Yeremia 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 31 (Swahili) Jeremiah 31 (English)

Wakati huo, asema Bwana, nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu. Yeremia 31:1

At that time, says Yahweh, will I be the God of all the families of Israel, and they shall be my people.

Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha. Yeremia 31:2

Thus says Yahweh, The people who were left of the sword found favor in the wilderness; even Israel, when I went to cause him to rest.

Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Yeremia 31:3

Yahweh appeared of old to me, [saying], Yes, I have loved you with an everlasting love: therefore with loving kindness have I drawn you.

Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Yeremia 31:4

Again will I build you, and you shall be built, O virgin of Israel: again shall you be adorned with your tambourines, and shall go forth in the dances of those who make merry.

Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake. Yeremia 31:5

Again shall you plant vineyards on the mountains of Samaria; the planters shall plant, and shall enjoy [the fruit of it].

Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu. Yeremia 31:6

For there shall be a day, that the watchmen on the hills of Ephraim shall cry, Arise you, and let us go up to Zion to Yahweh our God.

Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli. Yeremia 31:7

For thus says Yahweh, Sing with gladness for Jacob, and shout for the chief of the nations: publish you, praise you, and say, Yahweh, save your people, the remnant of Israel.

Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa. Yeremia 31:8

Behold, I will bring them from the north country, and gather them from the uttermost parts of the earth, [and] with them the blind and the lame, the woman with child and her who travails with child together: a great company shall they return here.

Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu. Yeremia 31:9

They shall come with weeping; and with petitions will I lead them: I will cause them to walk by rivers of waters, in a straight way in which they shall not stumble; for I am a father to Israel, and Ephraim is my firstborn.

Lisikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake. Yeremia 31:10

Hear the word of Yahweh, you nations, and declare it in the isles afar off; and say, He who scattered Israel will gather him, and keep him, as shepherd does his flock.

Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye. Yeremia 31:11

For Yahweh has ransomed Jacob, and redeemed him from the hand of him who was stronger than he.

Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa. Yeremia 31:12

They shall come and sing in the height of Zion, and shall flow to the goodness of Yahweh, to the grain, and to the new wine, and to the oil, and to the young of the flock and of the herd: and their soul shall be as a watered garden; and they shall not sorrow any more at all.

Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao. Yeremia 31:13

Then shall the virgin rejoice in the dance, and the young men and the old together; for I will turn their mourning into joy, and will comfort them, and make them rejoice from their sorrow.

Nami nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono, na watu wangu watashiba kwa wema wangu, asema Bwana Yeremia 31:14

I will satiate the soul of the priests with fatness, and my people shall be satisfied with my goodness, says Yahweh.

Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako, Yeremia 31:15

Thus says Yahweh: A voice is heard in Ramah, lamentation, and bitter weeping, Rachel weeping for her children; she refuses to be comforted for her children, because they are no more.

Bwana asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo Bwana. Yeremia 31:16

Thus says Yahweh: Refrain your voice from weeping, and your eyes from tears; for your work shall be rewarded, says Yahweh; and they shall come again from the land of the enemy.

Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe. Yeremia 31:17

There is hope for your latter end, says Yahweh; and [your] children shall come again to their own border.

Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoelea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu. Yeremia 31:18

I have surely heard Ephraim bemoaning himself [thus], You have chastised me, and I was chastised, as a calf unaccustomed [to the yoke]: turn you me, and I shall be turned; for you are Yahweh my God.

Hakika baada ya kugeuzwa kwangu, nalitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga pajani; nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wangu. Yeremia 31:19

Surely after that I was turned, I repented; and after that I was instructed, I struck on my thigh: I was ashamed, yes, even confounded, because I did bear the reproach of my youth.

Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema Bwana. Yeremia 31:20

Is Ephraim my dear son? is he a darling child? for as often as I speak against him, I do earnestly remember him still: therefore my heart yearns for him; I will surely have mercy on him, says Yahweh.

Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa Israeli, irudie hii miji yako. Yeremia 31:21

Set up road signs, make guideposts; set your heart toward the highway, even the way by which you went: turn again, virgin of Israel, turn again to these your cities.

Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume. Yeremia 31:22

How long will you go here and there, you backsliding daughter? for Yahweh has created a new thing in the earth: a woman shall encompass a man.

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Watatumia tena neno hili katika nchi ya Yuda, na katika miji yake, nitakapowarudisha mateka yao; Bwana na akubariki, Ee kao la haki, Ee mlima wa utakatifu. Yeremia 31:23

Thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel, Yet again shall they use this speech in the land of Judah and in the cities of it, when I shall bring again their captivity: Yahweh bless you, habitation of righteousness, mountain of holiness.

Na Yuda, na miji yake yote, watakaa humo pamoja; wakulima, nao waendao huko na huko pamoja na makundi yao. Yeremia 31:24

Judah and all the cities of it shall dwell therein together, the farmers, and those who go about with flocks.

Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni. Yeremia 31:25

For I have satiated the weary soul, and every sorrowful soul have I replenished.

Basi, nikaamka, nikaangalia; na usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu. Yeremia 31:26

On this I awakened, and saw; and my sleep was sweet to me.

Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama. Yeremia 31:27

Behold, the days come, says Yahweh, that I will sow the house of Israel and the house of Judah with the seed of man, and with the seed of animal.

Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung'oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema Bwana. Yeremia 31:28

It shall happen that, like as I have watched over them to pluck up and to break down and to overthrow and to destroy and to afflict, so will I watch over them to build and to plant, says Yahweh.

Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Yeremia 31:29

In those days they shall say no more, The fathers have eaten sour grapes, and the children's teeth are set on edge.

Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi. Yeremia 31:30

But everyone shall die for his own iniquity: every man who eats the sour grapes, his teeth shall be set on edge.

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Yeremia 31:31

Behold, the days come, says Yahweh, that I will make a new covenant with the house of Israel, and with the house of Judah:

Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Yeremia 31:32

not according to the covenant that I made with their fathers in the day that I took them by the hand to bring them out of the land of Egypt; which my covenant they broke, although I was a husband to them, says Yahweh.

Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Yeremia 31:33

But this is the covenant that I will make with the house of Israel after those days, says Yahweh: I will put my law in their inward parts, and in their heart will I write it; and I will be their God, and they shall be my people:

Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena. Yeremia 31:34

and they shall teach no more every man his neighbor, and every man his brother, saying, Know Yahweh; for they shall all know me, from the least of them to the greatest of them, says Yahweh: for I will forgive their iniquity, and their sin will I remember no more.

Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi, ndilo jina lake; Yeremia 31:35

Thus says Yahweh, who gives the sun for a light by day, and the ordinances of the moon and of the stars for a light by night, who stirs up the sea, so that the waves of it roar; Yahweh of hosts is his name:

Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele. Yeremia 31:36

If these ordinances depart from before me, says Yahweh, then the seed of Israel also shall cease from being a nation before me forever.

Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema Bwana. Yeremia 31:37

Thus says Yahweh: If heaven above can be measured, and the foundations of the earth searched out beneath, then will I also cast off all the seed of Israel for all that they have done, says Yahweh.

Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, mji huu utakapojengwa kwa ajili ya Bwana, toka buruji ya Hananeli hata lango la pembeni. Yeremia 31:38

Behold, the days come, says Yahweh, that the city shall be built to Yahweh from the tower of Hananel to the gate of the corner.

Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hata mlima Garebu, tena itazunguka na kufika Goa. Yeremia 31:39

The measuring line shall go out further straight onward to the hill Gareb, and shall turn about to Goah.

Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa Bwana; hapatang'olewa, wala hapatabomolewa, hata milele. Yeremia 31:40

The whole valley of the dead bodies and of the ashes, and all the fields to the brook Kidron, to the corner of the horse gate toward the east, shall be holy to Yahweh; it shall not be plucked up, nor thrown down any more forever.