Yeremia 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 17 (Swahili) Jeremiah 17 (English)

Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu; Yeremia 17:1

The sin of Judah is written with a pen of iron, [and] with the point of a diamond: it is engraved on the tablet of their heart, and on the horns of your altars;

na wakati huo watoto wao wazikumbuka madhabahu zao, na maashera yao, karibu na miti yenye majani mabichi juu ya milima mirefu. Yeremia 17:2

while their children remember their altars and their Asherim by the green trees on the high hills.

Ee mlima wangu wa uwandani, nitatoa mali zako na hazina zako zote ziwe nyara, na mahali pako palipoinuka, kwa sababu ya dhambi, katika mipaka yako yote. Yeremia 17:3

My mountain in the field, I will give your substance and all your treasures for a spoil, [and] your high places, because of sin, throughout all your borders.

Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele. Yeremia 17:4

You, even of yourself, shall discontinue from your heritage that I gave you; and I will cause you to serve your enemies in the land which you don't know: for you have kindled a fire in my anger which shall burn forever.

Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. Yeremia 17:5

Thus says Yahweh: Cursed is the man who trusts in man, and makes flesh his arm, and whose heart departs from Yahweh.

Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Yeremia 17:6

For he shall be like the heath in the desert, and shall not see when good comes, but shall inhabit the parched places in the wilderness, a salt land and not inhabited.

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. Yeremia 17:7

Blessed is the man who trusts in Yahweh, and whose trust Yahweh is.

Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. Yeremia 17:8

For he shall be as a tree planted by the waters, who spreads out its roots by the river, and shall not fear when heat comes, but its leaf shall be green; and shall not be careful in the year of drought, neither shall cease from yielding fruit.

Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Yeremia 17:9

The heart is deceitful above all things, and it is exceedingly corrupt: who can know it?

Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. Yeremia 17:10

I, Yahweh, search the mind, I try the heart, even to give every man according to his ways, according to the fruit of his doings.

Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa mpumbavu. Yeremia 17:11

As the partridge that sits on [eggs] which she has not laid, so is he who gets riches, and not by right; in the midst of his days they shall leave him, and at his end he shall be a fool.

Kiti cha enzi, cha utukufu, kilichowekwa juu tangu mwanzo, ndicho mahali patakatifu petu. Yeremia 17:12

A glorious throne, [set] on high from the beginning, is the place of our sanctuary.

Ee Bwana, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha Bwana, kisima cha maji yaliyo hai. Yeremia 17:13

Yahweh, the hope of Israel, all who forsake you shall be disappointed. Those who depart from me shall be written in the earth, because they have forsaken Yahweh, the spring of living waters.

Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu. Yeremia 17:14

Heal me, O Yahweh, and I shall be healed; save me, and I shall be saved: for you are my praise.

Tazama, wao waniambia, Neno la Bwana liko wapi? Na lije, basi. Yeremia 17:15

Behold, they tell me, Where is the word of Yahweh? let it come now.

Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kufisha; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako. Yeremia 17:16

As for me, I have not hurried from being a shepherd after you; neither have I desired the woeful day; you know: that which came out of my lips was before your face.

Usiwe sababu ya hofu kuu kwangu mimi; wewe ndiwe uliye kimbilio langu siku ya uovu. Yeremia 17:17

Don't be a terror to me: you are my refuge in the day of evil.

Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu. Yeremia 17:18

Let them be disappointed who persecute me, but let not me be disappointed; let them be dismayed, but don't let me be dismayed; bring on them the day of evil, and destroy them with double destruction.

Bwana akaniambia hivi, Enenda ukasimame katika lango la wana wa watu hawa, waingiapo wafalme wa Yuda, na watokeapo, na katika malango yote ya Yerusalemu, Yeremia 17:19

Thus said Yahweh to me: Go, and stand in the gate of the children of the people, through which the kings of Judah come in, and by which they go out, and in all the gates of Jerusalem;

ukawaambie, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na Yuda wote, nanyi wenyeji wote wa Yerusalemu, ninyi mwingiao kwa malango haya; Yeremia 17:20

and tell them, Hear you the word of Yahweh, you kings of Judah, and all Judah, and all the inhabitants of Jerusalem, that enter in by these gates:

Bwana asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wo wote siku ya sabato, wala msiulete ndani kwa malango ya Yerusalemu; Yeremia 17:21

Thus says Yahweh, Take heed to yourselves, and bear no burden on the Sabbath day, nor bring it in by the gates of Jerusalem;

wala msitoe mzigo katika nyumba zenu siku ya sabato, wala msifanye kazi yo yote; bali itakaseni siku ya sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu; Yeremia 17:22

neither carry forth a burden out of your houses on the Sabbath day holy, neither do any work: but make the Sabbath day, as I commanded your fathers.

lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, ili wasisikilize wala wasipokee mafundisho. Yeremia 17:23

But they didn't listen, neither turn their ear, but made their neck stiff, that they might not hear, and might not receive instruction.

Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema Bwana, msiingize mzigo wo wote kwa malango ya mji huu siku ya sabato, bali mkiitakasa siku ya sabato, bila kufanya kazi yo yote siku hiyo; Yeremia 17:24

It shall happen, if you diligently listen to me, says Yahweh, to bring in no burden through the gates of this city on the Sabbath day, but to make the Sabbath day holy, to do no work therein;

ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele. Yeremia 17:25

then shall there enter in by the gates of this city kings and princes sitting on the throne of David, riding in chariots and on horses, they, and their princes, the men of Judah, and the inhabitants of Jerusalem; and this city shall remain forever.

Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, na milima,na upande wa Negebu,wakileta sadaka za kuteketezwa,na dhabihu,na sadaka za unga,na ubani,wakileta pia sadaka za shukurani,nyumbani kwa BWANA. Yeremia 17:26

They shall come from the cities of Judah, and from the places round about Jerusalem, and from the land of Benjamin, and from the lowland, and from the hill-country, and from the South, bringing burnt offerings, and sacrifices, and meal-offerings, and frankincense, and bringing [sacrifices of] thanksgiving, to the house of Yahweh.

Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo na kuingia kwa malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika. Yeremia 17:27

But if you will not listen to me to make the Sabbath day holy, and not to bear a burden and enter in at the gates of Jerusalem on the Sabbath day; then will I kindle a fire in the gates of it, and it shall devour the palaces of Jerusalem, and it shall not be quenched.