Yeremia 37 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 37 (Swahili) Jeremiah 37 (English)

Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki badala ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadreza amemmilikisha katika nchi ya Yuda. Yeremia 37:1

Zedekiah the son of Josiah reigned as king, instead of Coniah the son of Jehoiakim, whom Nebuchadrezzar king of Babylon made king in the land of Judah.

Lakini yeye, wala watumishi wake, wala watu wa nchi, hawakuyasikiliza maneno ya Bwana aliyonena kwa kinywa cha nabii Yeremia. Yeremia 37:2

But neither he, nor his servants, nor the people of the land, did listen to the words of Yahweh, which he spoke by the prophet Jeremiah.

Sedekia, mfalme, akamtuma Yehukali, mwana wa Shelemia, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kwa Yeremia, nabii, kusema, Utuombee sasa kwa Bwana, Mungu wetu. Yeremia 37:3

Zedekiah the king sent Jehucal the son of Shelemiah, and Zephaniah the son of Maaseiah, the priest, to the prophet Jeremiah, saying, Pray now to Yahweh our God for us.

Basi Yeremia alikuwa akiingia na kutoka kati ya watu; kwa maana walikuwa hawakumfunga gerezani. Yeremia 37:4

Now Jeremiah came in and went out among the people; for they had not put him into prison.

Na jeshi la Farao lilikuwa limetoka nchi ya Misri; na Wakaldayo waliohusuru Yerusalemu, waliposikia habari zao, wakavunja kambi yao mbele ya Yerusalemu. Yeremia 37:5

Pharaoh's army was come forth out of Egypt; and when the Chaldeans who were besieging Jerusalem heard news of them, they broke up from Jerusalem.

Ndipo neno la Bwana likamjia nabii Yeremia, kusema, Yeremia 37:6

Then came the word of Yahweh to the prophet Jeremiah, saying,

Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mtamwambia hivi mfalme wa Yuda, aliyewatuma kwangu kuniuliza; Angalieni, jeshi la Farao, ambalo linakuja kuwasaidia, litarudi Misri, nchi yao wenyewe. Yeremia 37:7

Thus says Yahweh, the God of Israel, Thus shall you tell the king of Judah, who sent you to me to inquire of me: Behold, Pharaoh's army, which is come forth to help you, shall return to Egypt into their own land.

Na Wakaldayo watakuja tena, na kupigana na mji huu; nao watautwaa, na kuuteketeza. Yeremia 37:8

The Chaldeans shall come again, and fight against this city; and they shall take it, and burn it with fire.

Bwana asema hivi, Msijidanganye mkisema, Bila shaka Wakaldayo watatuacha na kwenda zao; maana hawatawaacha. Yeremia 37:9

Thus says Yahweh, Don't deceive yourselves, saying, The Chaldeans shall surely depart from us; for they shall not depart.

Maana mngelipiga jeshi lote la Wakaldayo wanaopigana nanyi, wakabaki kati yao watu waliojeruhiwa tu, hata hivyo wangeondoka kila mtu katika hema yake, na kuuteketeza mji huu. Yeremia 37:10

For though you had struck the whole army of the Chaldeans who fight against you, and there remained but wounded men among them, yes would they rise up every man in his tent, and burn this city with fire.

Hata ikawa, jeshi la Wakaldayo lilipokuwa limevunja kambi yao mbele ya Yerusalemu, kwa kuliogopa jeshi la Farao, Yeremia 37:11

It happened that, when the army of the Chaldeans was broken up from Jerusalem for fear of Pharaoh's army,

ndipo Yeremia akatoka Yerusalemu, ili aende mpaka nchi ya Benyamini, alipokee huko fungu lake kati ya watu. Yeremia 37:12

then Jeremiah went forth out of Jerusalem to go into the land of Benjamin, to receive his portion there, in the midst of the people.

Naye alipokuwa katika lango la Benyamini, akida wa walinzi alikuwapo, jina lake Iriya, mwana wa Shelemia, mwana wa Hanania; akamkamata Yeremia, nabii, akisema, Unakwenda kujiunga na Wakaldayo. Yeremia 37:13

When he was in the gate of Benjamin, a captain of the guard was there, whose name was Irijah, the son of Shelemiah, the son of Hananiah; and he laid hold on Jeremiah the prophet, saying, You are falling away to the Chaldeans.

Ndipo Yeremia akasema, Ni uongo, siendi kujiunga na Wakaldayo; lakini yeye asimsadiki; basi Iriya akamkamata Yeremia, akamleta kwa wakuu. Yeremia 37:14

Then said Jeremiah, It is false; I am not falling away to the Chaldeans. But he didn't listen to him; so Irijah laid hold on Jeremiah, and brought him to the princes.

Nao wakuu wakamkasirikia Yeremia, wakampiga, wakamtia gerezani katika nyumba ya Yonathani, mwandishi; kwa maana ndiyo waliyoifanya kuwa gereza. Yeremia 37:15

The princes were angry with Jeremiah, and struck him, and put him in prison in the house of Jonathan the scribe; for they had made that the prison.

Basi, Yeremia alipokuwa ameingia katika nyumba ya shimo, na katika vyumba vya ndani; na Yeremia alipokuwa amekaa humo siku nyingi; Yeremia 37:16

When Jeremiah was come into the dungeon-house, and into the cells, and Jeremiah had remained there many days;

ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa Bwana? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli. Yeremia 37:17

Then Zedekiah the king sent, and fetched him: and the king asked him secretly in his house, and said, Is there any word from Yahweh? Jeremiah said, There is. He said also, You shall be delivered into the hand of the king of Babylon.

Pamoja na haya Yeremia akamwambia mfalme Sedekia, Nimefanya kosa gani juu yako, au juu ya watumishi wako, au juu ya watu hawa, hata mkanitia gerezani? Yeremia 37:18

Moreover Jeremiah said to king Zedekiah, Wherein have I sinned against you, or against your servants, or against this people, that you have put me in prison?

Wako wapi sasa manabii wenu waliowatabiria, wakisema, Mfalme wa Babeli hatakuja juu yenu, wala juu ya nchi hii? Yeremia 37:19

Where now are your prophets who prophesied to you, saying, The king of Babylon shall not come against you, nor against this land?

Na sasa unisikilize, Ee bwana wangu mfalme; maombi yangu yakapate kibali mbele yako; usinirudishe nyumbani mwa Yonathani, mwandishi, nisije nikafa humo. Yeremia 37:20

Now please hear, my lord the king: please let my supplication be presented before you, that you not cause me to return to the house of Jonathan the scribe, lest I die there.

Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika uwanda wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika uwanda wa walinzi. Yeremia 37:21

Then Zedekiah the king commanded, and they committed Jeremiah into the court of the guard; and they gave him daily a loaf of bread out of the bakers' street, until all the bread in the city was spent. Thus Jeremiah remained in the court of the guard.