Yeremia 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 25 (Swahili) Jeremiah 25 (English)

Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, katika habari za watu wote wa Yuda; katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda mwaka ule ndio mwaka wa kwanza wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli; Yeremia 25:1

The word that came to Jeremiah concerning all the people of Judah, in the fourth year of Jehoiakim the son of Josiah, king of Judah (the same was the first year of Nebuchadrezzar king of Babylon),

ambalo Yeremia, nabii, aliwaambia watu wote wa Yuda, na wenyeji wote wa Yerusalemu, kusema, Yeremia 25:2

which Jeremiah the prophet spoke to all the people of Judah, and to all the inhabitants of Jerusalem, saying:

Tangu mwaka wa kumi na tatu wa kutawala kwake Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, hata siku hii ya leo, miaka hii ishirini na mitatu, neno la Bwana limenijia, nami nimesema nanyi, nikiamka mapema na kusema; lakini ninyi hamkusikiliza. Yeremia 25:3

From the thirteenth year of Josiah the son of Amon, king of Judah, even to this day, these twenty-three years, the word of Yahweh has come to me, and I have spoken to you, rising up early and speaking; but you have not listened.

Naye Bwana ametuma kwenu watumishi wake wote, hao manabii, akiamka mapema na kuwatuma, lakini ninyi hamkusikiliza, wala hamkutega masikio yenu, msikilize. Yeremia 25:4

Yahweh has sent to you all his servants the prophets, rising up early and sending them, (but you have not listened, nor inclined your ear to hear),

Akasema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya; uacheni uovu wa matendo yenu, mkae katika nchi ambayo Bwana aliwapa, ninyi na baba zenu, tangu zamani za kale na hata milele; Yeremia 25:5

saying, Return you now everyone from his evil way, and from the evil of your doings, and dwell in the land that Yahweh has given to you and to your fathers, from of old and even forevermore;

wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia na kuwasujudia, wala msinikasirishe kwa kazi ya mikono yenu; basi, mimi sitawadhuru ninyi kwa dhara lo lote. Yeremia 25:6

and don't go after other gods to serve them or worship them, and don't provoke me to anger with the work of your hands; and I will do you no harm.

Lakini ninyi hamkunisikiliza, asema Bwana; ili mnikasirishe kwa kazi ya mikono yenu, na kujidhuru nafsi zenu. Yeremia 25:7

Yet you have not listened to me, says Yahweh; that you may provoke me to anger with the work of your hands to your own hurt.

Basi Bwana wa majeshi asema hivi, Kwa kuwa hamkuyasikiliza maneno yangu, Yeremia 25:8

Therefore thus says Yahweh of Hosts: Because you have not heard my words,

angalieni, nitapeleka watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema Bwana, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyopo pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima. Yeremia 25:9

behold, I will send and take all the families of the north, says Yahweh, and [I will send] to Nebuchadrezzar the king of Babylon, my servant, and will bring them against this land, and against the inhabitants of it, and against all these nations round about; and I will utterly destroy them, and make them an astonishment, and a hissing, and perpetual desolations.

Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na nuru ya mishumaa. Yeremia 25:10

Moreover I will take from them the voice of mirth and the voice of gladness, the voice of the bridegroom and the voice of the bride, the sound of the millstones, and the light of the lamp.

Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini. Yeremia 25:11

This whole land shall be a desolation, and an astonishment; and these nations shall serve the king of Babylon seventy years.

Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema Bwana, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele. Yeremia 25:12

It shall happen, when seventy years are accomplished, that I will punish the king of Babylon, and that nation, says Yahweh, for their iniquity, and the land of the Chaldeans; and I will make it desolate forever.

Nami nitaleta juu ya nchi ile maneno yangu yote niliyoyanena juu yake, naam, yote yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki, aliyotabiri Yeremia juu ya mataifa haya yote. Yeremia 25:13

I will bring on that land all my words which I have pronounced against it, even all that is written in this book, which Jeremiah has prophesied against all the nations.

Kwa maana mataifa mengi na wafalme wakuu watawatumikisha; naam, hao pia; nami nitawalipa kwa kadiri ya matendo yao, na kwa kadiri ya kazi ya mikono yao. Yeremia 25:14

For many nations and great kings shall make bondservants of them, even of them; and I will recompense them according to their deeds, and according to the work of their hands.

Maana Bwana, Mungu wa Israeli, aniambia hivi, Pokea kikombe cha divai ya ghadhabu hii mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote, ambao nitakupeleka kwao; Yeremia 25:15

For thus says Yahweh, the God of Israel, to me: take this cup of the wine of wrath at my hand, and cause all the nations, to whom I send you, to drink it.

nao watakunywa, na kulewalewa, na kufanya wazimu, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yao. Yeremia 25:16

They shall drink, and reel back and forth, and be mad, because of the sword that I will send among them.

