Yeremia 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 19 (Swahili) Jeremiah 19 (English)

Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani; Yeremia 19:1

Thus said Yahweh, Go, and buy a potter's earthen bottle, and [take] of the elders of the people, and of the elders of the priests;

ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia, Yeremia 19:2

and go forth to the valley of the son of Hinnom, which is by the entry of the gate Harsith, and proclaim there the words that I shall tell you;

ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka. Yeremia 19:3

and say, Hear you the word of Yahweh, kings of Judah, and inhabitants of Jerusalem: thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel, Behold, I will bring evil on this place, which whoever hears, his ears shall tingle.

Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia; Yeremia 19:4

Because they have forsaken me, and have estranged this place, and have burned incense in it to other gods, that they didn't know, they and their fathers and the kings of Judah; and have filled this place with the blood of innocents,

nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu; Yeremia 19:5

and have built the high places of Baal, to burn their sons in the fire for burnt offerings to Baal; which I didn't command, nor spoke it, neither came it into my mind:

basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo. Yeremia 19:6

therefore, behold, the days come, says Yahweh, that this place shall no more be called Topheth, nor The valley of the son of Hinnom, but The valley of Slaughter.

Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao. Yeremia 19:7

I will make void the counsel of Judah and Jerusalem in this place; and I will cause them to fall by the sword before their enemies, and by the hand of those who seek their life: and their dead bodies will I give to be food for the birds of the sky, and for the animals of the earth.

Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake. Yeremia 19:8

I will make this city an astonishment, and a hissing; everyone who passes thereby shall be astonished and hiss because of all the plagues of it.

Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha. Yeremia 19:9

I will cause them to eat the flesh of their sons and the flesh of their daughters; and they shall eat everyone the flesh of his friend, in the siege and in the distress, with which their enemies, and those who seek their life, shall distress them.

Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe, Yeremia 19:10

Then shall you break the bottle in the sight of the men who go with you,

na kuwaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika. Yeremia 19:11

and shall tell them, Thus says Yahweh of Hosts: Even so will I break this people and this city, as one breaks a potter's vessel, that can't be made whole again; and they shall bury in Topheth, until there be no place to bury.

Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema Bwana, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi; Yeremia 19:12

Thus will I do to this place, says Yahweh, and to the inhabitants of it, even making this city as Topheth:

na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. Yeremia 19:13

and the houses of Jerusalem, and the houses of the kings of Judah, which are defiled, shall be as the place of Topheth, even all the houses on whose roofs they have burned incense to all the host of the sky, and have poured out drink-offerings to other gods.

Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako Bwana alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote, Yeremia 19:14

Then came Jeremiah from Topheth, where Yahweh had sent him to prophesy; and he stood in the court of Yahweh's house, and said to all the people:

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, kusudi wasiyasikie maneno yangu. Yeremia 19:15

Thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel, Behold, I will bring on this city and on all its towns all the evil that I have pronounced against it; because they have made their neck stiff, that they may not hear my words.