Sifa Lyrics

Yesu ni Muweza by Yusto Onesmo cover art

Yusto Onesmo - Yesu ni Muweza Lyrics

Artist:
Yusto Onesmo

Lyrics

Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaaah aweza Yote,
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaah aweza Yote,

Siku moja bwana Yesu kwa uweza njiani alikemea mti ukanyauka
watu wote walioliona tendo hili la ajabu wakashangaa,
vilevile alikemea thoruba bahari ikatulia
pia aliwaponya wagonjwa na kuwafufua wafu watu wakashangaa
ndivyo itakavyo kuwa leo hii bwana yesu akianza kushugulika, kuondoa matatizo mbalimbali uliyo nayo, utafurahi na kushangilia

Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaaah aweza Yote,
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaah aweza Yote.

Hatakama daktari alishakukatisha tamaa hutapona,
bwana yesu anaweza kukuponya leo ukafurahi na kushangilia,
kama ni matatizo ya ndoa au kiuchumi, Yesu ni muweza
kama ni masomo darasani au biashara, Bwana yesu anainua. aaaah

Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaaah aweza Yote,
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaah aweza Yote

Bibilia inaeleza habari ya zakayo, aliyepanda mkuyuni
kwa kuwa bwana yesu ni muweza, akatambua mawazo yake
kwa upendo akamwita kwa Jina, "Zakayo shuka" akashuka
siku iyo akawa wa neema kwa Bwana yesu akapata wokovu
Basi leo anakuita kwa jina, shuka upesi
akuchongechonge, akufanye apendevyo yeye iyee

Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaaah aweza Yote,
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaah aweza Yote
{bridge}
Oh Yesuuu
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaaah aweza Yote,
Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, Yesu ni muweza, aaah aweza Yote

JESUS IS ABLE, JESUS IS ABLE, JESUS IS ABLE, HE IS ABLE OF ALL THINGS.
@Yusto Onesmo -YESU NI MUWEZA

Video