Mungu umenihurumia
Baba umenihurumia
Yesu umenihurumia
Baba umenihurumia
Nakumbuka maumivu
Nakumbuka na machozi
Ulionifuta wewe
Nilivyosetwa na watesi wangu
Asante kwa ujasiri
Nashukuru kwa amani Yesu
Uliyoweka moyoni
Nilivyotingwa na ya walimwegu
Aibu, aibu, aibu
Fedheha fedheha, fedheha
Umeniondolea aibu
Sijui nikulipeje? Ooh Bwana
Aaah, umeniona nami, umeniona na mimi
Ehee, umeniona nami, umeniona na mimi
Aaah, umeniona nami, umeniona na mimi
Ehee, umeniona nami, umeniona na mimi
Wala sikuwa dhamani
Kama nilivyoonekana
Na nilishachoka
Kuendelea tena mbele
Siri yangu yote
Ukaijua wewe Bwana
Nawaza kama angelijua mwengine
Angeshatangaza je?
Nashukuru kwa kuniondolea aibu
Sijui nikulipeje?
Ooh kama je, isingekuwa huruma yako
Angenipendaga nani?
Yaani we, isingekuwa rehema zako
Ningekumbukwa na nani?
Ah tumaini langu ni wewe
Toka siku zile
Msaada wangu ni wewe
Toka siku zile
Ooh kimbilio langu ni wewe
Toka siku zile
Msaada wangu wa mwisho ni wewe Yesu
Toka siku zile
Aaah, umeniona nami, umeniona na mimi
Ehee, umeniona nami, umeniona na mimi
Aaah, umeniona nami, umeniona na mimi
Ehee, umeniona nami, umeniona na mimi
Umeniona, umeniona na mimi
Na mimi iyee iyee
Umenilipia deni la aibu
Umeniponya yote tabibu
Nini tena hujafanya mwalimu
Oooh asante, ooh
Umenilipia deni la aibu
Umeniponya yote tabibu
Nini tena hujafanya mwalimu
Oooh asante, ooh