Sifa Lyrics

Usiniache by Zabron Singers cover art

Zabron Singers - Usiniache Lyrics

Artist:
Zabron Singers

Lyrics

Sitaki kuwa wa hivi hivi mimi 


Kuipenda dunia nikaikosa mbingu 


Kuwa vumbi la jibu kwa watakatifu 


Litakalo kanyagwa na washindi wa dhambi


Duniani mbingu tuwe wote 


Mbali ulikonitoa usiniache 


Ikiwa umeniheshimisha hapa chini 


Yesu akija ruhusu niende na yeye 


Ninafurahi kuona vile unanijali 


Nikiwa mdogo mkubwa uko na mimi 


Kwenye vikwazo vitisho umekuwa na mimi 


Mchana usiku bega kwa bega uko na mimi 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


Baba tangu ni mdogo mdogo 


Umekuwa nami siku zote 


(Umenibariki na vingi ukanisamehe mengi)


Baba ukinibariki nikumbushe nisikusahau 


(Nia yangu unimiliki Baba)


Baba unapo mpango pale Yerusalemu 


(Jana leo hata kesho)


unikumbuke niwe pale 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


Siku zote


Lutu alikata kubaki hivyo hivyo 


Kakataa kupenda uovu wa Sodoma 


Katikati ya mji wa uovu wa dhambi 


Kwa uaminifu akamuakilisha Mungu 


Naomba nami niwe mtumwa mwaminifu 


Niwakilishe vyema jina la Yesu 


Hata kama dunia ikithiri uovu 


Ruhusu nisimame nikutetee


Na siku ile mwokozi wangu atakaporudi 


Aseme vyema wewe ni mtumishi mwema 


Kisha nipae nipae mawinguni na Yesu 


Kuanzisha familia mpya na Mungu 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


Baba tangu ni mdogo mdogo 


Umekuwa nami siku zote 


(Umenibariki na vingi ukanisamehe mengi)


Baba ukinibariki nikumbushe nisikusahau 


(Nia yangu unimiliki Baba)


Baba unapo mpango pale Yerusalemu 


(Jana leo hata kesho)


unikumbuke niwe pale 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


(Usiniache Mungu wangu) Baba 


Siku zote


Video