Ambwene Mwasongwe - Utoshefu Lyrics
Lyrics
Nimejifunza kuwa radhi, katika hali yeyote niliyonayo Najua kudhiriwa, tena na kufanikiwa katika hali yeyote Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa, nayaweza yote kwa anitiaye nguvu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Furahini siku zote katika bwana Tena nasema ndugu zangu furahini Upole wenu ujulikane na watu wote Bwana yu karibu kuja Furaha niliyonayo, ni tunda la roho furaha hiyo hailetwi na vitu Sisubiri nipewe ili nifurahi, nafurahi hata kwenye mateso Upole nilionao, umetoka kwa roho hautegemei ninavyotendewa Amani ya Kristo imenitawala ndani naimba wimbo wakati wa shida Imenihifadhi moyo na nia yangu ninayapenda mambo ya staha Haki, usafi kupendeza na sifa njema Ukiwepo wema wowote nautafakari, nafurahi Nimehuishwa fikra zangu, nafurahi Nimeridhika na utauwa kwa bwana
Upendo wa dunia hii una sababu Sababu hizo zikiisha huisha Upendo huo ni wa nipe nikupe Vitu vikienda na upendo umeenda Furaha ya dunia hii ni ya sababu Ukivikosa vitu inaisha Amani ya dunia hii ni ya sababu Hetengenezwa na mazingira yasiyodumu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu Utauwa, na kuridhika vimenipa utoshefu
Nitawapenda watu tena nitawaamini Ntakupenda zaidi wewe usiyeumiza Nitafurahi tena nitatabasamu na kuwainyesha mwanya ila sitawapa moyo Moyo hadanganya Nitaukabidhi kukupa wewe uliyeuumba, moyo huua Sitalpa mtu maana haujui Watu wanatibu ila wewe waponya, wao hunenepesha ila wewe unawandisha Japo twaanguka twaumia, twateseka tunalia Wewe bwana ni faraja yetu, nimeridhika Na utauwa umenipa kutosheka, nimeridhika Nimekupa moyo wangu utawale Nimejifunza kuwa radhi, katika hali yeyote niliyonayo Najua kudhiriwa tena na kufanikiwa katika hali yeyote Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa Nayaweza yote kwa anitiaye nguvu Nimejifunza kuwa radhi katika hali yeyote niliyonayo Najua kudhiriwa tena na kufanikiwa katika hali yeyote Na katika mambo yeyote nimejifunza kushiba na kuona njaa Nimejifunza kuwa na vingi na kupungukiwa Nayaweza yote kwa anitiaye nguvu
Video
AMBWENE MWASONGWE_UTOSHEFU LYRICS