighbors; and he is no more.

Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini mimi. Yeremia 49:11

Leave your fatherless children, I will preserve them alive; and let your widows trust in me.

Maana Bwana asema hivi, Tazama, wale wasioandikiwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa. Yeremia 49:12

For thus says Yahweh: Behold, they to whom it didn't pertain to drink of the cup shall assuredly drink; and are you he who shall altogether go unpunished? you shall not go unpunished, but you shall surely drink.

Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima. Yeremia 49:13

For I have sworn by myself, says Yahweh, that Bozrah shall become an astonishment, a reproach, a waste, and a curse; and all the cities of it shall be perpetual wastes.

Nimepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Jikusanyeni, mkaujie, Mkainuke kwenda vitani. Yeremia 49:14

I have heard news from Yahweh, and an ambassador is sent among the nations, [saying], Gather yourselves together, and come against her, and rise up to the battle.

Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa, Na kudharauliwa katika watu. Yeremia 49:15

For, behold, I have made you small among the nations, and despised among men.

Katika habari za kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana. Yeremia 49:16

As for your terror, the pride of your heart has deceived you, O you who dwell in the clefts of the rock, who hold the height of the hill: though you should make your nest as high as the eagle, I will bring you down from there, says Yahweh.

Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote. Yeremia 49:17

Edom shall become an astonishment: everyone who passes by it shall be astonished, and shall hiss at all the plagues of it.

Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema Bwana; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. Yeremia 49:18

As in the overthrow of Sodom and Gomorrah and the neighbor cities of it, says Yahweh, no man shall dwell there, neither shall any son of man sojourn therein.

Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu? Yeremia 49:19

Behold, he shall come up like a lion from the pride of the Jordan against the strong habitation: for I will suddenly make them run away from it; and whoever is chosen, him will I appoint over it: for who is like me? and who will appoint me a time? and who is the shepherd who will stand before me?

Basi, lisikieni shauri la Bwana; Alilolifanya juu ya Edomu; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu yao wakaao Temani; Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao. Yeremia 49:20

Therefore hear the counsel of Yahweh, that he has taken against Edom; and his purposes, that he has purposed against the inhabitants of Teman: Surely they shall drag them away, [even] the little ones of the flock; surely he shall make their habitation desolate over them.

Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao; Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu. Yeremia 49:21

The earth trembles at the noise of their fall; there is a cry, the noise which is heard in the Red Sea.

Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake. Yeremia 49:22

Behold, he shall come up and fly as the eagle, and spread out his wings against Bozrah: and the heart of the mighty men of Edom at that day shall be as the heart of a woman in her pangs.

Habari za Dameski. Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia; Maana wamesikia habari mbaya; Wameyeyuka kabisa; Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia. Yeremia 49:23

Of Damascus. Hamath is confounded, and Arpad; for they have heard evil news, they are melted away: there is sorrow on the sea; it can't be quiet.

Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake. Yeremia 49:24

Damascus has grown feeble, she turns herself to flee, and trembling has seized on her: anguish and sorrows have taken hold of her, as of a woman in travail.

Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu? Yeremia 49:25

How is the city of praise not forsaken, the city of my joy?

Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi. Yeremia 49:26

Therefore her young men shall fall in her streets, and all the men of war shall be brought to silence in that day, says Yahweh of Hosts.

Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi. Yeremia 49:27

I will kindle a fire in the wall of Damascus, and it shall devour the palaces of Ben Hadad.

Habari za Kedari, na za falme za Hazori, ambazo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alizipiga. Bwana asema hivi, Ondokeni, pandeni hata Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki. Yeremia 49:28

Of Kedar, and of the kingdoms of Hazor, which Nebuchadrezzar king of Babylon struck. Thus says Yahweh: Arise you, go up to Kedar, and destroy the children of the east.

Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia zao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote. Yeremia 49:29

Their tents and their flocks shall they take; they shall carry away for themselves their curtains, and all their vessels, and their camels; and they shall cry to them, Terror on every side!

Kimbieni ninyi, enendeni mbali mkitanga-tanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema Bwana; maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu. Yeremia 49:30

Flee you, wander far off, dwell in the depths, you inhabitants of Hazor, says Yahweh; for Nebuchadrezzar king of Babylon has taken counsel against you, and has conceived a purpose against you.

Ondokeni, pandeni hata taifa lililo katika hali ya raha, likaalo bila kuhangaika, asema Bwana; wasio na malango wala makomeo, wakaao peke yao. Yeremia 49:31

Arise, go up to a nation that is at ease, that dwells without care, says Yahweh; that have neither gates nor bars, that dwell alone.

Na ngamia zao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya hata pepo zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema Bwana. Yeremia 49:32

Their camels shall be a booty, and the multitude of their cattle a spoil: and I will scatter to all winds those who have the corners [of their hair] cut off; and I will bring their calamity from every side of them, says Yahweh.

Na Hazori utakuwa kao la mbwa-mwitu; ukiwa milele; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. Yeremia 49:33

Hazor shall be a dwelling-place of jackals, a desolation forever: no man shall dwell there, neither shall any son of man sojourn therein.

Neno la Bwana lililomjia Yeremia, nabii, juu ya Elamu, mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, kusema, Yeremia 49:34

The word of Yahweh that came to Jeremiah the prophet concerning Elam, in the beginning of the reign of Zedekiah king of Judah, saying,

Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama nitauvunja upinde wa Elamu, ulio mkuu katika nguvu zao. Yeremia 49:35

Thus says Yahweh of Hosts: Behold, I will break the bow of Elam, the chief of their might.

Na juu ya Elamu nitazileta pepo nne, toka pembe nne za mbinguni, nami nitawatawanya hata pepo nne zote, wala hapana taifa ambalo hawatalifikilia watu wa Elamu waliofukuzwa. Yeremia 49:36

On Elam will I bring the four winds from the four quarters of the sky, and will scatter them toward all those winds; and there shall be no nation where the outcasts of Elam shall not come.

Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema Bwana; nami nitautuma upanga uwafuatie, hata nitakapowaangamiza; Yeremia 49:37

I will cause Elam to be dismayed before their enemies, and before those who seek their life; and I will bring evil on them, even my fierce anger, says Yahweh; and I will send the sword after them, until I have consumed them;

nami nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu, nami nitawaharibu, mfalme na wakuu, watoke huko, asema Bwana. Yeremia 49:38

and I will set my throne in Elam, and will destroy from there king and princes, says Yahweh.

Lakini itakuwa, katika siku za mwisho, nitawarudisha wafungwa wa Elamu, asema Bwana. Yeremia 49:39

But it shall happen in the latter days, that I will bring back the captivity of Elam, says Yahweh.