Kuna wakati ukinyamaza unakosa baraka
Maana Yesu anataka useme ili atatue shida zako
Mimi sitaki tena mimi kunyamaza nitazitaja tajaa
Shida zangu zote nitamwambia Yesu ili azitatue
Baraka nitasema nibariki nitasema
Na shida nitasema niugue nitasema
Nitasema yote kwako Yesu wangu labda mimi ndiyo batimayo wako leo
Sisikilizi la mtu sibadili mtazamo
Hata wanadamu wanizibe mdomo wakidhani sisitahili mimi ni
Mdhambi
Yanini niuumie moyo hata usijali wakati Yesu upo
Nichekwe nidharauliwe na kusimangwa naamini we upo
Niishi maisha magumu hata usijali wakati Yesu upo
Nikose ka gari na nyumba maisha mazuri naamini we upo.
Nita drive nifagie na kanyumba kangu
Niende benki nihesabu na vipesa vyangu
Nita drive nifagie na kanyumba kangu
Niende benki nihesabu na vipesa vyangu
Majereha unapitia moyo waumia umenyamaza
Kimywa kimywa na hausemi chozi shavuni ni kama chakula
Wajishauri umweleze nani wa kuweza kusitisha
Shida zote maumivu ya dunia hapa hapa chini ya jua
Sina pesa nitasema chakula nitasema
Mawazo nitasema kuonewa nitasema
Nitasema yote yote kwako Yesu wangu labda mimi ndiyo zamu zamu yangu leo
Nakuamini ni wewe wakuamua ni wewe
Hata wanadamu watadhani baba umeniacha kumbe ni jaribu la mda tu
Yanini niuumie moyo hata usijali wakati Yesu upo
Nichekwe nidharauliwe na kusimangwa naamini we upo
Niishi maisha magumu hata usijali wakati Yesu upo
Nikose ka gari na nyumba maisha mazuri naamini we upo.
Nita drive nifagie na kanyumba kangu
Niende benki nihesabu na vipesa vyangu
Nita drive nifagie na kanyumba kangu
Niende benki nihesabu na vipesa vyangu