Yeremia 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 5 (Swahili) Jeremiah 5 (English)

Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. Yeremia 5:1

Run you back and forth through the streets of Jerusalem, and see now, and know, and seek in the broad places of it, if you can find a man, if there are any who does justly, who seeks truth; and I will pardon her.

Na wajaposema, Kama Bwana aishivyo, hakika waapa kwa uongo. Yeremia 5:2

Though they say, As Yahweh lives; surely they swear falsely.

Ee Bwana, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi. Yeremia 5:3

O Yahweh, don't your eyes look on truth? you have stricken them, but they were not grieved; you have consumed them, but they have refused to receive correction: they have made their faces harder than a rock; they have refused to return.

Ndipo nikasema, Hakika, hawa ni maskini; ni wajinga hawa; maana hawaijui njia ya Bwana, wala hukumu ya Mungu wao; Yeremia 5:4

Then I said, Surely these are poor; they are foolish; for they don't know the way of Yahweh, nor the law of their God:

nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya Bwana, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo. Yeremia 5:5

I will get me to the great men, and will speak to them; for they know the way of Yahweh, and the law of their God. But these with one accord have broken the yoke, and burst the bonds.

Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwa-mwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi. Yeremia 5:6

Therefore a lion out of the forest shall kill them, a wolf of the evenings shall destroy them, a leopard shall watch against their cities; everyone who goes out there shall be torn in pieces; because their transgressions are many, [and] their backsliding is increased.

Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. Yeremia 5:7

How can I pardon you? your children have forsaken me, and sworn by them that are no gods: when I had fed them to the full, they committed adultery, and assembled themselves in troops at the prostitutes' houses.

Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. Yeremia 5:8

They were as fed horses roaming at large; everyone neighed after his neighbor's wife.

Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii? Yeremia 5:9

Shall I not visit for these things? says Yahweh; and shall not my soul be avenged on such a nation as this?

Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake Bwana. Yeremia 5:10

Go up on her walls, and destroy; but don't make a full end: take away her branches; for they are not Yahweh's.

Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema Bwana. Yeremia 5:11

For the house of Israel and the house of Judah have dealt very treacherously against me, says Yahweh.

Wamemkataa Bwana, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa; Yeremia 5:12

They have denied Yahweh, and said, It is not he; neither shall evil come on us; neither shall we see sword nor famine:

na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa. Yeremia 5:13

and the prophets shall become wind, and the word is not in them: thus shall it be done to them.

Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala. Yeremia 5:14

Therefore thus says Yahweh, the God of hosts, Because you speak this word, behold, I will make my words in your mouth fire, and this people wood, and it shall devour them.

Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema Bwana; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo. Yeremia 5:15

Behold, I will bring a nation on you from far, house of Israel, says Yahweh: it is a mighty nation, it is an ancient nation, a nation whose language you don't know, neither understand what they say.

Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia. Yeremia 5:16

Their quiver is an open tomb, they are all mighty men.

Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga. Yeremia 5:17

They shall eat up your harvest, and your bread, [which] your sons and your daughters should eat; they shall eat up your flocks and your herds; they shall eat up your vines and your fig trees; they shall beat down your fortified cities, in which you trust, with the sword.

Lakini hata katika siku zile, asema Bwana, sitawakomesha ninyi kabisa. Yeremia 5:18

But even in those days, says Yahweh, I will not make a full end with you.

Tena itakuwa mtakapouliza, Bwana ametutenda mambo hayo yote kwa sababu gani? Ndipo utakapowaambia, Vile vile kama ninyi mlivyoniacha mimi, na kuwatumikia miungu mingine katika nchi yenu wenyewe, ndivyo mtakavyowatumikia wageni katika nchi isiyo yenu. Yeremia 5:19

It shall happen, when you shall say, Why has Yahweh our God done all these things to us? then shall you say to them, Like as you have forsaken me, and served foreign gods in your land, so shall you serve strangers in a land that is not yours.

Tangazeni neno hili katika nyumba ya Yakobo, litangazeni katika Yuda, kusema, Yeremia 5:20

Declare you this in the house of Jacob, and publish it in Judah, saying,

Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamwoni; mlio na masikio ila hamsikii. Yeremia 5:21

Hear now this, foolish people, and without understanding; who have eyes, and don't see; who have ears, and don't hear:

Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita. Yeremia 5:22

Don't you fear me? says Yahweh: won't you tremble at my presence, who have placed the sand for the bound of the sea, by a perpetual decree, that it can't pass it? and though the waves of it toss themselves, yet they can't prevail; though they roar, yet they can't pass over it.

Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao. Yeremia 5:23

But this people has a revolting and a rebellious heart; they are revolted and gone.

Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa. Yeremia 5:24

Neither say they in their heart, Let us now fear Yahweh our God, who gives rain, both the former and the latter, in its season; who preserves to us the appointed weeks of the harvest.

Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate. Yeremia 5:25

Your iniquities have turned away these things, and your sins have withheld good from you.

Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. Yeremia 5:26

For among my people are found wicked men: they watch, as fowlers lie in wait; they set a trap, they catch men.

Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Yeremia 5:27

As a cage is full of birds, so are their houses full of deceit: therefore they are become great, and grew rich.

Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. Yeremia 5:28

They are grew fat, they shine: yes, they overpass in deeds of wickedness; they don't plead the cause, the cause of the fatherless, that they may prosper; and the right of the needy they don't judge.

Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii? Yeremia 5:29

Shall I not visit for these things? says Yahweh; shall not my soul be avenged on such a nation as this?

Jambo la ajabu, la kuchukiza, limetokea katika nchi hii! Yeremia 5:30

A wonderful and horrible thing is happen in the land:

Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake? Yeremia 5:31

the prophets prophesy falsely, and the priests bear rule by their means; and my people love to have it so: and what will you do in the end of it?