Yeremia 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 33 (Swahili) Jeremiah 33 (English)

Tena, neno la Bwana likamjia Yeremia mara ya pili, hapo alipokuwa akali amefungwa katika uwanda wa walinzi, kusema, Yeremia 33:1

Moreover the word of Yahweh came to Jeremiah the second time, while he was yet shut up in the court of the guard, saying,

Bwana alitendaye jambo hili, Bwana aliumbaye ili alithibitishe; Bwana ndilo jina lake; asema hivi, Yeremia 33:2

Thus says Yahweh who does it, Yahweh who forms it to establish it; Yahweh is his name:

Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Yeremia 33:3

Call to me, and I will answer you, and will show you great things, and difficult, which you don't know.

Maana Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga; Yeremia 33:4

For thus says Yahweh, the God of Israel, concerning the houses of this city, and concerning the houses of the kings of Judah, which are broken down [to make a defense] against the mounds and against the sword;

Wanakuja kupigana na Wakaldayo, lakini ni kuzijaza kwa mizoga ya watu, niliowaua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu. Yeremia 33:5

while [men] come to fight with the Chaldeans, and to fill them with the dead bodies of men, whom I have killed in my anger and in my wrath, and for all whose wickedness I have hid my face from this city:

Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli. Yeremia 33:6

Behold, I will bring it health and cure, and I will cure them; and I will reveal to them abundance of peace and truth.

Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza. Yeremia 33:7

I will cause the captivity of Judah and the captivity of Israel to return, and will build them, as at the first.

Nami nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu yangu. Yeremia 33:8

I will cleanse them from all their iniquity, by which they have sinned against me; and I will pardon all their iniquities, by which they have sinned against me, and by which they have transgressed against me.

Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo. Yeremia 33:9

[This city] shall be to me for a name of joy, for a praise and for a glory, before all the nations of the earth, which shall hear all the good that I do to them, and shall fear and tremble for all the good and for all the peace that I procure to it.

Bwana asema hivi, katika mahali hapo ambapo mnasema kwamba ni ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, naam, katika miji ya Yuda na katika njia za Yerusalemu, zilizo ukiwa, hazina mwanadamu wala mwenyeji wala mnyama, Yeremia 33:10

Thus says Yahweh: Yet again there shall be heard in this place, about which you say, It is waste, without man and without animal, even in the cities of Judah, and in the streets of Jerusalem, that are desolate, without man and without inhabitant and without animal,

itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni Bwana wa majeshi, maana Bwana ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa Bwana. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema Bwana. Yeremia 33:11

the voice of joy and the voice of gladness, the voice of the bridegroom and the voice of the bride, the voice of those who say, Give thanks to Yahweh of Hosts, for Yahweh is good, for his loving kindness endures forever; [and of them] who bring [sacrifices of] thanksgiving into the house of Yahweh. For I will cause the captivity of the land to return as at the first, says Yahweh.

Bwana wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakizilaza kondoo zao. Yeremia 33:12

Thus says Yahweh of Hosts: Yet again shall there be in this place, which is waste, without man and without animal, and in all the cities of it, a habitation of shepherds causing their flocks to lie down.

Katika miji ya nchi ya vilima, katika miji ya nchi tambarare, katika miji ya Negebu, na katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo karibu na Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mikono yake awahesabuye, asema Bwana. Yeremia 33:13

In the cities of the hill-country, in the cities of the lowland, and in the cities of the South, and in the land of Benjamin, and in the places about Jerusalem, and in the cities of Judah, shall the flocks again pass under the hands of him who numbers them, says Yahweh.

Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda. Yeremia 33:14

Behold, the days come, says Yahweh, that I will perform that good word which I have spoken concerning the house of Israel and concerning the house of Judah.

Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii. Yeremia 33:15

In those days, and at that time, will I cause a Branch of righteousness to grow up to David; and he shall execute justice and righteousness in the land.

Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu. Yeremia 33:16

In those days shall Judah be saved, and Jerusalem shall dwell safely; and this is [the name] by which she shall be called: Yahweh our righteousness.

Maana Bwana asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli; Yeremia 33:17

For thus says Yahweh: David shall never want a man to sit on the throne of the house of Israel;

wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima. Yeremia 33:18

neither shall the priests the Levites want a man before me to offer burnt offerings, and to burn meal-offerings, and to do sacrifice continually.

Neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema, Yeremia 33:19

The word of Yahweh came to Jeremiah, saying,

Bwana asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake, Yeremia 33:20

Thus says Yahweh: If you can break my covenant of the day, and my covenant of the night, so that there shall not be day and night in their season;

ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika. Yeremia 33:21

then may also my covenant be broken with David my servant, that he shall not have a son to reign on his throne; and with the Levites the priests, my ministers.

Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia. Yeremia 33:22

As the host of the sky can't be numbered, neither the sand of the sea measured; so will I multiply the seed of David my servant, and the Levites who minister to me.

Kisha neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema, Yeremia 33:23

The word of Yahweh came to Jeremiah, saying,

Je! Hufikiri neno hili walilolisema watu hawa, wakinena, Jamaa zile mbili alizozichagua Bwana amezitupilia mbali? Hivyo ndivyo wanavyowadharau watu wangu, ili wasiwe taifa tena mbele yao. Yeremia 33:24

Don't you consider what this people has spoken, saying, The two families which Yahweh did choose, he has cast them off? thus do they despise my people, that they should be no more a nation before them.

Bwana asema hivi, Ikiwa agano langu la mchana na usiku halikai imara, ikiwa mimi sikuziamuru kawaida za mbingu na dunia; Yeremia 33:25

Thus says Yahweh: If my covenant of day and night fails, if I have not appointed the ordinances of heaven and earth;

ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu. Yeremia 33:26

then will I also cast away the seed of Jacob, and of David my servant, so that I will not take of his seed to be rulers over the seed of Abraham, Isaac, and Jacob: for I will cause their captivity to return, and will have mercy on them.