Ndipo nikakipokea kikombe kile mkononi mwa Bwana, nikawanywesha mataifa yote, ambao Bwana alinipeleka kwao; Yeremia 25:17

Then took I the cup at Yahweh's hand, and made all the nations to drink, to whom Yahweh had sent me:

yaani, Yerusalemu, na miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, ili kuwafanya kuwa ukiwa, na ajabu, na mazomeo, na laana; vile vile kama ilivyo leo; Yeremia 25:18

[to wit], Jerusalem, and the cities of Judah, and the kings of it, and the princes of it, to make them a desolation, an astonishment, a hissing, and a curse, as it is this day;

Farao, mfalme wa Misri, na watumishi wake na wakuu wake na watu wake wote; Yeremia 25:19

Pharaoh king of Egypt, and his servants, and his princes, and all his people;

na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi; Yeremia 25:20

and all the mixed people, and all the kings of the land of the Uz, and all the kings of the Philistines, and Ashkelon, and Gaza, and Ekron, and the remnant of Ashdod;

Edomu, na Moabu, na wana wa Amoni; Yeremia 25:21

Edom, and Moab, and the children of Ammon;

na wafalme wote wa Tiro, na wafalme wote wa Sidoni, na wafalme wote wa kisiwa kilicho ng'ambo ya pili ya bahari; Yeremia 25:22

and all the kings of Tyre, and all the kings of Sidon, and the kings of the isle which is beyond the sea;

Dedani, na Tema, na Buzi, na watu wote wakatao denge; Yeremia 25:23

Dedan, and Tema, and Buz, and all who have the corners [of their hair] cut off;

na wafalme wote wa Arabuni, na wafalme wote wa watu waliochanganyika wakaao jangwani; Yeremia 25:24

and all the kings of Arabia, and all the kings of the mixed people who dwell in the wilderness;

na wafalme wote wa Zimri, na wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi; Yeremia 25:25

and all the kings of Zimri, and all the kings of Elam, and all the kings of the Medes;

na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na mfalme wa Sheshaki atakunywa baada yao. Yeremia 25:26

and all the kings of the north, far and near, one with another; and all the kingdoms of the world, which are on the surface of the earth: and the king of Sheshach shall drink after them.

Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu. Yeremia 25:27

You shall tell them, Thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel: Drink you, and be drunken, and spew, and fall, and rise no more, because of the sword which I will send among you.

Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa. Yeremia 25:28

It shall be, if they refuse to take the cup at your hand to drink, then shall you tell them, Thus says Yahweh of Hosts: You shall surely drink.

Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema Bwana wa majeshi. Yeremia 25:29

For, behold, I begin to work evil at the city which is called by my name; and should you be utterly unpunished? You shall not be unpunished; for I will call for a sword on all the inhabitants of the earth, says Yahweh of Hosts.

Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia, Bwana atanguruma toka juu, Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake; Atanguruma sana juu ya zizi lake; Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu, Juu ya wenyeji wote wa dunia. Yeremia 25:30

Therefore prophesy you against them all these words, and tell them, Yahweh will roar from on high, and utter his voice from his holy habitation; he will mightily roar against his fold; he will give a shout, as those who tread [the grapes], against all the inhabitants of the earth.

Mshindo utafika hata mwisho wa dunia; Maana Bwana ana mashindano na mataifa, Atateta na watu wote wenye mwili; Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema Bwana. Yeremia 25:31

A noise shall come even to the end of the earth; for Yahweh has a controversy with the nations; he will enter into judgment with all flesh: as for the wicked, he will give them to the sword, says Yahweh.

Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. Yeremia 25:32

Thus says Yahweh of hosts, Behold, evil shall go forth from nation to nation, and a great tempest shall be raised up from the uttermost parts of the earth.

Na waliouawa na Bwana siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi. Yeremia 25:33

The slain of Yahweh shall be at that day from one end of the earth even to the other end of the earth: they shall not be lamented, neither gathered, nor buried; they shall be dung on the surface of the ground.

Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa. Yeremia 25:34

Wail, you shepherds, and cry; and wallow [in ashes], you principal of the flock; for the days of your slaughter and of your dispersions are fully come, and you shall fall like a goodly vessel.

Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka. Yeremia 25:35

The shepherds shall have no way to flee, nor the principal of the flock to escape.

Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika kundi, kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao. Yeremia 25:36

A voice of the cry of the shepherds, and the wailing of the principal of the flock! for Yahweh lays waste their pasture.

Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya Bwana. Yeremia 25:37

The peaceable folds are brought to silence because of the fierce anger of Yahweh.

Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali. Yeremia 25:38

He has left his covert, as the lion; for their land is become an astonishment because of the fierceness of the oppressing [sword], and because of his fierce anger.