Yeremia 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 14 (Swahili) Jeremiah 14 (English)

Neno la Bwana lililomjia Yeremia, katika habari ya ukosefu wa mvua. Yeremia 14:1

The word of Yahweh that came to Jeremiah concerning the drought.

Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea; Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu. Yeremia 14:2

Judah mourns, and the gates of it languish, they sit in black on the ground; and the cry of Jerusalem is gone up.

Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji; Nao hufika visimani wasione maji; Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao. Yeremia 14:3

Their nobles send their little ones to the waters: they come to the cisterns, and find no water; they return with their vessels empty; they are disappointed and confounded, and cover their heads.

Kwa sababu ya nchi iliyopasuka, Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi, Wenye kulima wametahayarika, Na kuvifunika vichwa vyao. Yeremia 14:4

Because of the ground which is cracked, because no rain has been in the land, the plowmen are disappointed, they cover their heads.

Naam, kulungu naye uwandani amezaa, Akamwacha mwanawe kwa kuwa hapana majani. Yeremia 14:5

Yes, the hind also in the field calves, and forsakes [her young], because there is no grass.

Na punda-mwitu husimama juu ya vilele vya milima, Hutwetea pumzi kama mbwa-mwitu; Macho yao hayaoni sawasawa, Kwa kuwa hapana majani. Yeremia 14:6

The wild donkeys stand on the bare heights, they pant for air like jackals; their eyes fail, because there is no herbage.

Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee Bwana, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi. Yeremia 14:7

Though our iniquities testify against us, work you for your name's sake, Yahweh; for our backslidings are many; we have sinned against you.

Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, hali ya mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu? Yeremia 14:8

You hope of Israel, the Savior of it in the time of trouble, why should you be as a foreigner in the land, and as a wayfaring man who turns aside to stay for a night?

Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyesituka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, Bwana, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache. Yeremia 14:9

Why should you be like a scared man, as a mighty man who can't save? yet you, Yahweh, are in the midst of us, and we are called by your name; don't leave us.

Bwana awaambia watu hawa hivi, Hivyo ndivyo walivyopenda kutanga-tanga; hawakuizuia miguu yao; basi, Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, atawapatiliza dhambi zao. Yeremia 14:10

Thus says Yahweh to this people, Even so have they loved to wander; they have not refrained their feet: therefore Yahweh does not accept them; now will he remember their iniquity, and visit their sins.

Naye Bwana akaniambia, Usiwaombee watu hawa wapate heri. Yeremia 14:11

Yahweh said to me, Don't pray for this people for [their] good.

Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni. Yeremia 14:12

When they fast, I will not hear their cry; and when they offer burnt offering and meal-offering, I will not accept them; but I will consume them by the sword, and by the famine, and by the pestilence.

Ndipo nikasema, Aa, Bwana, MUNGU! Tazama, manabii huwaambia, Hamtauona upanga, wala hamtakuwa na njaa; bali nitawapa amani iliyo thabiti mahali hapa. Yeremia 14:13

Then said I, Ah, Lord Yahweh! behold, the prophets tell them, You shall not see the sword, neither shall you have famine; but I will give you assured peace in this place.

Ndipo Bwana akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao. Yeremia 14:14

Then Yahweh said to me, The prophets prophesy lies in my name; I didn't send them, neither have I commanded them, neither spoke I to them: they prophesy to you a lying vision, and divination, and a thing of nothing, and the deceit of their own heart.

Basi, kwa hiyo Bwana asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, lakini husema, Upanga na njaa havitaingia katika nchi hii; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa. Yeremia 14:15

Therefore thus says Yahweh concerning the prophets who prophesy in my name, and I didn't send them, yet they say, Sword and famine shall not be in this land: By sword and famine shall those prophets be consumed.

Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao. Yeremia 14:16

The people to whom they prophesy shall be cast out in the streets of Jerusalem because of the famine and the sword; and they shall have none to bury them-them, their wives, nor their sons, nor their daughters: for I will pour their wickedness on them.

Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha isiyoponyeka. Yeremia 14:17

You shall say this word to them, Let my eyes run down with tears night and day, and let them not cease; for the virgin daughter of my people is broken with a great breach, with a very grievous wound.

Nikitoka kwenda shambani, tazama, wako huko waliouawa kwa upanga! Na nikiingia mjini, tazama, wamo humo wanaougua kwa sababu ya njaa! Maana nabii na kuhani, wote wawili, huenda huko na huko katika nchi, wala hawana maarifa. Yeremia 14:18

If I go forth into the field, then, behold, the slain with the sword! and if I enter into the city, then, behold, those who are sick with famine! for both the prophet and the priest go about in the land, and have no knowledge.

Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yo yote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu! Yeremia 14:19

Have you utterly rejected Judah? has your soul loathed Zion? why have you struck us, and there is no healing for us? We looked for peace, but no good came; and for a time of healing, and, behold, dismay!

Ee Bwana, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi. Yeremia 14:20

We acknowledge, Yahweh, our wickedness, and the iniquity of our fathers; for we have sinned against you.

Usituchukie, kwa ajili ya jina lako; usikifedheheshe kiti cha enzi cha utukufu wako, kumbuka, usilivunje agano ulilofanya nasi. Yeremia 14:21

Do not abhor [us], for your name's sake; do not disgrace the throne of your glory: remember, don't break your covenant with us.

Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee Bwana, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote. Yeremia 14:22

Are there any among the vanities of the nations that can cause rain? or can the sky give showers? Aren't you he, Yahweh our God? therefore we will wait for you; for you have made all these things.