Yeremia 44 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 44 (Swahili) Jeremiah 44 (English)

Neno lililomjia Yeremia, katika habari za Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tahpanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema, Yeremia 44:1

The word that came to Jeremiah concerning all the Jews who lived in the land of Egypt, who lived at Migdol, and at Tahpanhes, and at Memphis, and in the country of Pathros, saying,

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ninyi mmeona mabaya yote niliyoleta juu ya Yerusalemu, na juu ya miji yote ya Yuda; na, tazama, ni ukiwa leo, wala hapana mtu akaaye ndani yake; Yeremia 44:2

Thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel: You have seen all the evil that I have brought on Jerusalem, and on all the cities of Judah; and, behold, this day they are a desolation, and no man dwells therein,

kwa sababu ya uovu wao, waliotenda ili kunikasirisha, kwa kuwa walikwenda kufukiza uvumba, na kuwatumikia miungu mingine, ambao hawakuwajua, wao, wala ninyi, wala baba zenu. Yeremia 44:3

because of their wickedness which they have committed to provoke me to anger, in that they went to burn incense, [and] to serve other gods, that they didn't know, neither they, nor you, nor your fathers.

Tena nalituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linichukizalo. Yeremia 44:4

However I sent to you all my servants the prophets, rising up early and sending them, saying, Oh, don't do this abominable thing that I hate.

Lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, ili wageuke na kuacha uovu wao, wasifukizie uvumba miungu mingine. Yeremia 44:5

But they didn't listen, nor inclined their ear to turn from their wickedness, to burn no incense to other gods.

Kwa sababu hiyo ghadhabu yangu, na hasira yangu, zilimwagika, nazo ziliwaka katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, na miji hiyo imeachwa ukiwa, na kuharibika, kama ilivyo leo. Yeremia 44:6

Therefore my wrath and my anger was poured forth, and was kindled in the cities of Judah and in the streets of Jerusalem; and they are wasted and desolate, as it is this day.

Basi, sasa, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye; Yeremia 44:7

Therefore now thus says Yahweh, the God of hosts, the God of Israel: Why commit you [this] great evil against your own souls, to cut off from you man and woman, infant and suckling, out of the midst of Judah, to leave you none remaining;

kwa kuwa mnanikasirisha kwa matendo ya mikono yenu, mkifukizia uvumba miungu mingine katika nchi ya Misri, mlikokwenda kukaa ugenini; mpate kukatiliwa mbali, na kuwa laana, na aibu, katika mataifa yote ya dunia? Yeremia 44:8

in that you provoke me to anger with the works of your hands, burning incense to other gods in the land of Egypt, where you are gone to sojourn; that you may be cut off, and that you may be a curse and a reproach among all the nations of the earth?

Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na uovu wa wake zao, na uovu wenu wenyewe, na uovu wa wake zenu, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu? Yeremia 44:9

Have you forgotten the wickedness of your fathers, and the wickedness of the kings of Judah, and the wickedness of their wives, and your own wickedness, and the wickedness of your wives which they committed in the land of Judah, and in the streets of Jerusalem?

Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, nilizoweka mbele yenu, na mbele ya baba zenu. Yeremia 44:10

They are not humbled even to this day, neither have they feared, nor walked in my law, nor in my statutes, that I set before you and before your fathers.

Basi, kwa sababu hiyo Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaelekeza uso wangu juu yenu, ili niwaletee mabaya, hata kukatilia mbali Yuda yote. Yeremia 44:11

Therefore thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel: Behold, I will set my face against you for evil, even to cut off all Judah.

Nami nitawatwaa mabaki ya Yuda, walioelekeza nyuso zao kuiingia nchi ya Misri, wakae huko, nao wataangamia wote pia; wataanguka katika nchi ya Misri; wataangamia kwa upanga, na kwa njaa; watakufa, tangu wadogo hata wakubwa, kwa upanga, na kwa njaa; nao watakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu. Yeremia 44:12

I will take the remnant of Judah, that have set their faces to go into the land of Egypt to sojourn there, and they shall all be consumed; in the land of Egypt shall they fall; they shall be consumed by the sword and by the famine; they shall die, from the least even to the greatest, by the sword and by the famine; and they shall be an object of horror, [and] an astonishment, and a curse, and a reproach.

Kwa maana nitawaadhibu wakaao katika nchi ya Misri, kama nilivyouadhibu Yerusalemu, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; Yeremia 44:13

For I will punish those who dwell in the land of Egypt, as I have punished Jerusalem, by the sword, by the famine, and by the pestilence;

hata katika watu wale wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili wakae huko, hapatakuwa na mtu ye yote atakayepona, wala atakayesalia, na kupata kurudi nchi ya Yuda, ambayo wanatamani kurudi ili kukaa huko; maana hapana atakayerudi, ila wao watakaopona. Yeremia 44:14

so that none of the remnant of Judah, who have gone into the land of Egypt to sojourn there, shall escape or be left, to return into the land of Judah, to which they have a desire to return to dwell there: for none shall return save such as shall escape.

Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema, Yeremia 44:15

Then all the men who knew that their wives burned incense to other gods, and all the women who stood by, a great assembly, even all the people who lived in the land of Egypt, in Pathros, answered Jeremiah, saying,

Neno lile ulilotuambia kwa jina la Bwana, sisi hatutakusikiliza. Yeremia 44:16

As for the word that you have spoken to us in the name of Yahweh, we will not listen to you.

Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. Yeremia 44:17

But we will certainly perform every word that is gone forth out of our mouth, to burn incense to the queen of the sky, and to pour out drink-offerings to her, as we have done, we and our fathers, our kings and our princes, in the cities of Judah, and in the streets of Jerusalem; for then had we plenty of food, and were well, and saw no evil.

Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. Yeremia 44:18

But since we left off burning incense to the queen of the sky, and pouring out drink-offerings to her, we have wanted all things, and have been consumed by the sword and by the famine.

Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo? Yeremia 44:19

When we burned incense to the queen of the sky, and poured out drink-offerings to her, did we make her cakes to worship her, and pour out drink-offerings to her, without our husbands?

Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema, Yeremia 44:20

Then Jeremiah said to all the people, to the men, and to the women, even to all the people who had given him who answer, saying,

Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake? Yeremia 44:21

The incense that you burned in the cities of Judah, and in the streets of Jerusalem, you and your fathers, your kings and your princes, and the people of the land, didn't Yahweh remember them, and didn't it come into his mind?

Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo. Yeremia 44:22

so that Yahweh could no longer bear, because of the evil of your doings, and because of the abominations which you have committed; therefore is your land become a desolation, and an astonishment, and a curse, without inhabitant, as it is this day.

Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. Yeremia 44:23

Because you have burned incense, and because you have sinned against Yahweh, and have not obeyed the voice of Yahweh, nor walked in his law, nor in his statutes, nor in his testimonies; therefore this evil is happened to you, as it is this day.

Tena Yeremia akawaambia watu wote, na wanawake wote, Lisikieni neno hili la Bwana, ninyi nyote wa Yuda, mliopo hapa katika nchi ya Misri; Yeremia 44:24

Moreover Jeremiah said to all the people, and to all the women, Hear the word of Yahweh, all Judah who are in the land of Egypt:

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ninyi na wake zenu mmenena kwa vinywa vyenu, na kutimiza kwa mikono yenu, mkisema, Bila shaka tutazitimiza nadhiri zetu tulizoziweka, na kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji; basi, zithibitisheni nadhiri zenu, zitimizeni nadhiri zenu. Yeremia 44:25

Thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel, saying, You and your wives have both spoken with your mouths, and with your hands have fulfilled it, saying, We will surely perform our vows that we have vowed, to burn incense to the queen of the sky, and to pour out drink-offerings to her: establish then your vows, and perform your vows.

Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la Bwana, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema Bwana, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo! Yeremia 44:26

Therefore hear the word of Yahweh, all Judah who dwell in the land of Egypt: Behold, I have sworn by my great name, says Yahweh, that my name shall no more be named in the mouth of any man of Judah in all the land of Egypt, saying, As the Lord Yahweh lives.

Tazama, nawaangalia niwaletee mabaya, wala si mema; nao watu wote wa Yuda, waliopo hapa katika nchi ya Misri, wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa, hata wakomeshwe kabisa. Yeremia 44:27

Behold, I watch over them for evil, and not for good; and all the men of Judah who are in the land of Egypt shall be consumed by the sword and by the famine, until there be an end of them.

Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao. Yeremia 44:28

Those who escape the sword shall return out of the land of Egypt into the land of Judah, few in number; and all the remnant of Judah, who have gone into the land of Egypt to sojourn there, shall know whose word shall stand, mine, or theirs.

Na hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu, asema Bwana, kwamba mimi nitawaadhibu ninyi mahali hapa, mpate kujua ya kuwa maneno yangu yatasimama juu yenu, kuwaletea mabaya bila shaka; Yeremia 44:29

This shall be the sign to you, says Yahweh, that I will punish you in this place, that you may know that my words shall surely stand against you for evil:

Bwana asema hivi, Tazama, nitamtia Farao Hofra, mfalme wa Misri, katika mikono ya adui zake, na katika mikono yao wamtafutao roho yake; kama vile nilivyomtia Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, adui yake aliyemtafuta roho yake. Yeremia 44:30

Thus says Yahweh, Behold, I will give Pharaoh Hophra king of Egypt into the hand of his enemies, and into the hand of those who seek his life; as I gave Zedekiah king of Judah into the hand of Nebuchadrezzar king of Babylon, who was his enemy, and sought his life.