Yeremia 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 21 (Swahili) Jeremiah 21 (English)

Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, hapo mfalme Sedekia alipompelekea Pashuri, mwana wa Malkiya, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kusema, Yeremia 21:1

The word which came to Jeremiah from Yahweh, when king Zedekiah sent to him Pashhur the son of Malchijah, and Zephaniah the son of Maaseiah, the priest, saying,

Tafadhali utuulizie habari kwa Bwana; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda Bwana atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache. Yeremia 21:2

Please inquire of Yahweh for us; for Nebuchadrezzar king of Babylon makes war against us: peradventure Yahweh will deal with us according to all his wondrous works, that he may go up from us.

Basi Yeremia akawaambia, Mwambieni Sedekia neno hili, Yeremia 21:3

Then said Jeremiah to them, Thus shall you tell Zedekiah:

Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu. Yeremia 21:4

Thus says Yahweh, the God of Israel, Behold, I will turn back the weapons of war that are in your hands, with which you fight against the king of Babylon, and against the Chaldeans who besiege you, without the walls; and I will gather them into the midst of this city.

Na mimi mwenyewe nitapigana nanyi, kwa mkono ulionyoshwa na kwa mkono hodari, naam, kwa hasira, na kwa ukali, na kwa ghadhabu nyingi. Yeremia 21:5

I myself will fight against you with an outstretched hand and with a strong arm, even in anger, and in wrath, and in great indignation.

Nami nitawapiga wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama pia; watakufa kwa tauni kubwa. Yeremia 21:6

I will strike the inhabitants of this city, both man and animal: they shall die of a great pestilence.

Na baada ya hayo, asema Bwana, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu. Yeremia 21:7

Afterward, says Yahweh, I will deliver Zedekiah king of Judah, and his servants, and the people, even such as are left in this city from the pestilence, from the sword, and from the famine, into the hand of Nebuchadrezzar king of Babylon, and into the hand of their enemies, and into the hand of those who seek their life: and he shall strike them with the edge of the sword; he shall not spare them, neither have pity, nor have mercy.

Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. Yeremia 21:8

To this people you shall say, Thus says Yahweh: Behold, I set before you the way of life and the way of death.

Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake. Yeremia 21:9

He who remains in this city shall die by the sword, and by the famine, and by the pestilence; but he who goes out, and passes over to the Chaldeans who besiege you, he shall live, and his life shall be to him for a prey.

Maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema Bwana; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza. Yeremia 21:10

For I have set my face on this city for evil, and not for good, says Yahweh: it shall be given into the hand of the king of Babylon, and he shall burn it with fire.

Na katika habari za nyumba ya mfalme wa Yuda, lisikieni neno la Bwana, Yeremia 21:11

Touching the house of the king of Judah, hear you the word of Yahweh:

Ee nyumba ya Daudi, Bwana asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu ye yote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu. Yeremia 21:12

House of David, thus says Yahweh, Execute justice in the morning, and deliver him who is robbed out of the hand of the oppressor, lest my wrath go forth like fire, and burn so that none can quench it, because of the evil of your doings.

Tazama, mimi ni juu yako, Ewe ukaaye bondeni, na kwenye jabali la uwandani, asema Bwana ninyi mnaosema, Ni nani atakayeshuka apigane nasi? Au, Ni nani atakayeingia katika makao yetu? Yeremia 21:13

Behold, I am against you, O inhabitant of the valley, [and] of the rock of the plain, says Yahweh; you that say, Who shall come down against us? or who shall enter into our habitations?

Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matunda ya matendo yenu, asema Bwana; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo. Yeremia 21:14

I will punish you according to the fruit of your doings, says Yahweh; and I will kindle a fire in her forest, and it shall devour all that is round about her.