Nimeachilia Lyrics - Ambwene Mwasongwe

Ambwene Mwasongwe swahili

Chorus:
Eeh
Nimeachilia
jifunze kuambia moyo wako
Nimeachilia
hatakama inauma sana jifunze kusema
Nimeachilia
Nimesamehe Mungu anaona mimi
Nimeachilia

Nimeachilia Video

Buy/Download Audio

Nimeachilia Lyrics

Ulipanda mti mzuri ukategemea kuvuna matunda
ila mti wenyewe umezaa miiba na michongoma 
Uliwekeza muda na mali,ukamwagilia ukitarajia 
matarajio yamekuwa sio sasa umebaki na maumivu
japokuwa uliiona miiba,ulijipa muda ukapogolea
ukitarajia mabadiliko,labda kesho mti utazaa
sasa imekuwa kinyume,mti wako mwenyewe unakuchoma 

Unalia
Aaah ah
ukikumbuka Mbegu 
Aaah ah
Unalia
Aaah ah
ukikumbuka maji
Unalia
Aaah ah
ukikumbuka kazi
Aaah ah

Sio kila kinachokuja kwako ni chako
na si kiondokacho kwako ni chako
hata kama unavipenda sio vyako 
vingine mungu huviondoa, ili wewe ubaki salama
iwe kazi,nafsi,mahusiano au cheo 
japo vyaondoka kwa maumivu ili jifunze kuacha viende
nafasi ya moyo wako mpe mungu

Chochote kile kikuumizacho kufikia hatua ya kukuua
jua ulikikalisha mahali pa mungu 
jifunze kukiacha kiende,jifunze kusema Bye Bye
maana sio vyote vya kwako

Walitoka kwetu hawakuwa wa kwetu
maana wangelikuwa wetu wangelikaa nasi
walitoka ili wafunuliwe sio wote wa kwetu

Walitoka kwetu hawakuwa wa kwetu
maana wangelikuwa wetu wangelikaa nasi
wafunuliwa ili tujue sio wote wa kwetu

Eeh 
Nimeachilia 
jifunze kuambia moyo wako 
Nimeachilia
hatakama inauma sana jifunze kusema
Nimeachilia
Nimesamehe Mungu anaona mimi 
Nimeachilia

Tafuta mahali kaa pekee Yako Mahali Hakuna akuonaye
Mahali pa siri pa utulivu,mahali hakuna akusikiaye
ukakumbuke machungu yako,maumivu yako na machozi yako
kayakumbuke maneno yote yakuumizayo moyo wako
kayakumbuke vitu ulivyopoteza,kayakumbuke muda na watu wa karibu 
kakumbuke hasara uliyopata,usiyasahau machungu yote

Lia usibakishe machozi 
lia usiyameze yeyote
toa yanayousibu moyo
toa yasibakiye yeyote
Aaaah ah ah ah aaah ah
toa usibaki na machungu
hakikisha umetuliza moyo,umesahau yote yaliyopita 
achilia yote uloshikilia waache waende sio Riziki yako
hakikisha umekuwa mwepesi ji-edit,moyo ubaki salama

Inuka sema kwa ujasiri 
Nimeachilia ninaanza upya
Inuka jikung'ute mavumbi ya kale
yamepita sasa ni mapya 
Nimeachilia sema
Nimeachilia
Nimesamehe yote
Nimeachilia
Nimejinyonyoa manyoya ya kale sasa ni mwepesi
Nimeachilia 
Sasa niko Huru
Aah ah aah aaah aah
Nimeachilia 

Nimesamehea sasa ninayo amani Ooh oh o
maumivu ya kale nimeacha nyuma 
Nimeachilia