Natasha Lisimo - Umwema Lyrics
Lyrics
Hey yeah yeah .... Wewe ni mwema
Niliyovuka ni mengi Siwezi tazama nyuma Kwa visa vingi vitimbwi Aaai, asante Baba
Si kwa akili zangu Wala nguvu zangu mwenyewe Wewe ni mwema Umenuivusha na mengi magumu Yanayoelezeka na yasiyoelezeka Umenifuta maumivu Ukanipa amani
Wa ajabu, fahari yangu Mtetezi wangu, wewe ni mwema Mwalimu wangu, shujaa wangu Kiongozi wangu wewe ni Baba
Oooh oooh ...umenikunguta mavumbi wewe ni mwema Oooh oooh ...umenipandisha pandisha wewe ni Baba Oooh oooh ...umenifanya chombo cha sifa kwa walimwengu Oooh oooh ...umenipandisha pandisha wewe ni mwema
Ungetazama vyeo Uzuri na mali mimi ningekuwa wapi? Kiukweli upendo wako hauna kipimo Umenipenda bure Kwa kupigwa kwako mimi nimepona Neema yako ya kweli ya ajabu
Umenifanya mwanao Ukanipa uzima na afya Umenifuta maumivu (eh) ukanipa amani Wa ajabu, fahari yangu Mtetezi wangu, wewe ni mwema Mwalimu wangu, shujaa wangu Kiongozi wangu wewe ni baba
Oooh oooh ...umenikunguta mavumbi wewe ni mwema Oooh oooh ...umenipandisha pandisha wewe ni Baba Oooh oooh ...umenifanya chombo cha sifa kwa walimwengu Oooh oooh ...umenikunguta mavumbi wewe ni mwema
Wewe ulikuwa mwanzo Na bado utabaki kuwa mwisho Kwenye utata na vikwazo Bado utabaki sukuhisho
Wewe ni taa na mwanga Humulika popote palipo na giza Maana hakuna jambo gumu ambalo wewe bwana unashindwa
Umenipa amani (aaah hey) Umenipa furaha(aah hey) Jemedari (aah hey) Yesu nakupenda
Umenipa uzima (aaah hey) Umenipa heshima(aah hey) Yesu weeeh (aah hey) Bwana nakusifu
Oooh oooh ...umenikunguta mavumbi wewe ni mwema Oooh oooh ...umenipandisha pandisha wewe ni Baba Oooh oooh ...umenifanya chombo cha sifa kwa walimwengu Oooh oooh ...umenipandisha pandisha wewe ni mwema
Video
Natasha Lisimo UMwema