Yeremia 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 3 (Swahili) Jeremiah 3 (English)

Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema Bwana. Yeremia 3:1

They say, If a man put away his wife, and she go from him, and become another man's, will he return to her again? Won't that land be greatly polluted? But you have played the prostitute with many lovers; yet return again to me, says Yahweh.

Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako. Yeremia 3:2

Lift up your eyes to the bare heights, and see; where have you not been lain with? By the ways have you sat for them, as an Arabian in the wilderness; and you have polluted the land with your prostitution and with your wickedness.

Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika. Yeremia 3:3

Therefore the showers have been withheld, and there has been no latter rain; yet you have a prostitute's forehead, you refused to be ashamed.

Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, wewe u kiongozi wa ujana wangu? Yeremia 3:4

Will you not from this time cry to me, My Father, you are the guide of my youth?

Je! Ataishika hasira yake hata milele? Ataishika hata mwisho? Tazama, umesema hivyo, bali umetenda mambo mabaya, umefuata njia yako mwenyewe. Yeremia 3:5

Will he retain [his anger] forever? will he keep it to the end? Behold, you have spoken and have done evil things, and have had your way.

Tena, Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi. Yeremia 3:6

Moreover Yahweh said to me in the days of Josiah the king, Have you seen that which backsliding Israel has done? she is gone up on every high mountain and under every green tree, and there has played the prostitute.

Nami nalisema baada ya yeye kuyatenda hayo yote, Atanirudia mimi, lakini hakurudi; na dada yake, Yuda mwenye hiana, akayaona hayo. Yeremia 3:7

I said after she had done all these things, She will return to me; but she didn't return: and her treacherous sister Judah saw it.

Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya mambo ya ukahaba. Yeremia 3:8

I saw, when, for this very cause that backsliding Israel had committed adultery, I had put her away and given her a bill of divorce, yet treacherous Judah, her sister, didn't fear; but she also went and played the prostitute.

Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti. Yeremia 3:9

It happened through the lightness of her prostitution, that the land was polluted, and she committed adultery with stones and with stocks.

Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema Bwana. Yeremia 3:10

Yet for all this her treacherous sister Judah has not returned to me with her whole heart, but only in pretense, says Yahweh.

Bwana, akaniambia, Israeli mwenye kuasi amejionyesha kuwa mwenye haki kuliko Yuda mwenye hiana. Yeremia 3:11

Yahweh said to me, Backsliding Israel has shown herself more righteous than treacherous Judah.

Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele. Yeremia 3:12

Go, and proclaim these words toward the north, and say, Return, you backsliding Israel, says Yahweh; I will not look in anger on you; for I am merciful, says Yahweh, I will not keep [anger] forever.

Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema Bwana. Yeremia 3:13

Only acknowledge your iniquity, that you have transgressed against Yahweh your God, and have scattered your ways to the strangers under every green tree, and you have not obeyed my voice, says Yahweh.

Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni; Yeremia 3:14

Return, backsliding children, says Yahweh; for I am a husband to you: and I will take you one of a city, and two of a family, and I will bring you to Zion:

nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu. Yeremia 3:15

and I will give you shepherds according to my heart, who shall feed you with knowledge and understanding.

Kisha itakuwa, mtakapoongezeka na kuwa wengi katika nchi hiyo, asema Bwana, siku zile hawatasema tena, Sanduku la agano la Bwana; wala halitaingia moyoni; wala hawatalikumbuka, wala hawatalizuru, wala hayatafanyika hayo tena. Yeremia 3:16

It shall come to pass, when you are multiplied and increased in the land, in those days, says Yahweh, they shall say no more, The ark of the covenant of Yahweh; neither shall it come to mind; neither shall they remember it; neither shall they miss it; neither shall it be made any more.

Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha Bwana; na mataifa yote watakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la Bwana; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya. Yeremia 3:17

At that time they shall call Jerusalem the throne of Yahweh; and all the nations shall be gathered to it, to the name of Yahweh, to Jerusalem: neither shall they walk any more after the stubbornness of their evil heart.

Siku zile nyumba ya Yuda watakwenda pamoja na nyumba ya Israeli, nao watakuja pamoja, kutoka nchi ya kaskazini, mpaka nchi ile niliyowapa baba zenu iwe urithi wao. Yeremia 3:18

In those days the house of Judah shall walk with the house of Israel, and they shall come together out of the land of the north to the land that I gave for an inheritance to your fathers.

Lakini mimi nalisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata. Yeremia 3:19

But I said, How I will put you among the children, and give you a pleasant land, a goodly heritage of the hosts of the nations! and I said, You shall call me My Father, and shall not turn away from following me.

Hakika kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiana, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiana, Ee nyumba ya Israeli, asema Bwana. Yeremia 3:20

Surely as a wife treacherously departs from her husband, so have you dealt treacherously with me, house of Israel, says Yahweh.

Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau Bwana, Mungu wao. Yeremia 3:21

A voice is heard on the bare heights, the weeping [and] the petitions of the children of Israel; because they have perverted their way, they have forgotten Yahweh their God.

Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu. Yeremia 3:22

Return, you backsliding children, I will heal your backsliding. Behold, we are come to you; for you are Yahweh our God.

Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika Bwana, Mungu wetu. Yeremia 3:23

Truly in vain is [the help that is looked for] from the hills, the tumult on the mountains: truly in Yahweh our God is the salvation of Israel.

Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao. Yeremia 3:24

But the shameful thing has devoured the labor of our fathers from our youth, their flocks and their herds, their sons and their daughters.

Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu. Yeremia 3:25

Let us lie down in our shame, and let our confusion cover us; for we have sinned against Yahweh our God, we and our fathers, from our youth even to this day; and we have not obeyed the voice of Yahweh our God.