Yeremia 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 12 (Swahili) Jeremiah 12 (English)

Wewe u mwenye haki, Ee Bwana, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama? Yeremia 12:1

Righteous are you, Yahweh, when I contend with you; yet would I reason the cause with you: why does the way of the wicked prosper? why are all they at ease who deal very treacherously?

Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali. Yeremia 12:2

You have planted them, yes, they have taken root; they grow, yes, they bring forth fruit: you are near in their mouth, and far from their heart.

Lakini wewe, Bwana, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa. Yeremia 12:3

But you, Yahweh, know me; you see me, and try my heart toward you: pull them out like sheep for the slaughter, and prepare them for the day of slaughter.

Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Hatauona mwisho wetu. Yeremia 12:4

How long shall the land mourn, and the herbs of the whole country wither? for the wickedness of those who dwell therein, the animals are consumed, and the birds; because they said, He shall not see our latter end.

Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani u salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani? Yeremia 12:5

If you have run with the footmen, and they have wearied you, then how can you contend with horses? and though in a land of peace you are secure, yet how will you do in the pride of the Jordan?

Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri. Yeremia 12:6

For even your brothers, and the house of your father, even they have dealt treacherously with you; even they have cried aloud after you: don't believe them, though they speak beautiful words to you.

Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake. Yeremia 12:7

I have forsaken my house, I have cast off my heritage; I have given the dearly beloved of my soul into the hand of her enemies.

Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia. Yeremia 12:8

My heritage is become to me as a lion in the forest: she has uttered her voice against me; therefore I have hated her.

Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wanamtulia pande zote? Enendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale. Yeremia 12:9

Is my heritage to me as a speckled bird of prey? are the birds of prey against her round about? go you, assemble all the animals of the field, bring them to devour.

Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa. Yeremia 12:10

Many shepherds have destroyed my vineyard, they have trodden my portion under foot, they have made my pleasant portion a desolate wilderness.

Wamelifanya kuwa ukiwa, na kwa kuwa ni ukiwa linanililia; nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa sababu hapana mtu aliyeweka haya moyoni mwake. Yeremia 12:11

They have made it a desolation; it mourns to me, being desolate; the whole land is made desolate, because no man lays it to heart.

Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa Bwana utakula toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani. Yeremia 12:12

Destroyers are come on all the bare heights in the wilderness; for the sword of Yahweh devours from the one end of the land even to the other end of the land: no flesh has peace.

Wamepanda ngano, lakini watavuna miiba; wamejiumiza nafsi zao, lakini hawatakuwa na faida; naam, tahayarini kwa ajili ya matunda yenu, kwa sababu ya hasira kali ya Bwana. Yeremia 12:13

They have sown wheat, and have reaped thorns; they have put themselves to pain, and profit nothing: and you shall be ashamed of your fruits, because of the fierce anger of Yahweh.

Bwana asema hivi juu ya jirani zangu wote walio wabaya, waugusao urithi wangu niliowarithisha watu wangu Israeli, Tazama, nitawang'oa katika nchi yao, nami nitaing'oa nyumba ya Yuda isiwe kati yao. Yeremia 12:14

Thus says Yahweh against all my evil neighbors, who touch the inheritance which I have caused my people Israel to inherit: behold, I will pluck them up from off their land, and will pluck up the house of Judah from among them.

Tena itakuwa, baada ya kuwang'oa, nitarudi na kuwahurumia; nami nitawaleta tena, kila mtu aingie katika urithi wake, na kila mtu aingie katika nchi yake. Yeremia 12:15

It shall happen, after that I have plucked them up, I will return and have compassion on them; and I will bring them again, every man to his heritage, and every man to his land.

Kisha itakuwa, ikiwa watajifunza kwa bidii njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu, Kama Bwana aishivyo, vile vile kama walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapojengwa kati ya watu wangu. Yeremia 12:16

It shall happen, if they will diligently learn the ways of my people, to swear by my name, As Yahweh lives; even as they taught my people to swear by Baal; then shall they be built up in the midst of my people.

Bali, kama hawataki kusikia, kung'oa nitaling'oa taifa lile, na kuliangamiza kabisa, asema Bwana. Yeremia 12:17

But if they will not hear, then will I pluck up that nation, plucking up and destroying it, says Yahweh.