Yeremia 47 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 47 (Swahili) Jeremiah 47 (English)

Neno la Bwana lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. Yeremia 47:1

The word of Yahweh that came to Jeremiah the prophet concerning the Philistines, before that Pharaoh struck Gaza.

Bwana asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe. Yeremia 47:2

Thus says Yahweh: Behold, waters rise up out of the north, and shall become an overflowing stream, and shall overflow the land and all that is therein, the city and those who dwell therein; and the men shall cry, and all the inhabitants of the land shall wail.

Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu; Yeremia 47:3

At the noise of the stamping of the hoofs of his strong ones, at the rushing of his chariots, at the rumbling of his wheels, the fathers don't look back to their children for feebleness of hands;

kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana Bwana atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori. Yeremia 47:4

because of the day that comes to destroy all the Philistines, to cut off from Tyre and Sidon every helper who remains: for Yahweh will destroy the Philistines, the remnant of the isle of Caphtor.

Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikata-kata? Yeremia 47:5

Baldness is come on Gaza; Ashkelon is brought to nothing, the remnant of their valley: how long will you cut yourself?

Ee upanga wa Bwana, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie. Yeremia 47:6

You sword of Yahweh, how long will it be before you be quiet? put up yourself into your scabbard; rest, and be still.

Utawezaje kutulia, Ikiwa Bwana amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo. Yeremia 47:7

How can you be quiet, seeing Yahweh has given you a charge? Against Ashkelon, and against the sea-shore, there has he appointed it.