Lyrics
Verse 1
Ndoa ni kwanza kuelewana, sio fujo, mateke na ngumi
Ndoa ni kwanza kusikizana, sio uwanja wa mapambano
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Chorus
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, furaha ya moyo
Verse 2
Nawaomba msigombane tena, na ndoa yenu msilie tena
Uliyempata leo ndiye kipenzi chako
Si unajua mmekubaliana kweli ni kwamba nyinyi mnapendana
Ndio maana tumekuja leo tumalize jambo lenu
Verse 3
Hivi unajua ilikuwaje mpaka huyo Eva apatikane?
Huyo Eva alitoka kwenye ubavu, ubavu wa mwanaume
Adam kasema sasa huyu ni mifupa katika mifupa yangu
Na nyama katika nyama yangu, ataitwa mwanamke
Kwa hiyo sasa huyo mwanaume atamwacha baba yake
Atamwacha baba yake na mama yake tena
Aambatane na mkewe wakaishi kwa furaha
Watakuwa mwili mmoja, wataishi pamoja
Verse 4
Hivi unajua ilikuwaje yupi harusi apatikane?
Bwana harusi hakika amepambana ampate kipenzi chake
Twaombea mkafurahi, vicheko, utani na raha nyingi
Watu wote leo tuko hapa tumalize jambo lenu
Chorus
Ndoa kwanza kuelewana, sio fujo na ngumi
Ndoa kwanza kusikizana, sio uwanja wa mapambano
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Verse 5
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, furaha ya moyo wako
Watu wamekuja kuwapa mti, ndugu na rafiki
Wote wamefurahi kuwa hapa kwa ajili yenu
Basi sasa msipigane, mpendane, mchukuliane
Mbebane, mvumiliane, ndoa ni kufichiana siri
Ugomvi na hasira hasira msifanye
Mueleweshane kwa upole, majibu mazuri kuupalilia upendo
Verse 6
Hapo sasa sisi tumeridhika, taratibu zote mmezifuata
Kama vile Bwana Mungu aliagiza tufunge ndoa takatifu
Kikubwa sasa twaombea Mungu awape maisha marefu
Yenye baraka, furaha, pia upendo katika nyumba yenu
Chorus
Basi sasa msipigane, mpendane, mchukuliane
Mbebane, mvumiliane, ndoa kufichiana siri
Ugomvi na hasira hasira, mbebane
Mueleweshane kwa upole, majibu mazuri upalilia upendo
Bridge
Usimpige mkeo, utakuwa wajipiga mwenyewe
Maana sasa nyinyi ni mwili mmoja
Asipoumia mwili, atakuwa ameumia moyo
Na wewe pia utajiumiza moyo, furaha hukosekana ndoani
Final Chorus
Kwanza kuelewana, sio fujo na ngumi
Ndoa kwanza kusikizana, sio uwanja wa mapambano
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Huyo ndiye wako, kipenzi cha moyo wako
Umtunze mkeo, umpende mmeo
Jivunie chako, furaha ya moyo yako
Credits & Song Information
Video
Meaning & Inspiration
A wedding-focused song about building marriage through mutual understanding, patience, gentleness, and care. It addresses both spouses, warns against violence and destructive conflict, and presents marriage as a committed partnership in which the couple supports one another.