Yeremia 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 28 (Swahili) Jeremiah 28 (English)

Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya Bwana, mbele ya makuhani na watu wote, akisema, Yeremia 28:1

It happened the same year, in the beginning of the reign of Zedekiah king of Judah, in the fourth year, in the fifth month, that Hananiah the son of Azzur, the prophet, who was of Gibeon, spoke to me in the house of Yahweh, in the presence of the priests and of all the people, saying,

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli. Yeremia 28:2

Thus speaks Yahweh of Hosts, the God of Israel, saying, I have broken the yoke of the king of Babylon.

Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli. Yeremia 28:3

Within two full years will I bring again into this place all the vessels of Yahweh's house, that Nebuchadnezzar king of Babylon took away from this place, and carried to Babylon:

Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema Bwana; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. Yeremia 28:4

and I will bring again to this place Jeconiah the son of Jehoiakim, king of Judah, with all the captives of Judah, who went to Babylon, says Yahweh; for I will break the yoke of the king of Babylon.

Ndipo nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, mbele ya makuhani, na mbele ya watu wote waliosimama ndani ya nyumba ya Bwana, Yeremia 28:5

Then the prophet Jeremiah said to the prophet Hananiah in the presence of the priests, and in the presence of all the people who stood in the house of Yahweh,

naam, nabii Yeremia akasema, Amina, Bwana na atende hivi; Bwana ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya Bwana na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa. Yeremia 28:6

even the prophet Jeremiah said, Amen: Yahweh do so; Yahweh perform your words which you have prophesied, to bring again the vessels of Yahweh's house, and all them of the captivity, from Babylon to this place.

Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, Yeremia 28:7

Nevertheless hear you now this word that I speak in your ears, and in the ears of all the people:

Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni. Yeremia 28:8

The prophets who have been before me and before you of old prophesied against many countries, and against great kingdoms, of war, and of evil, and of pestilence.

Nabii atabiriye habari za amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa Bwana amemtuma kweli kweli. Yeremia 28:9

The prophet who prophesies of peace, when the word of the prophet shall happen, then shall the prophet be known, that Yahweh has truly sent him.

Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja. Yeremia 28:10

Then Hananiah the prophet took the bar from off the prophet Jeremiah's neck, and broke it.

Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake. Yeremia 28:11

Hananiah spoke in the presence of all the people, saying, Thus says Yahweh: Even so will I break the yoke of Nebuchadnezzar king of Babylon within two full years from off the neck of all the nations. The prophet Jeremiah went his way.

Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia, baada ya Hanania, nabii, kuivunja ile nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, kusema, Yeremia 28:12

Then the word of Yahweh came to Jeremiah, after that Hananiah the prophet had broken the bar from off the neck of the prophet Jeremiah, saying,

Enenda ukamwambie Hanania, ukisema, Bwana asema hivi, Umezivunja nira za mti; lakini badala yake utafanya nira za chuma. Yeremia 28:13

Go, and tell Hananiah, saying, Thus says Yahweh: You have broken the bars of wood; but you have made in their place bars of iron.

Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo ya mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia. Yeremia 28:14

For thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel: I have put a yoke of iron on the neck of all these nations, that they may serve Nebuchadnezzar king of Babylon; and they shall serve him: and I have given him the animals of the field also.

Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo. Yeremia 28:15

Then said the prophet Jeremiah to Hananiah the prophet, Hear now, Hananiah: Yahweh has not sent you; but you make this people to trust in a lie.

Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana. Yeremia 28:16

Therefore thus says Yahweh, Behold, I will send you away from off the surface of the earth: this year you shall die, because you have spoken rebellion against Yahweh.

Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba. Yeremia 28:17

So Hananiah the prophet died the same year in the seventh month.