Ambwene Mwasongwe - Unikumbuke Lyrics

Album: Unikumbuke - Single
Released: 06 Aug 2021
iTunes Amazon Music

Lyrics

Nimekuita uambie watu ushuhuda wangu Miaka tisa nimekaa jela Nilifungwa kwa kosa la kusingiziwa Namshukuru Mungu nimetoka

Usiku ule nilikamatwa kama mchezo Na mke wangu na mtoto mdogo Nikadhani labda walikuwa wanatania Labda ilikuwa siku ya wajinga

Hakuna mtu alielewa ukweli wa ushahidi wangu Wala sikuwa na wakumweleza akanielewa Mazingira ya kesi, ushahidi, sheria za kazi Siri ni ban, mpaka mke wangu kaniambia Kama umefanya kiri kosa tujue moja

Nikumbuke, kumbuka haki yangu, sikufanya ubaya Nikumbuke, nikumbuke, sikufanya ubaya Nikumbuke, namna walivyonishtaki kwa hila na wivu Nikumbuke, bwana unikumbuke nililia

Hey, kumbuka bwana haki yangu Hey, wakumbuke, walivyo kufanikiwa jela Uwakumbuke, Mungu wakumbuke washa mshumaa ndani ya nyumba Mkumbuke mtoto mchanga asiye na hatia Uwakumbuke, kama ningekuwepo angekonda Kumbuka Adam, aliyebaki, alikufanya kushtuka kwa ajili yako

Nilidhani Mungu kalisahau faili langu Nikadhani kwamba nitaaibika Sikuwa tena na tumaini lililobaki Haki yangu ilikuwa tumaini pekee

Waweza elewa shahidi wangu alikuwa Mungu Labda na wale walioua Mwisho wa siku Mungu alinitetea Na waliofanya kosa kunikana

Haki yangu ikasitana kama mtende na mwelezi Pale banoni, walinichimba wakuning'oa sababu ya Mungu Waliinamisha wakunivunja, walinitikisa sikupukutika Walinichuma ili niishe Wewe bwana ulinitetea na haki yangu

Nikumbuke, kumbuka maadui walivyonizunguka Nikumbuke, kumbuka ushahidi wa maneno yao Nikumbuke, kumbuka walivyonichafua jina langu Nikumbuke, kumbuka walivyoniona  Mi ni mhalifu, hey ukalisafishe jina langu

Hey bwana, uwakumbuke! Uwakumbuke Ukarehemu makosa yao Uwakumbuke! Japo walifanya ubaya bwana na uwasamehe Uwakumbuke! Nilienda jela nikiwa bado sikujui Uwakumbuke! Nimetoka nimeokoka nimekujua Nikumbuke! Bwana unikumbuke usinisahau

Natengeza fadhili zako, niimbe Mungu baba Nimefurahi, niimbe Mungu bwana Nimefurahi, niimbe Mungu bwana Nimefurahi, niimbe Mungu bwana Nimefurahi, niimbe Mungu bwana

Video

Ambwene Mwasongwe - Unikumbuke (Official Music Video)

Thumbnail for Unikumbuke video
Loading...
In Queue
View Lyrics