Yeremia 52 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 52 (Swahili) Jeremiah 52 (English)

Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja hapo alipoanza kumiliki; naye akamiliki miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna. Yeremia 52:1

Zedekiah was twenty-one years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem: and his mother's name was Hamutal the daughter of Jeremiah of Libnah.

Naye alitenda yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyatenda Yehoyakimu. Yeremia 52:2

He did that which was evil in the sight of Yahweh, according to all that Jehoiakim had done.

Maana, kwa sababu ya hasira ya Bwana, mambo haya yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata akawaondosha wasiwe mbele za uso wake, naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli. Yeremia 52:3

For through the anger of Yahweh did it happen in Jerusalem and Judah, until he had cast them out from his presence. Zedekiah rebelled against the king of Babylon.

Ikawa, katika mwaka wa kenda wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote. Yeremia 52:4

It happened in the ninth year of his reign, in the tenth month, in the tenth day of the month, that Nebuchadrezzar king of Babylon came, he and all his army, against Jerusalem, and encamped against it; and they built forts against it round about.

Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na mmoja wa mfalme Sedekia. Yeremia 52:5

So the city was besieged to the eleventh year of king Zedekiah.

Katika mwezi wa nne, siku ya kenda ya mwezi, njaa ilizidi sana ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi. Yeremia 52:6

In the fourth month, in the ninth day of the month, the famine was sore in the city, so that there was no bread for the people of the land.

Ukuta wa mji ukabomolewa, watu wote wa vita wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji pande zote;) wakaenda zao kwa njia ya Araba. Yeremia 52:7

Then a breach was made in the city, and all the men of war fled, and went forth out of the city by night by the way of the gate between the two walls, which was by the king's garden; (now the Chaldeans were against the city round about;) and they went toward the Arabah.

Lakini jeshi la Wakaldayo wakamfuatia mfalme, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko, na jeshi lake lote walikuwa wametawanyika na kumwacha. Yeremia 52:8

But the army of the Chaldeans pursued after the king, and overtook Zedekiah in the plains of Jericho; and all his army was scattered from him.

Nao wakamshika mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli, aliyekuwa huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake. Yeremia 52:9

Then they took the king, and carried him up to the king of Babylon to Riblah in the land of Hamath; and he gave judgment on him.

Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake; pia akawaua wakuu wote wa Yuda huko Ribla. Yeremia 52:10

The king of Babylon killed the sons of Zedekiah before his eyes: he killed also all the princes of Judah in Riblah.

Akampofusha macho Sedekia; tena mfalme wa Babeli akamfunga kwa pingu, akamchukua mpaka Babeli, akamtia gerezani hata siku ya kufa kwake. Yeremia 52:11

He put out the eyes of Zedekiah; and the king of Babylon bound him in fetters, and carried him to Babylon, and put him in prison until the day of his death.

Basi katika mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli; Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, aliyesimama mbele ya mfalme wa Babeli, aliingia Yerusalemu. Yeremia 52:12

Now in the fifth month, in the tenth day of the month, which was the nineteenth year of king Nebuchadrezzar, king of Babylon, came Nebuzaradan the captain of the guard, who stood before the king of Babylon, into Jerusalem:

Akaiteketeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. Yeremia 52:13

and he burned the house of Yahweh, and the king's house; and all the houses of Jerusalem, even every great house, burned he with fire.

Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo amiri wa askari walinzi, wakazibomoa kuta zote za Yerusalemu pande zote. Yeremia 52:14

All the army of the Chaldeans, who were with the captain of the guard, broke down all the walls of Jerusalem round about.

Kisha Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua wafungwa baadhi ya watu waliokuwa maskini, na mabaki ya watu walioachwa katika mji, nao wale walioasi na kumkimbilia mfalme wa Babeli, nao mabaki ya vibarua. Yeremia 52:15

Then Nebuzaradan the captain of the guard carried away captive of the poorest of the people, and the residue of the people who were left in the city, and those who fell away, who fell to the king of Babylon, and the residue of the multitude.

Lakini Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawaacha watu walio maskini kabisa ili wawe watunza mizabibu na wakulima. Yeremia 52:16

But Nebuzaradan the captain of the guard left of the poorest of the land to be vineyard keepers and farmers.

Na nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya Bwana, na matako ya bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Bwana, Wakaldayo walivivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli. Yeremia 52:17

The pillars of brass that were in the house of Yahweh, and the bases and the brazen sea that were in the house of Yahweh, did the Chaldeans break in pieces, and carried all the brass of them to Babylon.

Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote. Yeremia 52:18

The pots also, and the shovels, and the snuffers, and the basins, and the spoons, and all the vessels of brass with which they ministered, took they away.

Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, amiri wa askari walinzi akavichukua. Yeremia 52:19

The cups, and the fire pans, and the basins, and the pots, and the lampstands, and the spoons, and the bowls-that which was of gold, in gold, and that which was of silver, in silver,-the captain of the guard took away.

Nguzo mbili, bahari moja, na ng'ombe kumi na mbili za shaba zilizokuwa chini ya matako yake, ambavyo mfalme Sulemani aliifanyia nyumba ya Bwana; shaba ya vitu hivyo vyote ilikuwa haiwezi kupimwa kwa kuwa nyingi sana. Yeremia 52:20

The two pillars, the one sea, and the twelve brazen bulls that were under the bases, which king Solomon had made for the house of Yahweh. The brass of all these vessels was without weight.

Na nguzo hizo, urefu wa nguzo moja ulikuwa dhiraa kumi na nane, na uzi wa dhiraa kumi na mbili ungeweza kuizunguka; na unene wake ulikuwa nyanda nne; nayo ilikuwa ya uvungu. Yeremia 52:21

As for the pillars, the height of the one pillar was eighteen cubits; and a line of twelve cubits did compass it; and the thickness of it was four fingers: it was hollow.

Nayo ilikuwa na kichwa cha shaba juu yake; na urefu wa kichwa kimoja ulikuwa dhiraa tano; palikuwa na mapambo ya wavu na makomamanga juu ya kichwa hicho pande zote; vyote vilikuwa vya shaba; nayo nguzo ya pili ilikuwa na mapambo kama hayo, na makomamanga. Yeremia 52:22

A capital of brass was on it; and the height of the one capital was five cubits, with network and pomegranates on the capital round about, all of brass: and the second pillar also had like these, and pomegranates.

Palikuwa na makomamanga tisini na sita katika pande zake; makomamanga; yote yalikuwa mia juu ya wavu huo pande zote. Yeremia 52:23

There were ninety-six pomegranates on the sides; all the pomegranates were one hundred on the network round about.

Naye amiri wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watatu wa mlango; Yeremia 52:24

The captain of the guard took Seraiah the chief priest, and Zephaniah the second priest, and the three keepers of the threshold:

na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji. Yeremia 52:25

and out of the city he took an officer who was set over the men of war; and seven men of those who saw the king's face, who were found in the city; and the scribe of the captain of the host, who mustered the people of the land; and sixty men of the people of the land, who were found in the midst of the city.

Na Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawatwaa, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. Yeremia 52:26

Nebuzaradan the captain of the guard took them, and brought them to the king of Babylon to Riblah.

Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake. Yeremia 52:27

The king of Babylon struck them, and put them to death at Riblah in the land of Hamath. So Judah was carried away captive out of his land.

Watu hawa ndio wale ambao Nebukadreza aliwachukua mateka; katika mwaka wa saba, Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu; Yeremia 52:28

This is the people whom Nebuchadrezzar carried away captive: in the seventh year three thousand twenty-three Jews;

katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza aliwachukua toka Yerusalemu watu mia nane na thelathini na wawili; Yeremia 52:29

in the eighteenth year of Nebuchadrezzar he carried away captive from Jerusalem eight hundred thirty-two persons;

katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita. Yeremia 52:30

in the three and twentieth year of Nebuchadrezzar Nebuzaradan the captain of the guard carried away captive of the Jews seven hundred forty-five persons: all the persons were four thousand and six hundred.

Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. Yeremia 52:31

It happened in the seven and thirtieth year of the captivity of Jehoiachin king of Judah, in the twelfth month, in the five and twentieth day of the month, that Evilmerodach king of Babylon, in the [first] year of his reign, lifted up the head of Jehoiachin king of Judah, and brought him forth out of prison;

Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli. Yeremia 52:32

and he spoke kindly to him, and set his throne above the throne of the kings who were with him in Babylon,

Naye akabadili mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake. Yeremia 52:33

and changed his prison garments. [Jehoiachin] ate bread before him continually all the days of his life:

Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme wa Babeli; kila siku alipewa posho hata siku ya kufa kwake, siku zote za maisha yake. Yeremia 52:34

and for his allowance, there was a continual allowance given him by the king of Babylon, every day a portion until the day of his death, all the days of his life.