Yeremia 50 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 50 (Swahili) Jeremiah 50 (English)

Neno hili ndilo alilosema Bwana, katika habari za Babeli, na katika habari za Wakaldayo, kwa kinywa cha Yeremia, nabii. Yeremia 50:1

The word that Yahweh spoke concerning Babylon, concerning the land of the Chaldeans, by Jeremiah the prophet.

Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika. Yeremia 50:2

Declare you among the nations and publish, and set up a standard; publish, and don't conceal: say, Babylon is taken, Bel is disappointed, Merodach is dismayed; her images are disappointed, her idols are dismayed.

Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hapana mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia. Yeremia 50:3

For out of the north there comes up a nation against her, which shall make her land desolate, and none shall dwell therein: they are fled, they are gone, both man and animal.

Katika siku hizo, na wakati huo, asema Bwana, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta Bwana, Mungu wao. Yeremia 50:4

In those days, and in that time, says Yahweh, the children of Israel shall come, they and the children of Judah together; they shall go on their way weeping, and shall seek Yahweh their God.

Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na Bwana, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa. Yeremia 50:5

They shall inquire concerning Zion with their faces turned toward it, [saying], Come you, and join yourselves to Yahweh in an everlasting covenant that shall not be forgotten.

Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika. Yeremia 50:6

My people have been lost sheep: their shepherds have caused them to go astray; they have turned them away on the mountains; they have gone from mountain to hill; they have forgotten their resting-place.

Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya Bwana, aliye kao la haki, yaani, Bwana, tumaini la baba zao. Yeremia 50:7

All who found them have devoured them; and their adversaries said, We are not guilty, because they have sinned against Yahweh, the habitation of righteousness, even Yahweh, the hope of their fathers.

Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi. Yeremia 50:8

Flee out of the midst of Babylon, and go forth out of the land of the Chaldeans, and be as the male goats before the flocks.

Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hapana hata mmoja utakaorudi bure. Yeremia 50:9

For, behold, I will stir up and cause to come up against Babylon a company of great nations from the north country; and they shall set themselves in array against her; from there she shall be taken: their arrows shall be as of an expert mighty man; none shall return in vain.

Nao Ukaldayo utakuwa mateka; wote wautekao watashiba, asema Bwana. Yeremia 50:10

Chaldea shall be a prey: all who prey on her shall be satisfied, says Yahweh.

Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmewanda kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu; Yeremia 50:11

Because you are glad, because you rejoice, O you who plunder my heritage, because you are wanton as a heifer that treads out [the grain], and neigh as strong horses;

mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika. Yeremia 50:12

your mother shall be utterly disappointed; she who bore you shall be confounded: behold, she shall be the least of the nations, a wilderness, a dry land, and a desert.

Kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote. Yeremia 50:13

Because of the wrath of Yahweh she shall not be inhabited, but she shall be wholly desolate: everyone who goes by Babylon shall be astonished, and hiss at all her plagues.

Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda Bwana dhambi. Yeremia 50:14

Set yourselves in array against Babylon round about, all you who bend the bow; shoot at her, spare no arrows: for she has sinned against Yahweh.

Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha Bwana; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye. Yeremia 50:15

Shout against her round about: she has submitted herself; her bulwarks are fallen, her walls are thrown down; for it is the vengeance of Yahweh: take vengeance on her; as she has done, do to her.

Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake. Yeremia 50:16

Cut off the sower from Babylon, and him who handles the sickle in the time of harvest: for fear of the oppressing sword they shall turn everyone to his people, and they shall flee everyone to his own land.

Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadreza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake. Yeremia 50:17

Israel is a hunted sheep; the lions have driven him away: first, the king of Assyria devoured him; and now at last Nebuchadrezzar king of Babylon has broken his bones.

Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, mimi nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru. Yeremia 50:18

Therefore thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel: Behold, I will punish the king of Babylon and his land, as I have punished the king of Assyria.

Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi. Yeremia 50:19

I will bring Israel again to his pasture, and he shall feed on Carmel and Bashan, and his soul shall be satisfied on the hills of Ephraim and in Gilead.

Katika siku hizo na wakati huo, asema Bwana, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki. Yeremia 50:20

In those days, and in that time, says Yahweh, the iniquity of Israel shall be sought for, and there shall be none; and the sins of Judah, and they shall not be found: for I will pardon them whom I leave as a remnant.

Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema Bwana, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia. Yeremia 50:21

Go up against the land of Merathaim, even against it, and against the inhabitants of Pekod: kill and utterly destroy after them, says Yahweh, and do according to all that I have commanded you.

Pana mshindo wa vita katika nchi, Mshindo wa uharibifu mkuu. Yeremia 50:22

A sound of battle is in the land, and of great destruction.

Imekuwaje nyundo ya dunia yote Kukatiliwa mbali na kuvunjwa? Imekuwaje Babeli kuwa ukiwa Katikati ya mataifa? Yeremia 50:23

How is the hammer of the whole earth cut apart and broken! how is Babylon become a desolation among the nations!

Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na Bwana. Yeremia 50:24

I have laid a snare for you, and you are also taken, Babylon, and you weren't aware: you are found, and also caught, because you have striven against Yahweh.

Bwana amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, Bwana wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo. Yeremia 50:25

Yahweh has opened his armory, and has brought forth the weapons of his indignation; for the Lord, Yahweh of Hosts, has a work [to do] in the land of the Chaldeans.

Njoni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu cho chote. Yeremia 50:26

Come against her from the utmost border; open her store-houses; cast her up as heaps, and destroy her utterly; let nothing of her be left.

Wachinjeni mafahali wake wote; Na watelemkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao. Yeremia 50:27

Kill all her bulls; let them go down to the slaughter: woe to them! for their day is come, the time of their visitation.

Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza Sayuni kisasi cha Bwana, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake. Yeremia 50:28

The voice of those who flee and escape out of the land of Babylon, to declare in Zion the vengeance of Yahweh our God, the vengeance of his temple.

Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya Bwana, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli. Yeremia 50:29

Call together the archers against Babylon, all those who bend the bow; encamp against her round about; let none of it escape: recompense her according to her work; according to all that she has done, do to her; for she has been proud against Yahweh, against the Holy One of Israel.

Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana. Yeremia 50:30

Therefore shall her young men fall in her streets, and all her men of war shall be brought to silence in that day, says Yahweh.

Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, Bwana wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujilia. Yeremia 50:31

Behold, I am against you, you proud one, says the Lord, Yahweh of Hosts; for your day is come, the time that I will visit you.

Na mwenye kiburi atajikwaa, na kuanguka, wala hapana atakayemwinua; nami nitawasha moto katika miji yake, nao utawala wote wamzungukao pande zote. Yeremia 50:32

The proud one shall stumble and fall, and none shall raise him up; and I will kindle a fire in his cities, and it shall devour all who are round about him.

Bwana wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda, wameonewa pamoja; na wote waliowachukua mateka wanawashika sana; wanakataa kuwaacha. Yeremia 50:33

Thus says Yahweh of hosts: The children of Israel and the children of Judah are oppressed together; and all who took them captive hold them fast; they refuse to let them go.

Mkombozi wao ni hodari; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli. Yeremia 50:34

Their Redeemer is strong; Yahweh of Hosts is his name: he will thoroughly plead their cause, that he may give rest to the earth, and disquiet the inhabitants of Babylon.

Upanga u juu ya Wakaldayo, asema Bwana, na juu yao wakaao Babeli, na juu ya wakuu wake, na juu ya watu wake wenye hekima. Yeremia 50:35

A sword is on the Chaldeans, says Yahweh, and on the inhabitants of Babylon, and on her princes, and on her wise men.

Upanga u juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga u juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika. Yeremia 50:36

A sword is on the boasters, and they shall become fools; a sword is on her mighty men, and they shall be dismayed.

Upanga u juu ya farasi zao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa. Yeremia 50:37

A sword is on their horses, and on their chariots, and on all the mixed people who are in the midst of her; and they shall become as women: a sword is on her treasures, and they shall be robbed.

Ukosefu wa mvua u juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu. Yeremia 50:38

A drought is on her waters, and they shall be dried up; for it is a land of engraved images, and they are mad over idols.

Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwa-mwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hapana mtu atakayekaa huko tangu kizazi hata kizazi. Yeremia 50:39

Therefore the wild animals of the desert with the wolves shall dwell there, and the ostriches shall dwell therein: and it shall be no more inhabited forever; neither shall it be lived in from generation to generation.

Kama vile vilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema Bwana; kadhalika hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo. Yeremia 50:40

As when God overthrew Sodom and Gomorrah and the neighbor cities of it, says Yahweh, so shall no man dwell there, neither shall any son of man sojourn therein.

Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia. Yeremia 50:41

Behold, a people comes from the north; and a great nation and many kings shall be stirred up from the uttermost parts of the earth.

Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli. Yeremia 50:42

They lay hold on bow and spear; they are cruel, and have no mercy; their voice roars like the sea; and they ride on horses, everyone set in array, as a man to the battle, against you, daughter of Babylon.

Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke katika utungu wake. Yeremia 50:43

The king of Babylon has heard the news of them, and his hands wax feeble: anguish has taken hold of him, [and] pangs as of a woman in travail.

Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu? Yeremia 50:44

Behold, [the enemy] shall come up like a lion from the pride of the Jordan against the strong habitation: for I will suddenly make them run away from it; and whoever is chosen, him will I appoint over it: for who is like me? and who will appoint me a time? and who is the shepherd who can stand before me?

Basi, lisikieni shauri la Bwana, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao. Yeremia 50:45

Therefore hear the counsel of Yahweh, that he has taken against Babylon; and his purposes, that he has purposed against the land of the Chaldeans: Surely they shall drag them away, [even] the little ones of the flock; surely he shall make their habitation desolate over them.

Kwa mshindo wa kutwaliwa Babeli nchi yatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa. Yeremia 50:46

At the noise of the taking of Babylon the earth trembles, and the cry is heard among the nations.